Jamvi la Habari ni gazeti la ACT-Wazalendo?

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
Habari Wakuu,

Inakuaje wenye vyombo vya habari kama magazeti wanashindwa kuwa wazi? Mfano, Unakuta gazeti linamilikiwa na Mwanasiasa, lakini wanaficha kuweka wazi, au unakuta gazeti linamilikiwa na Chama cha siasa lakini kinaficha watu wasijue. Nini madhara ya kuweka wazi?

Mfano Unakuta hili gazeti la Jamvi la Habari, Matangazo yake yote unakuta Wanatangaza matangazo ya Viongozi wao, je wanalipa VAT?

Mfano gazeti la Jamvi la Habari huweka tangazo la TETERE INTERNATIONAL MEDIA, Ambapo mmiliki wake ni Habib Mchange ambaye ni kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo.

Kitu kingine gazeti hili limenishangaza kitu kimoja kwa zaidi ya mwezi sasa limekomaa front page na habari ya Mbowe kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti zake za nje.

Halafu gazeti hili halioni mabaya ya CCM lenyewe kila likiamka ni Mbowe na CHADEMA.

Haliangalii CCM,

Lakini nachukua fursa hii kuwapongeza ACT kuanzisha gazeti lao, lakini nashangaa haliandiki habari za ujamaa wa kidemokrasia.
 
Huo ndio uandish wa habari Tanzania unaanzisha gazeti kwaajili ya kumpiga madongo mtu fulani.
 
Ki-Gazeti Mipasho, Ki-meanzishwa Kumchafua Mh. Mbowe; Huku Kikifumbia Macho Walioficha Pesa Nje ya Nchi Kama

Alivyosema Mh. Zitto. Hiki Ki-Gazeti Nadhani Mmiliki Mkuu Ni Yule Kijana Wa Kibaha Aliyekuwa Anamtuka Sana Mh. Lowassa

Bila Sababu za Kimsingi. Yule Kijana Wa ACT-Wazalendo.
 
Mwanahalisi, Mawio na Tanzania Daima wameacha kuandika habari za ufisadi dhidi ya Fisadi Mkuu Lowassa.

Acha magazeti ya CCM na ACT-CCM waandike.
 
Mimi mwenyewe hiki kitendo cha kumkomalia Mh. Mbowe kimenishangaza sana, ni ukosefu wa weledi wa kijarida sasa issue ya Mh Mbowe itakapoisha kitaandika nini?
 
Hilo ni jamvi la Mbowe la wala si habari!! Eti ayumbisha dola kuna mswahili mmoja kaizamisha kabisa dola ila hawamuoni!!! Watakua walimtong*za Mbowe akakataa c bure
 
Hilo ni jamvi la Mbowe la wala si habari!! Eti ayumbisha dola, si heri yye imeyumba kuna mswahili mmoja kaizamisha kabisa dola ila hawamuoni!!! Watakua walimtong*za Mbowe akakataa c bure
 
Tatizo nini!!? Ukweli wa habari au mmiliki wa media? Kama habari siyo sahihi why muhusika hasichukue hatua?
 
Nchi iko kwenye market economy.

Ni haki yao kuanzisha mradi/biashara ndani ya sheria ambayo itawanufaisha kulingana na matarajio yao.

Wewe kama msomaji una haki yako ya kuchagua kipi cha kusoma lakini huna haki ya kuwachagulia wenye gazeti habari ya kuandika.
 
kwani tatizo lako ni nini? ni habari husika au mwenye gazeti? ungekuja na taarifa kuwa hizo habari sio za kweli tungekuelewa. lakini umekuja na majungu tu humu. kwani kuna anayekulazimisha kusoma hilo gazeti? wewe nenda kasome tanzania daima tuachie hilo jamvi la habari tutasoma sisi.

Habari Wakuu,

Inakuaje Wenye vyombo vya habari kama magazeti wanashindwa Kuwa Waziri? Mfano, Unakuta gazeti linamilikiwa na Mwansiasa, lakini wanaficha kuweka wazi, au unakuta gazeti linamilikiwa na Chama cha siasa lakini kinaficha watu wasijue. Nini madhara ya kuweka wazi?

Mfano Unakuta hili gazeti la Jamvi la Habari, Matangazo yake yote unakuta Wanatangaza matangazo ya Viongozi wao, je wanalipa VAT?

Mfano gazeti la Jamvi la Habari huweka tangazo la TETERE INTERNATIONAL MEDIA, Ambapo mmiliki wake ni Habib Mchange ambaye ni kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo.

Kitu kingine gazeti hili limenishangaza kitu kimoja kwa zaidi ya mwezi sasa limekomaa front page na habari ya Mbowe kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti zake za nje.

Halafu gazeti hili halioni mabaya ya CCM lenyewe kila likiamka ni Mbowe na CHADEMA.

Haliangalii CCM,

Lakini nachukua fursa hii kuwapongeza ACT kuanzisha gazeti lao, lakini nashangaa haliandiki habari za ujamaa wa kidemokrasia.
 
Kama magzeti ya Uhuru, Tanzania Daima, Mtanzania, etc yanaendelea kuuza unadhani kwa nini hili life.

Kapa post ya Act-wazalendo humu JF wanapata reply 10 kwa nini lisifee, biashara ni watu kaka
 
Last edited by a moderator:
Hii habari ya Mbowe, kumbe kuna watu inawachoma kiasi hikI? Hoja ni je, habari inayoandikwa ni kweli au siyo kweli? Kama siyo ya kweli basi nashauri mtakatifu Mbowe akalishitaki haraka sana hili gazeti maana 'linamchafua'..
 
Back
Top Bottom