Janga La Elimu Tanzania: Tulikosea Wapi?


Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Messages
4,820
Likes
1,151
Points
280
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2007
4,820 1,151 280
Licha ya kusifikia kama kisiwa cha amani na utulivu, Tanzania ni Taifa la Majanga ya Kila Aina. Kwa miaka zaidi ya hamsini sasa, bado tunapambana na maadui wale wale wa maendeleo – Umaskini, Ujinga na Maradhi huku pakiwa na dalili zote kwamba tumeishiwa silaha na na mbinu za kivita kukabiliana na maadui hawa watatu. Mada yangu ya leo itajikita zaidi katika janga la elimu ambalo ndio chimbuko wa adui ‘ujinga’. Janga la elimu ni suala linalotawala mijadala mingi kwa muda mrefu nchini, lakini kwa muda mrefu, viongozi walikuwa wanaendesha shughuli zao kama vile mfumo wa elimu ulikuwa hauna tatizo lolote.

Mjadala wetu utakuwa na tija zaidi iwapo utajikita katika kutafuta majibu kwa maswali makuu muhimu yafuatayo:


 1. Je, mfumo wetu wa elimu umekumbwa na tatizo gani?
 2. Je, ni wapi tulikosea huko nyuma (chini ya Ujamaa)?
 3. Je, mfumo wetu wa elimu unalipeleka wapi taifa letu (chini ya uliberali)?
 4. Nini kifanyike kuokoa taifa letu na janga hili?

Majibu kwa maswali haya yanahitaji utafiti wa kina, ila ni bahati mbaya sana, binafsi sijawahi kusoma utafiti wa aina hii popote, hasa utafiti uliotokana na juhudi zetu wenyewe kama taifa; Lakini kukosekana kwa utafiti wa namna hii haiwezi kutuzuia watanzania wenye mapenzi na pia nia njema na taifa letu kujadili suala hili, hasa ikiwa lengo ni kubadilishana mawazo juu ya ufumbuzi. Katika bandiko langu la kwanza, nitajadili Swali la Kwanza na la Pili (rejea hapo juu). Swali la tatu na la nne nitayajadili katika bandiko lingine ili kuepuka kuweka bandiko moja refu.

Historia ya nchi yetu inatuonyesha kwamba mara tu baada ya uhuru wa Tanganyika (1961), motivation na drive for education ilikuwa ni ya juu sana; Kwa mfano, ndani ya kipindi cha miaka kumi ya mwanzo ya uhuru, sekta ya elimu nchini ilikuwa kwa kasi kubwa – idadi ya shule iliongezeka, chuo kikuu cha DSM kilipanuliwa zaidi kutoka kuwa chuo chenye idara moja na kuwa chuo chenye idara nyingi zaidi, taasisi mbalimbali za elimu ya juu, ufundi, utafiti n.k, pia zilianzishwa. Lakini haikuchukua muda mrefu kabla ya sekta yetu ya elimu kuanza kukumbwa na msukosuko kama nitakavyojadili hapo chini:

Kwanza, Serikali ilifanya kosa kubwa la kuwa na utamaduni wa kutenga fedha kidogo sana kwenye bajeti kwa ajili ya Sekta ya elimu, hasa katika mazingira ambayo kasi ya ongezeko la watu nchini (population growth) ikiwa ni kubwa mno (i.e. tangia uhuru, wastani wa kasi ya ongezeko la watu imekuwa takribani 3%); Kwa mfano, bajeti kwa ajili ya Sekta ya Elimu haikuwa inazidi 10% - 12% kila mwaka; Katika kipindi hicho hicho, takwimu zinaonyesha kwamba serikali na taasisi zake mbalimbali zilikuwa zikitengewa mafungu makubwa sana tofauti na sekta ya elimu.

