Uchaguzi umekwisha kwa namna yake ya ajabu ambayo kila mmoja ameondoka na moja kichwani. Kwa aina ya Rais tulie naye ambaye ni king'ang'anizi na hana mjadala kwenye aliloamua, tunajua fika baada ya mbilinge za uchaguzi kuna baadhi ya vikwazo vitakuja na hata kubali kuwa mnyonge.
Uhakika wa vikwazo kuja upo wazi wazi lakini tumejipanga vipi kuvikabili. Kama ilivyokuwa kwa corona Je, tutaibuka kidedea. Kama tukiwekewa vikwazo na tukashinda basi tutakuwa taifa huru linalojitegemea kiuchumi kama tutaanguka basi tutakuwa tumerudi nyuma sana kama taifa.
Kama tumedhamiria kusimama na kujitegemea ni wakati sasa wa kuachana na uchumi wa kuchuuza vitu. Ukitembea kwenye masoko, stendi za mabasi na pembezoni mwa barabara utakutana na meza lukuki zimejaa vitu kutoka China vingi vikiwa na ubora hafifu.
Sekta za kilimo na viwanda zinakufa, vijana wengi wamegeuka wachuuzi. Vijana wengine wasomi wenye taaluma mbalimbali wamekuwa wachuuzi wa online. Je, tutaweza kuhimili vikwazo? Tuna taifa ambalo vijana hawajui wimbo wa taifa lakini wanajua nyimbo za Diamond.
Tuna taifa la wambea na lisilo la wachapakazi, juzi mchezaji wetu Samatta amesitishiwa mkataba na club ya Aston Villa.
Umati wa watu waliojaa kutoka Tanzania wakilaani ilionyesha ni kiwango gani watanzania wako kwenye mitandao muda mwingi kuliko kufanya kazi, ukilinganisha hata na taifa la Uingereza watu wake wakiwa kwenye lockdown ya Covid19.
Ili kuweza kuhimili vikwazo vinavyokuja lazima tuwe tayari kufanya kazi lazima tuwe na viongozi wanaowaza na kupanga mipango kwa umakini. Kama tukijipanga karata hii ya vikwazo tukaitumia vizuri inaweza kuwa mwanzo wa kusimama kama taifa.