Jamhuri ya Chechnya ni watu gani?

Jamhuri ya Chechnya ni watu gani?

Life2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,387
Reaction score
4,881
Binafsi nimeshindwa kuwaelewa hawa watu wanaounda Jamhuri ya Chenchya hawa watu ni kina nani ni species gani ile.

Ukiangalia vita vya Ukraine hawa jamaa wapo upande wa Mrusi wakidai wanapigania Dini yao na kuwaita wenzao Saitan/mashetani nashindwa kuelewa wanafaidika vipi na hii vita.

Wanajiita Chechen republic at the same time wameshawahi kupigana na mrusi Mara mbili Mara ya kwanza Mrusi alipigwa kipigo kikali tu na hawa jamaa na kumsababishia Urusi hasara kubwa, Mara ya pili walipigwa na kufikia kukaa meza ya mazungumzo na Mrusi ila leo naona wamechagua upande dhalimu wa Mrusi.

Wanarais wao sijui Kaydrov kama nimekosea mtanirekebisha hakuna kitu anaongea Mrusi hawa jamaa wakapinga its like Lukashenka na Belarus yake.

Swali la kujiuliza je hawa ndio Mercenaries ambao mrusi anawatumia nchi mbalimbali kwa malipo mfano Libya, Mali, Sudan kaskazini, Ukraine, Syria na kuwalipa Rubble?

Manake sidhani kama kuna shughuli yoyote ya uzalishaji wanayofanya inaonekana kama kupigana/Vita ndio ajira yao.

Mwenye maekezo zaid atujuze
 
Binafsi nimeshindwa kuwaelewa hawa watu wanaounda Jamhuri ya Chenchya hawa watu ni kina nani ni species gani ile.

Wale ni wazawa na wenyeji wa kanda ile ya Caucasia miaka na miaka, wengi wao ni waislamu na wana lugha yao ya kuitwa ‘chechen’ na huzungumza kirusi pia.

Ukiangalia vita vya Ukraine hawa jamaa wapo upande wa Mrusi wakidai wanapigania Dini yao na kuwaita wenzao Saitan/mashetani nashindwa kuelewa wanafaidika vipi na hii vita.

Kwa sasa Chechen wapo chini ya Urusi, ni kama Zanzibar ilivyo chini ya Tanzania bara au Tigray, Ogaden na Oromo chini ya Ethiopia, au Lagos chini ya Nigeria.

Wana askari wao wa kuitwa ‘Kadyrovites’ ambao katikati mwa miaka ya 2000s walirasimishwa na kuingizwa ndani ya mfumo wa jeshi la taifa la Urusi ndani ya Chechnya.
Na huko Ukraine ilielezwa kuwa walikuwa wakipigana dhidi ya waChechen wenzao, ambao wao waliiunga mkono Ukraine.

Wanajiita Chechen republic at the same time wameshawahi kupigana na mrusi Mara mbili Mara ya kwanza Mrusi alipigwa kipigo kikali tu na hawa jamaa na kumsababishia Urusi hasara kubwa, Mara ya pili walipigwa na kufikia kukaa meza ya mazungumzo na Mrusi ila leo naona wamechagua upande dhalimu wa Mrusi.

Sahihi, kimsingi ktk vita vya pili vya Chechen vilivyoanza 1999 Akhmad Kadyrov, aliyekuwa kiongozi wa Chechnya, alielewana na Urusi akahamia upande wa serikali ya Urusi kupigana na waChechen walokuwa wakitaka kujitenga. Hawa walotaka kujitenga baadhi yao wako Ukraine wanapigana dhidi ya Urusi.

Wana rais wao sijui Kaydrov kama nimekosea mtanirekebisha hakuna kitu anaongea Mrusi hawa jamaa wakapinga its like Lukashenka na Belarus yake.

Wala hujakosea.

Swali la kujiuliza je hawa ndio Mercenaries ambao mrusi anawatumia nchi mbalimbali kwa malipo mfano Libya, Mali, Sudan kaskazini, Ukraine, Syria na kuwalipa Rubble?

