Wang Shu
JF-Expert Member
- Feb 1, 2014
- 2,563
- 3,708
Katika mafanikio kila mtu hutamani hayafikie basi ni kumiliki nyumba ni moja ya ndoto ya kila mmoja na rika tofauti, kila mtu anataka kuwa na kwake na familia yake.
Kwa Hali ya maisha ya sasa ni ngumu kiasi kujenga angali kijana,wapo wanaofanikiwa kujenga nyumba ya kuishi kipato cha kawaida hawa watu naweza sema ni "Silence Motivation Speaker".
Jamii inayomzunguka hasa vijana wa rika lake na wale wa karibu yake wanapata msukumo wa ujasiri wa kuthubutu wakiamini kumbe inawezekana!
Miaka 2 iliyopita nilipatwa na roho ya wivu wa maendeleo na kujitafakari Sana ni pale rafiki yangu niliyesoma nae aliponambia anapaua nyumba yake ya chumba 2 nilimuuliza swali moja tu "Umewezaje?"
Ni rafiki yangu ambaye nilimtangulia darasa 1 tulikuwa kama ndugu tulipanga chumba kimoja shule za kutwa changamoto nyingi tulitatua pamoja hatimae nilimaliza nikamuacha anaendelea na masomo.
Baada ya miaka kadhaa ananipa taarifa anajenga yeye alafu mimi bado nimepanga sikukubali kirahisi namna hiyo niliona kumbe naweza kujenga zaidi yake,hatimae sasa mwaka huu 2020 unaisha na mimi nampatia taarifa kuwa boma langu lipo kwenye linta.
Asante Sana rafiki yangu hujanipatia pesa lakini matendo yako na maneno yako ni vitu muhimu kwangu.