JamiiForums thanks

Ok Dar unaishi VIP wakati hauna kazi . Wewe ni Kabila gani samahan kwa kukuuliza ila ningependa kujua Kabila lako

dar yupo bro so alinichukulia chumba single akanilipia miezi 4 maswala ya msosi namaliza kwake huku nikisoma ramani...kuhusu kabila mimi ni mwenyeji wa kanda ya ziwa
 
dar yupo bro so alinichukulia chumba single akanilipia miezi 4 maswala ya msosi namaliza kwake huku nikisoma ramani...kuhusu kabila mimi ni mwenyeji wa kanda ya ziwa
Huyo kaka yako ingekuwa bora angekupa mtaji ila usijali mungu ni mwema utafanikiwa kanda ya ziwa musoma au . Endapo nikisikia kaz mahali nitakujulisha
 
Huyo kaka yako ingekuwa bora angekupa mtaji ila usijali mungu ni mwema utafanikiwa kanda ya ziwa musoma au . Endapo nikisikia kaz mahali nitakujulisha

bro hawezi nipa mtaji maana na yeye anaunga unga bado ....musoma ndio kabila la baba wa taifa ukisikia nishtue ndugu yangu tabu haina aibu
 
bro hawezi nipa mtaji maana na yeye anaunga unga bado ....musoma ndio kabila la baba wa taifa ukisikia nishtue ndugu yangu tabu haina aibu
Nilijua utakuwa wa musoma manake baadhi ya wanaume wa musoma wanatabia ya kuhama nyumba zao . Wakipata tatizo wenyewe wanakimbia badala ya kutatua tatizo . Nitakustua mkuu
 
Nilijua utakuwa wa musoma manake baadhi ya wanaume wa musoma wanatabia ya kuhama nyumba zao . Wakipata tatizo wenyewe wanakimbia badala ya kutatua tatizo . Nitakustua mkuu

haya bwana
 
Pole sana kiongozi, Mungu ni mwema utafanikiwa tu usikate tamaa
 
Nimehis tu huyo atakua mtu w kanda ileee!! Pole we mwanaume huna haja ya kua na wsws na maamuz yako. Walk the talk
 
Mkuuu ushauri mzuni ni wewe kutafta maisha.ukirudi ataendelea kukudharau zaidi.kumbuka hapo hujaitekeleza ila unatafta maisha kwa ajili ya familia yako
 
I lov this comment
 
Pole bro na kila la kheri..pia mshirikishe Mungu kwenye mihangaiko yako ya siku na ukienda kulala shukuru kwa lolote.
 
Majibu rahisi.kwenye maswali magumu.
Unadhani hajui sitution aliyonayo mme wake?

Wameishi miaka 12 kwa furaha hilo hulioni??

Man usirudi kwani tatizo liko pale pale kama huna mshiko huyo wife ataendelea kukupanda kichwani tu, so long watoto wako mikononi mwa mama na anauwezo wa kuwatunza tafuta kwanza.
 
thanks men nimeipenda hii maana ndio haswa lilikua wazo langu
 
thanks men nimeipenda hii maana ndio haswa lilikua wazo langu
Kumbe Una mastress yakoee ndo mana Kule PM ulikuwa unaongea utumbo mwanzo mwisho, subir nimtafute huyo bidada nkampeleke kwa dokta akapate sindano yetu ilee
 
Kumbe Una mastress yakoee ndo mana Kule PM ulikuwa unaongea utumbo mwanzo mwisho, subir nimtafute huyo bidada nkampeleke kwa dokta akapate sindano yetu ilee

ha ha nsamehe kama nilikukwaza huyo bidada wewe mpeleke tu akadungwe sindano ,,,sindano zipo kwaajili
 
hii story badoo sijaridhika sasa hapa town unafanya nn mkuu upo kwa nani?

umepata kazi kama umepata kwanni bado unaikimbia familia mke alikosea na wewe umekosea watoto wataumia

na unaishukuru nini forum hii?
 
mzee naishukuru forum kwa ushauri uliotukuka sio mara ya kwanza kuomba hapa ushauri na nafarjka kabisa...kuhusu nakaa wapi nmeshaelezea hapo nyuma nimepangishwa chumba na bro ambae yeye anakaa huku mda sasa...sijapata kaz bado maana tangu nije huku sasa n siku 40 zimepita......
 
