Janja mpya ya trafik 'kupiga pesa' hii hapa!

Madereva na wadau wengine napenda kuwataadharisha.
Mnapotumia barabara, zingatieni vile vibao vya speed limit vilivyowekwa.
Sasa hivi wazee wa kitochi wamekuja na mbinu mpya.. Yale maeneo ambayo yana vibao vya speed limit anajificha kamanda na tochi yake.
We ukipita pale si unaona hakuna trafik! Basi unaongeza mwendo. sasa hapo yule mwenye tochi aliyejificha anakumulika na kuwatumia taarifa za gari yako na speed trafik aliyeko mbele.
We ukifika unashangaa umesimamishwa na kusomewa madhambi yako.. Hapo sasa lazima thelasini ikutoke.
So cha muhimu unapopita kwenye kibao cha hamsini uwe hamsini kweli hata kama huoni kofia nyeupe, we zingatia tu sheria bila shuruti.. Ni hayo tu....
hii tumeshaizoea. tunasoma vibao sana siku hizi....
 
Sasa wanapigaje pesa wakati wewe ndio uliovunja sheria? Hivi sisi waafrica tuna matatizo gani!
 
Kwahiyo nia ya Traffic ni kukusanya mapato hata kwa njia haramu na sio kuwasaidia madereva kufuata sheria?
 
Mh Rais alishasema trafiki akichukua 5000 ya kubrash viatu siyo mbaya!
 
Tatizo, kwa ushuhuda wa kwao wenyeweTraffic siku moja walinikamata idodomya halaf wakanigandisha toka saa tano asubui hadi SAA 9 wao wenyewe( wakike) wanakwambia huwa wanatoa hela kupangiwa sehemu korofi, zenye mpunga, yaani hapo Uk kamatwa hutoki hivihivi. Mfano ni mizani pale idodomya.
 
Ni upumbavu kuendesha gari bila kuzingatia sheria

Tena ni upumbavu uliopitiliza, inaonekana huyu mleta mada hajasafiri siku.nyingi, hii teknology imekuwa ikifanya kazi kwa muda mrefu sana sasa lakini yeye anaonankama ni mbinu mpya
 
Kwa nini naye trafik ajifiche kwani kujifiicha ndio sheria? Hata wenyewe wanafanya makosa hakuna sheria ya barabarani inayomwambia askari ajifiche ili akamate waendao speed kubwa.
Sababu ya kuvaa nguo nyepe sio unadhifu bali kila mtumiia barabara amuone askarii kwa urahisi. Sasa kujifiicha ni kanuni ya wapi na yangapi katika usalama barabarani?
Kinachotokoea wakatii mwingine unakamatwa hata haukuwa speed au mlikuwa mnaongozana magari matatu wewe katikati unakamatwa peke yako.

NB: Madereva mbinu pekee ya kushinda hili suala ni kufuata sheria. Hata sehemu isiyo na kibao usmwage moto tu mpaka 150 huko!. jua nchi yetu speed yake ni ngapi? ndio tembelea hiyo.

Anapojificha inakuwa ni kama kile kibao kimekukamata ukiover speed kwa maneno mengine ni kuwa kama hizo kamera zingekuwa haziwezi kuhujumiwa, basi zingekuwa fixed kwenye maeneo husika
 
Kuna barabara moja inaelekea kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, kutokea barabara ya Ali Hassan, kumbe ni one way lakini hakuna alama.

Nimeingia kufika mbele kidogo Askari akanikamata akanambia magari yanaingia lakini hayatoki, akataka kuniandikia nikagoma nikamuuliza nitajuaje kuwa ni one way wakati hakuna halama? Akasema alama ilikuwepo ila imeharibika.
Nikamwambia apande gari twende nitalipia huko kituoni halafu ajieleze kwa mkubwa wake kwanini kibao kimeharibika hajatoa taarifa kiwekwe kipya.

Jamaa kusikia hivyo akanifukuza niondoke eti najifanya mjanja wa kuzijua sheria za barabara.
 
Madereva na wadau wengine napenda kuwataadharisha.

Mnapotumia barabara, zingatieni vile vibao vya speed limit vilivyowekwa.
Sasa hivi wazee wa kitochi wamekuja na mbinu mpya.. Yale maeneo ambayo yana vibao vya speed limit anajificha kamanda na tochi yake.

We ukipita pale si unaona hakuna trafik! Basi unaongeza mwendo. sasa hapo yule mwenye tochi aliyejificha anakumulika na kuwatumia taarifa za gari yako na speed trafik aliyeko mbele.

We ukifika unashangaa umesimamishwa na kusomewa madhambi yako.. Hapo sasa lazima thelasini ikutoke.

So cha muhimu unapopita kwenye kibao cha hamsini uwe hamsini kweli hata kama huoni kofia nyeupe, we zingatia tu sheria bila shuruti.. Ni hayo tu....
Hiyo wala si Mbinu Mpya Kamanda wa Traffics Police alisema kabisa kuwa mwenye camera hatovaa uniform na anaweza hata kuwa anaendesha baiskeli na ukifanya kosa anakupiga picha na anaituma kwa askari mbele ya safari unakamatwa... Tiini Sheria acheni mambo ya utawala wa Nne...
 
