Jamhuri ya sukari - kuna jambo

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
22,116
49,360
Nimeshangazwa sana na Mh. Rais na waliomwandalia hotuba yake, ukiacha upupu mwingine mwingi, jinsi walivyoikweza sukari hata kuifanya kama topic inayojitegemea kwenye hotuba yake. Hivi sukari na masuala kama ya elimu (rejea matokeo machafu ya form four mwaka uliopita, kupanda kwa kasi kwa ada za shule na vyuo mbalimbali, n.k), kuporomoka kwa kasi kwa uzalishaji katika maeneo mbalimbali, suala tete la ajira na mishahara duni, hali duni za wananchi (maisha kwenye nyumba za tembe, n.k. na mikakati ya kukabiliana nayo), migogoro inayoendelea huko uarabuni na kwingineko na hatma ya watanzania wenzetu waishio huko (wajibu na nafasi ya serikali ni nini?), kufilisika kabisa kwa mashirika muhimu kwa uchumi na hadhi ya taifa (reli, ATC, n.k.), suala muhimu kwa amani na utulivu wa nchi yetu - ARDHI (mashamba ya Mbarali, Mbulu, Bagamoyo, hata Zanzibar, n.k.); n.k. n.k.

Haya ndio masuala ambayo nilitegemea kama kiongozi mkuu wa Jamhuri na Amiri Jeshi Mkuu yanaangukia chini ya mamlaka yake tena ayazungumzie katika ngazi ya kitaifa (top-level). Badala yake anatuletea habari za tamtam - SUKARI ama kweli Tz yafaa pia kuitwa Jamhuri ya Sukari. Wenzetu leo wanaongelea si tu kwenda bali kuishi anga za mbali rais unazungumzia bei ya sukari gulioni. Na Meneja Masoko ya Kariakoo au Tandale azungumzie nini?

Lakini sukari nchi hii ina siri gani? Nakumbuka ilishawahi kumtimua waziri fulani na naibu wake tena wasomi wazuri tu; mmoja profesa na mwenzie dakta. Nadhni kuna kamchezo fulani kanawavutia hata wakuu kuingia kichwa kichwa; ni suala la muda tu.
 
..Umeliona hilo tu..na hii ya kwamba hotuba yote Mbowe alikuwa nayo jana mchana kabla haijatolewa, na akaijibu vipengele vile vya kuishambulia CHADEMA(rejea gazeti la Mwananchi 01-03-2011), na bado wasaidizi wamemwacha tu Rais aongee content hiyo hiyo iliyomo kwenye 'hotuba ambayo tayari imeshajibiwa'!....
 
nyie huyu prezidaa si mzima jamani mh mimi naona km tumemweka mpita njia tu ambaye hana uchungu na taifa letu.
 
Mtu wa kijiweni tusitarajie lolote maskini bado miaka mingapi atuachie nchi yetu!!
 
..Umeliona hilo tu..na hii ya kwamba hotuba yote Mbowe alikuwa nayo jana mchana kabla haijatolewa, na akaijibu vipengele vile vya kuishambulia CHADEMA(rejea gazeti la Mwananchi 01-03-2011), na bado wasaidizi wamemwacha tu Rais aongee content hiyo hiyo iliyomo kwenye 'hotuba ambayo tayari imeshajibiwa'!....

Hapo tunaweza kusema wasaidizi wake wameamua kumsaliti kwa makusudi..
Poor Kikwete.
 
Back
Top Bottom