Hahhaaa poapoa man!

Pale mwanamke unapojua kazi yake kwa mda mrefu, halafu siku anakwambia hivi wewe una akili? We unakula tu unajua hizi lesa nazipata wapi na nazipataje??

Inauma sana lkn no way!
 
Pole sana, ndo maisha yalivyo. Maamuzi uliyoyafanya sio mabaya sana, sometimes it happens even to others kwa sababu BINADAMU WANAKERA SANA. Hivyo kutafuta suluhu ya muda kuondoka home sio mbaya kwa sababu 1. uliepusha vita 2. Ulitafuta furaha ya muda 3. Uliotoa muda kwa wife ili aweze kuona umuhimu wako. 4. Umepata jambo la kutuambia ili nasi tujifunze toka kwenye haya matukio ya mahusiano.
Pamoja na yote hayo fahamu kuwa wewe ndio kichwa cha familia. Na ili uwe kichwa kizuri lazima ujue kuwa unapaswa kutimiza majukumu yako yakibaba kwa mkeo na wanao. So, unatakiwa uwe na shughuri ambayo itakuingizia kipato ya kukidhi mahitaji ya familia yako. Kwa maaana hiyo ni lazima ujitume ili gurudumu lisonge. Katika maisha kuna shughuri za aina nyingi kama vile Biashara, Ajira na Uwekezaji. Nilazima ufanye ma moja kati ya hizo au zote ili goma lisonge.
Kufukuzwa, kuondolewa, kusimamishwa kazi si mwisho wa maisha, yakikukuta hayo unachotakiwa kufany ni kubadilisha Mtazamo wako na kutafuta shughuri ambayo inaendena na wakati unaokabiliana nao. Si vyema kujifungia nyumbani. Toka, changanyika, jifunze usichokijua kwenye shughuri zilizopo mtani ili maisha yako yasonge.
Ukiondoa aibu, kila kitu kitakaa sawa kwani kuna shughuri kibao mtaani (Zimeambatanishw) ambazo ukizifanya zitakuingizia kipato cha kuendesha maisha ya familia yako. Usipofanya hivyo utakuwa unataka kubadili majukumu ya familia ambapo utamtaka mama achukue majukumu ya baba, hapo ndipo matatizo yanapoanziaga. Akianza yeye kutafuta kwa ajili ya kuziba pengo lako, inamaanisha kuwa wewe si muhimu tena kwao. Kinachofuata ndio kile kilichokukuta.

Badilika, acha kujifungia ndani, tafuta shuguri ya kufanya ili utimize majukumu yako kama baba.
 
Attachments

Mkuu miongoni mwa watu wenye akili na wewe umo, atakaesema umefanya makosa kuondoka na yeye ni akili zake.

Mwanaume unatakiwa kuwa mvumilivu lakini pia kuna uvumilivu wa kijinga.

Kwa maelezo yako hukuondoka nyumbani kwa kukwepa majukumu la ila kwa kuinusulu ndoa na familia yako pia kupuka manyanyaso ya akili na roho.

Kwa nionavyo mimi ulifanya jambo la busara kwani usingeondoka ambalo lilikuwa linajili ni kutengana na kugawana mali yenu hali ambayo ingewaweka watoto katika mazingira magumu sana.

Ushauri wangu ni kwamba endelea kuwasiliana na mkeo wasalimie watoto kila siku hata ikibidi wadanganye unafanya kazi na ukipata chochote wakumbuke uwatumie zawadi na mahitajio mengine.

Ila wakati huo ukiwa unatafuta kazi popote pale, mungu hamtupi mja wake utapata iwe arusha au hata huko Dar, baada ya kupata kazi rudi nyumbani.
 
komaa upate kazi la si hivyo mambo yatazidi kuwa mabaya yaani mie ni ke lakini huwa hata zege naweza kubeba naogopa sana ujobless kwakiwa sijaumbwa kutegemea mtu yeyote naogopa kuomba kwa mwanaume........naogopa manyanyaso uwii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…