Trafiki mjanja anatumia memory card yake kwenye ile tochi badala ya memory card ya serikali iliyomo kwenye tochi. Kabla hajaanza kupiga tochi anachomoa memory card ya serikali anaweka yake, akimaliza kazi anarudishia ile ya serikali. Serikali inakosa ela traffic analainisha ugumu wa maisha na ela za kubrashi viatu!
 
Kwa mfano wapi? Na umejuaje kama kilikuwepo kikaibwa?
Dar-Moro kuna sehemu nyingi tu havipo! Sehemu kadhaa kati ya Mlandizi na Chalinze. Naitumia hiyo njia kwa zaid ya miaka 20 sasa najua wapi vilikuwapo na sasa havipo. Kama havijaibwa basi vimeota miguu!
 
Leo ni
utii wa sheria bila shuruti ,mashine za tra kwa jeshi la polisi zianze kazi mikoa yote ikiwamo moshi ,Arusha na mingine kusiwe na sababu yeyote ya kuzuia hili ,utaratibu wa vitabu uwekwe kando hauna uadilifu.
Leo Traffic Police ananiuliza risiti ya petrol!!! Hii ni baada ya kutoka pale petrol station ya junction ya pugu road na chang'ombe road nikashangaa badae nikajua alidhani nimetanua kwa kuunganisha petrol station kuingia barabara kuu. Hv sheria inasenaje hapo?
 
Dar-Moro kuna sehemu nyingi tu havipo! Sehemu kadhaa kati ya Mlandizi na Chalinze. Naitumia hiyo njia kwa zaid ya miaka 20 sasa najua wapi vilikuwapo na sasa havipo. Kama havijaibwa basi vimeota miguu!
Sikiliza babuu, achana na janja janja na michezo ya kuigiza. Njia unayoitumia kila siku huwezi kuishia kutaja DAR - Moro. Kwa kifupi ni hivi: hakuna askari anaweza kukukamata ikiwa kibao hakipo. Speed Radar inawekwa sehemu zenye makatazo na zisizo na makatazo.

Kukosekana kwa kibao haimaanishi kuwa dereva ataendesha kasi aitakayo (mfano 190KpH), hilo ni kosa. Cha msingi ni kuzingatia sheria kwa manufaa yako, jamii yako na Taifa.
 
Leo ni

Leo Traffic Police ananiuliza risiti ya petrol!!! Hii ni baada ya kutoka pale petrol station ya junction ya pugu road na chang'ombe road nikashangaa badae nikajua alidhani nimetanua kwa kuunganisha petrol station kuingia barabara kuu. Hv sheria inasenaje hapo?
Bila shaka kwa hayo ulioandika kwenye bold unaonekana unafahamu fika kuwa kutanua ni kosa. Au sheria ya nini unauliza?
 
Kwa kifupi ni hivi: hakuna askari anaweza kukukamata ikiwa kibao hakipo. Speed Radar inawekwa sehemu zenye makatazo na zisizo na makatazo.
Duh...wewe ni wa wapi ndugu? Mtanzania? I can bet hujawahi kuendesha gari ukapambana na hao watu. Ni mazingira ya kupiga pesa tu. Hii nchi 'inanuka' rushwa (to be polite).

NB: Sisemi kuwa madereva wote ni watu wema na wanafuata sheria. Wengi ni vimeo.
 
You are right, sijawahi kupambana nao. Ili upambane na polisi lazima uwe na makosa, otherwise hamtapambana, ni suala la wewe kukana na kuendelea na safari yako.

Mtu umekamatwa kuwa umeoverspeed, unaoneshwa na ushahidi wa picha ya gari lako likiwa linanyuka mwendo kinyume na sheria, kuna haja ya mapambano?

Mwendo kasi unaua. Zingatia sheria za usalama barabarani, okoa maisha na mali
 
Madereva na wadau wengine napenda kuwataadharisha.

Mnapotumia barabara, zingatieni vile vibao vya speed limit vilivyowekwa.
Sasa hivi wazee wa kitochi wamekuja na mbinu mpya.. Yale maeneo ambayo yana vibao vya speed limit anajificha kamanda na tochi yake.

We ukipita pale si unaona hakuna trafik! Basi unaongeza mwendo. sasa hapo yule mwenye tochi aliyejificha anakumulika na kuwatumia taarifa za gari yako na speed trafik aliyeko mbele.

We ukifika unashangaa umesimamishwa na kusomewa madhambi yako.. Hapo sasa lazima thelasini ikutoke.

So cha muhimu unapopita kwenye kibao cha hamsini uwe hamsini kweli hata kama huoni kofia nyeupe, we zingatia tu sheria bila shuruti.. Ni hayo tu....
Ndio safi kabisa.. Piga faini hata milioni..
Tena kwa kuongeza hapo , hata ukimuona trafik ukapunguza alaf kumpita ukaongeza zaid ya 50kph kabla ya kutoka kwenye 50kph zone , basi trafik anaweza akakupiga picha kwa nyuma na ukahukumiwa... Zile torch zipo advanced sana .
 
Back
Top Bottom