Janja mpya ya trafik 'kupiga pesa' hii hapa!

Janja mpya ya trafik 'kupiga pesa' hii hapa!

Madereva na wadau wengine napenda kuwataadharisha.

Mnapotumia barabara, zingatieni vile vibao vya speed limit vilivyowekwa.
Sasa hivi wazee wa kitochi wamekuja na mbinu mpya.. Yale maeneo ambayo yana vibao vya speed limit anajificha kamanda na tochi yake.

We ukipita pale si unaona hakuna trafik! Basi unaongeza mwendo. sasa hapo yule mwenye tochi aliyejificha anakumulika na kuwatumia taarifa za gari yako na speed trafik aliyeko mbele.

We ukifika unashangaa umesimamishwa na kusomewa madhambi yako.. Hapo sasa lazima thelasini ikutoke.

So cha muhimu unapopita kwenye kibao cha hamsini uwe hamsini kweli hata kama huoni kofia nyeupe, we zingatia tu sheria bila shuruti.. Ni hayo tu....
Hatari sana
 
Back
Top Bottom