Jamii ipi iko sahihi?. . .

Jamani sikutaka mjadala huu uwe wa kulinganisha kati ya mwanamke na mwanaume ni nani anaathirika na ndoa na nani anafurahia hiyo ndoa,lengo langu lilikua ni kuangalia kati ya zamani na sasa ni wakati upi umetimiza kwa usahihi dhana ya ndoa,yaani kuishi pamoja til deth!Nadhani kile cha mgawanyo wa madaraka ndani ya ndoa ni mjadala mwingine.Pia inaonekana kama vile mada hii iko kimfumo dume zaidi(na tafsiri hii haikua lengo langu) ndo maana wanawake ma-independenti wamechangia kwa kuupenda mfumo wa ndoa wa sasa zaidi,wamefanya hivyo kwa sababu mfumo wa zamani unaonekana kama ulimbana mwanamke na kumnyima "uhuru" sijui kama ni kweli ama la!Hili linategemea na tafsiri yako ya uhuru!
 
Back
Top Bottom