Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,251
- 44,586
Mtandao wa Kijamii wa Jamii Forums, umekanusha madai yaliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Pius Msekwa, kuwa umeanzishwa na vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kwamba unatumiwa na chama hicho katika harakati zake za kisiasa hapa nchini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jamii Forums, unafanya kazi kwa kujitegemea na kwamba haumilikiwi na chama chochote cha kisiasa wala kufadhiliwa na Chadema kama alivyodai Msekwa.
Taarifa hiyo ilisema Msekwa alitoa madai hayo wiki iliyopita wakati akitambulisha Sekretarieti mpya ya CCM mjini Dodoma ambapo alitumia muda wake kushutumu mtandao huo.
Mtandao huo ulisema kwa sasa una wanachama 40,000 waliojiandikisha na kwamba unafanya kazi kama chanzo huru cha habari bila kutumiwa na mtu wala chama chochote cha siasa.
Shutuma hizo za Msekwa zilitolewa Aprili 14, mwaka huu mjini Dodoma ambapo pia mwanasiasa huyo alisema mtandao huo ulichangia kukikosesha kura CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Taarifa hiyo iliongeza kwamba shutuma zinazotolewa dhidi yao kwamba unatumika kuivuruga CCM na serikali yake sio za kweli na kwamba zinalenga kuukwamisha mtandao huo katika harakati zake za kuielimisha jamii na kuipasha habari.
Mtandao huo ulisema CCM inauandama kutokana na wao kuwa mstari wa mbele katika kupiga vita vitendo vya rushwa ambavyo hivi karibuni vimekichafua chama hicho na serikali yake.
Shutuma hizo zimewasababishia usumbufu kutoka kwa wanachama wao walioenea kona zote za nchi na nje ya nchi na kwamba hatua hiyo ya CCM ni ishara kuwa kimeanza kuuogopa mtandao huo.
This is good...but I also think at the end the forumist owner should have encourage sekretarieti mpya kujiunga na JF and engage in useful discussion just like other politicians do e.g Kabwe Z, and Slaa W.
chama cha magamba(ccm) msifungie jamii forum njoo mninyang'anye laptop na morden!!tehe! tehe!
Nsiande, kina Kabwe na Slaa hawakukaribishwa; kwanini tuwape huo umuhimu hao watu wa sekretariati ya CCM? kwa ujiko gani walionao. Wanajua anuani ya JF - https://www.jamiiforums.com kuna mahali pale juu panasema "register"...
Nsiande, kina Kabwe na Slaa hawakukaribishwa; kwanini tuwape huo umuhimu hao watu wa sekretariati ya CCM? kwa ujiko gani walionao. Wanajua anuani ya JF - https://www.jamiiforums.com kuna mahali pale juu panasema "register"...
Nsiande, kina Kabwe na Slaa hawakukaribishwa; kwanini tuwape huo umuhimu hao watu wa sekretariati ya CCM? kwa ujiko gani walionao. Wanajua anuani ya JF - https://www.jamiiforums.com kuna mahali pale juu panasema "register"...
Mtu mwenye hoja hahitaji mwaliko na yule asiye na hoja ukimbia midahalo na haoni umuhimu wake,CCM kutokana na ufinyu wa mawazo na mazoea ya kua CCM tofauti na juu ya vitu vyote.Tatizo hili limevifanya vichwa vyao kua vivivu kufikiri na kukimbilia njia za mkato "KUTAFUTA WACHAWI WAO"wakati wa uchaguzi ambapo ni wakati mzuri wa kunadi sela kwenye midahalo wao waliingia mitini.CCM WAKATI WA KUONGOZA KWA MAZOEA UMEPITWA NA WAKATI!Mungu ibariki TanzaniaNsiande, kina Kabwe na Slaa hawakukaribishwa; kwanini tuwape huo umuhimu hao watu wa sekretariati ya CCM? kwa ujiko gani walionao. Wanajua anuani ya JF - https://www.jamiiforums.com kuna mahali pale juu panasema "register"...