Maxence Melo
JF Founder
- Feb 10, 2006
- 4,230
- 13,415
Wakuu,
Tumerejea hewani baada ya siku 21 tukiwa hatutoi huduma hii.
Kilichotokea:
Mnamo Jumapili, tarehe 10 Juni 2018 tulipata kuiona notisi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) ikitutaka kusitisha huduma mara moja nasi tulitii na kusitisha siku hiyo.
Tuliwasiliana na Mamlaka na ilitusikiliza na tukafuata taratibu za kujisajili ambapo wikiendi hii imetupa leseni ya miaka 3 na kuturuhusu kuendelea na huduma kwa wateja wetu.
Pamoja na mengine, tuliwasilisha maoni yetu kwa maandishi kwa mamlaka(TCRA) juu ya vipengele vya kanuni tunavyoona hazitekelezeki na kutoa mapendekezo ya maboresho. Tulisisitiza mambo manne kwa haraka:
1) Kanuni ya 5 kipengele (e) kinavunja haki ya faragha ya watanzania iliyowekwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi na utekelezaji wake utakuwa changamoto kwa wengi.
2) Kanuni ya 10 kipengele (b) inayolifanya kosa la jinai kutoweka nywila(password) kwenye kifaa cha kidijitali, tulishauri iangaliwe upya.
3) Kanuni ya 6 kipengele (3) inayotoa muda wa saa 12 kuondolewa kwa maudhui yanayolalamikiwa tulishauri iangaliwe upya kwani kwa uzoefu wetu inazuia haki ya kusikilizwa na kupelekea kuzimwa sauti za wananchi.
4) Gharama za usajili zilizowekwa zinazuia baadhi ya wanaotoa huduma kuendelea kufanya hivyo kwani si wote wenye uwezo huo na si kila blog inafanya kazi kibiashara. Tulipendekeza ikibidi yawekwe madaraja ili hata wale wadogo wasiachwe nyuma.
Mwisho:
Tunasikitika kwa kilichotokea hivyo tunaomba radhi kwa watumiaji kwa usumbufu wowote uliotokana na kusitishwa kwa huduma hii. Pia tunawashukuru kwa uvumilivu wenu na kuendelea kuwa nasi katika kipindi chote huduma ikiwa haipatikani.
Wateja wetu walio nje ya mipaka ya Tanzania walioathirika na yaliyotokea, tunawaomba radhi sana.
KUHUSU USALAMA WA DATA:
Kwa wale ambao wanahitaji kuongeza kuimarisha faragha zao, kwenye profiles zenu mnaweza kuweka email mpya ya kuwa inatumika hapa JamiiForums na kwingineko mitandaoni. Tengeneza email mpya kupitia Hushmail - Enhanced email security to keep your data safe au Secure email: ProtonMail is free encrypted email ili uwe unaitumia kwa mawasiliano yaliyo salama zaidi. Ukiamua kutumia jina halisi (verified), wasiliana nasi ili tulithibitishe na uwekewe VERIFIED badge.
Tunatambua kuwa Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania imetoa ulinzi wa Uhuru wa Kujieleza na Uhuru wa kutoingiliwa mawasiliano kwa mujibu wa Ibara ya 18:
Kwa kiswahili:
Mambo ya kuzingatia:
Wateja wetu tunawashauri kusoma sera yetu juu ya faragha na pia mwongozo wa ushiriki katika utoaji maoni katika JamiiForums.
Asante