Pili, Administration ya Sekta ya elimu ikawa very centralized, na mbaya zaidi local authorities zikafutwa suala ambalo lilipelekea shule nyingi zilizokuwa zikiendeshwa na town councils kupotea; Ni katika kipindi hiki pia shule nyingi ambazo zilikuwa chini ya NGOs zikataifishwa na serikali; Masuala haya yakapelekea faida na hasara kadhaa. Tukianza na faida, kubwa kuliko zote ilikuwa ni integration of religious and racially segregated schools; Tukija upande wa hasara, kubwa kuliko zote ni kwamba centralization ya mfumo wa elimu ulipelekea de-professionalization of the teaching profession in Tanzania. A quick cost – benefit analysis katika suala hili utaonyesha kwamba madhara yalikuwa ni makubwa kuliko faida; Pigo takatifu kwa mfumo wetu wa elimu ilikuwa pale working & material conditions za walimu zilipoanzwa kuwa neglected na serikali; Ni katika kipindi hicho taifa likashuhudia jinsi gani ‘teaching profession’ ikaanza kuwa downgraded & degraded – both socially and materially huku professions nyingine zikianza kuwa upgraded zaidi. Kwa mfano, ilifikia hatua kwamba – kama mtu unataka kuwa wa maana katika jamii, basi ilikuwa hauna budi uwe mwana siasa wa CCM; Lakini pia iwapo mtu ulikuwa unataka kuboresha maisha yako kiuchumi, basi ilikuwa hauna budi uwe katika shirika la umma; Na huu ndio ukawa mwanza wa exodus ya professional teachers kuhamia kwenye siasa na mashirika ya umma; Kwa mfano, kuanzia miaka ya sabini, nafasi za utendaji serikalini, mashirika mengi ya umma (pamoja na viwanda vingi) yalianza kujaa maafisa wengi sana wenye background ya ualimu. Sababu za msingi juu ya hili haikuwa nyingine zaidi ya wahusika kutafuta maisha bora zaidi i.e. profession nje ya ualimu offered better material incentives;

Je, matokeo yake yakawa nini?


 • Kwanza, ubora/Viwango vya ufundishaji ukaanza kuporomoka (deterioration of quality of instructions);
 • Pili, ethics (maadili) katika sekta ya elimu yakaanza kuporomoka;
 • Tatu, fani ya ualimu ikaanza kugeuka kuwa biashara ambapo sasa walimu wengi wakaanzisha ‘Tuitions’ pembeni;

Pamoja na yote haya, response ya serikali haikuwa katika kuboresha sekta ya elimu, hasa kwa kuongeza allocation ya budget kwa ajili ya sekta ya elimu; In summary – the government got its priorities wrong, na the society got its social values wrong; Na haya mawili ya mahusiano makubwa sana kama ambavyo tutakuja jadiili baadae;

Kuna hoja zinajengwa kwamba ni muhimu janga la elimu pia likajadiliwa katika muktadha wa uchumi, hasa kwa kuzingatia mgogoro wa kiuchumi nchini katika kipindi cha miaka ya sabini na themanini; Pamoja na ukweli kwamba mgogoro huu ulichangia katika janga la elimu nchini, kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu kulaumu kila mapungufu yanayojitokeza nchini kwamba ni kwa sababu ya ujamaa (azimio la Arusha), huku wahusika wakijenga hoja kwamba mwarubaini wa matatizo/majanga yote katika taifa letu ni mfumo wa uliberali na soko huria; Swali langu kwa watu hawa ni:


 • Je, Wakati wa ujamaa, kulikuwa na chochote ndani ya azimio la Arusha kilichozuia serikali kuipa sekta ya elimu kipaumbele katika bajeti?
 • Je, Azimio la Arusha lilitukataza kuwathamini walimu na badala yake kuhimiza kuwathamini viongozi wa chama na serikali, morally & materially?

Nitarejea kujadili swali la tatu na nne nililyoainisha hapo juu i.e:


 1. Je, mfumo wetu wa elimu unalipeleka wapi taifa letu (chini ya uliberali)?
 2. Nini kifanyike kuokoa taifa letu na janga hili?
 
K

kinauche

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Messages
7,684
Likes
850
Points
280
Age
68
K

kinauche

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2012
7,684 850 280
Kwanza kabisa pawepo na sera ya elimu ambayo inaeleweka na ambayo itasimamiwa.na watu weledi na wala siyo washabiki wa siasa. Mtu anayeweza kuielewa sera na kuitafsiri. Ebu tuelezane. Hivi sasa hivi mfumo wa elimu unamwandaa Mtanzania wa namna gani? Is anybody interested to know? Kids are just going to school and come out unlearned. What is the aftermath?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 

Forum statistics

Threads 1,275,109
Members 490,908
Posts 30,532,856