isajorsergio
Platinum Member
- Apr 22, 2018
- 4,143
- 6,562
| Jamhuri ya Colombia, Republic of Colombia au República de Colombia ni taifa linalopatikana Amerika ya Kusini na kwa kiasi Kaskazini. Colombia ni taifa lenye ukubwa wa 1,138,910 Kilometer Sq sawa (439,736 Sq Miles).
Lugha rasmi ya taifa ni Kihispaniola, lakini takribani lugha 68 zinazungumzwa. Serikali kuu ni mfumo wa jamhuri, Pesa rasmi ni Colombian Peso (COP) COP 1 ni sawa na Centavos 100.
Bendera ya Jamhuri ya Colombia.
Colombia inakadiliwa kuwa na wastani wa watu million 52,018,088 kufikia Februari 25, 2020. Mji mkuu wa taifa hili ni Bogotá pia ndio mji ulioendelea zaidi kuufanya kuwa Jiji la Bogotá. Jiji hili linapatikana katika uwanda wa Cordillera Mashariki.
Miji mingine mikubwa na iliyoendelea ni Medellín, Santiago de Cali, Barranquilla, Cartagena, Cúcuta, Bucaramanga, Pereira hadi Santa Marta. Medellín, Antioquia ni Jiji lenye kuhodhi media, sanaa, ubunifu, burudani na sehemu mbalimbali za michezo na kustarehe.
Bogotá, Bogotá D.C ni sehemu rasmi ya Serikali na mamlaka kuu. Bogotá inahodhi Ikulu, Bunge la seneti, benki kuu, ofisi na afisi mbalimbali, mashirika na makao makuu mbalimbali ndani ya Colombia.
Bogotá, Bogotá D.C
| Shughuli za Kiuchumi, Biashara na Uzalishaji. Colombia inaendesha shughuli za kilimo hasa kahawa na ni taifa la tano duniani kwa uzalishaji wa kahawa asilia, kilimo cha ndizi, mpunga/mchele, mahindi, miwa, maharage, alizeti, mboga mboga pamoja na matunda.
Colombia inazalisha mafuta (Crude Oil) na mzalishaji mkuu wa mimea yenye usaidizi katika hospitali zote duniani (Madawa ya kulevya).
Colombia ni moja ya mataifa matatu katika bara la Amerika Kusini lenye uchumi thabiti, imara na maendeleo mithili ya moto. Colombia kufikia hapa ilipitia milima na mabonde hadi mwaka 1991 ilipobadili katiba kuu ya nchi iliyokuwa na mlengo wa ujamaa na kulifanya taifa kuwa la kibepari na uliberali.
Uwapo maeneo ya Medellín, Bogotá, Cartagena, Barranquilla au Santiago de Cali utashuhudia magari ya umma yenye kutumia umeme, mionzi jua na gesi asilia. Utashuhudia barabara zenye kiwango cha rami njia nane, nne, mbili na hata rami maeneo ya uchochoroni hadi milimani. Utastaajabu pale utapokutana na treni na askari wa usalama mitaani.
| Madawa ya kulevya. Kwa kipindi kirefu Colombia imekuwa chanzo au muhimili wa biashara hii duniani kote na hasa nchi za Amerika. Wamekuwepo waasisi kama Pablo Emilio Escobar Gaviria kiongozi wa NARCOS na muanzilishi wa Medellín Cartel iliyofanya uchakataji, uzalishaji na usambazaji wa madawa kuelekea US na mataifa mengine.
| Elimu. Colombia elimu yake ni Mwanzo, Awali, Secondary na Elimu ya Juu. Huku elimu ya juu ikiwa imelenga vitendo, ubunifu na teknolojia kwa asilimia 92.
Colombia ndani ya Departments (Mikoa) kuna vyuo vya Umma. Baadhi ya vyuo bora ni National University of Colombia, Universidad Nacional de Colombia, Universidad de Antioquia, Universidad El Bosque, Pontifical Xavierian University, Universidad de los Andes na University of Altantico.
| Kupitia Sanaa, Michezo na Burudani taifa la Colombia limejitangaza vyema duniani kote. Mpira wa miguu ni mchezo nambari moja ndani ya Colombia huku ikitambulishwa kimataifa na nyota kadha wa kadha kama, Carlos Valderrama, René Higuila, Faustino Hernán "Tino" Asprilla Hinestroza, Christian Zapata, James Rodríguez, David Ospina, Radamel Falcao, Juan Cuadrado, Jeison Murillo, Santiago Arias, Yerry Mina na Davinson Sánchez.
Shakira - Malkia wa muziki wa pop ya kilatini.
Katika upande wa burudani Colombia ndio nyumbani! Nyumbani kwa Shakira mwanamuziki mwenye levels juu zaidi ya kimataifa, mwanamama asiyechosha, mirindimo na miondoko ya ujana hakika Shakira ni Icon!. Wengine ni vijana machachali kama Maluma, J Balvin, Juanes, Farina, Manuel Turizo, Sebastian Yatra, Karol G na Kike Santander huku wakiwepo wenye ujazo kama Carlos Vives, Fonseca na Ilona.
Hii ndio Jamhuri ya Colombia 🇨🇴
Nakala: Jon Stephano
Nakala: yna2