Hapana, Mamluki (mercenaries) wanaotumika ktk nchi ulizozitaja kutokea Urusi ni ‘Wagner Group’.
‘Kadyrovites’ si mamluki, ni sehemu ya jeshi la taifa la shirikisho la Urusi ndani ya jamhuri ya Chechen.

Manake sidhani kama kuna shughuli yoyote ya uzalishaji wanayofanya inaonekana kama kupigana/Vita ndio ajira yao.

Mwenye maekezo zaid atujuze

Askari hawa hufanya shughuli za ulinzi kama wafanyavyo askari wa majeshi mengine.
 
Wale ni wazawa na wenyeji wa kanda ile ya Caucasia miaka na miaka, wengi wao ni waislamu na wana lugha yao ya kuitwa ‘chechen’ na huzungumza kirusi pia.

Kwa sasa Chechen wapo chini ya Urusi, ni kama Zanzibar ilivyo chini ya Tanzania bara au Tigray, Ogaden na Oromo chini ya Ethiopia, au Lagos chini ya Nigeria.

Wana askari wao wa kuitwa ‘Kadyrovites’ ambao katikati mwa miaka ya 2000s walirasimishwa na kuingizwa ndani ya mfumo wa jeshi la taifa la Urusi ndani ya Chechnya.
Na huko Ukraine ilielezwa kuwa walikuwa wakipigana dhidi ya waChechen wenzao, ambao wao waliiunga mkono Ukraine.

Sahihi, kimsingi ktk vita vya pili vya Chechen vilivyoanza 1999 Akhmad Kadyrov, aliyekuwa kiongozi wa Chechnya, alielewana na Urusi akahamia upande wa serikali ya Urusi kupigana na waChechen walokuwa wakitaka kujitenga. Hawa walotaka kujitenga baadhi yao wako Ukraine wanapigana dhidi ya Urusi.

Wala hujakosea.

Hapana, Mamluki (mercenaries) wanaotumika ktk nchi ulizozitaja kutokea Urusi ni ‘Wagner Group’.
‘Kadyrovites’ si mamluki, ni sehemu ya jeshi la taifa la shirikisho la Urusi ndani ya jamhuri ya Chechen.

Askari hawa hufanya shughuli za ulinzi kama wafanyavyo askari wa majeshi mengine.
Nashukuru sana Kiongozi kwa Shule iliyoshiba.
Hakika nimechota madini be blessed

Na vip hawa Wagner nimeona mwanzilishi wao alikua ndani ya Jeshi la Urusi na pia wakati mwingine wanakutana na Putin je ni kikundi kabisa kinachotambulika rasmi na nchi manake pia Ukraine wapo.
 
Naam, hutambulika rasmi na hupewa kandarasi za kufanya kazi huku wakiungwa mkono na serikali.

Watu wao wengi huwatoa jeshini.

Marekani pia wanazo mathalani wale ‘Blackwater’ ambao sasa wanajiita ‘Academi’.
 
Shukrani sana mtaalamu madini ya kutosha
 
Jamhuri ya Chechen, au Chechnya, ni jamhuri ya Urusi, inayokutikana katika eneo la Caucasus Kaskazini, kusini kabisaa mwa Ulaya Mashariki, na siyo mbali na Bahari ya Caspian. Mji Mkuu wa Chechnya ni Grozny.
Baada ya kuvunjika kwa muungano wa Kisoviet mwaka 1991, eneo hilo liligawiwa katika sehemu mbili: Jamhuri ya Ingushetia na Jamhuri ya Chechen, ambayo ilitaka uhuru wake. Kufuatia vita ya Chechnya na Urusi, Chechnya ilipata kile kinachofanana na uhuru, lakini udhibiti wa shirikisho la Urusi ulirejeshwa baada ya vita vya vipili vya Chechnya. Mapigano ya hapa na pale yanaendelea katika milima na mikoa ya kusini ya jamhuri hiyo.

Mashambulio ya kijeshi ili kupata ushawishi wa Kremlin sio mbinu ya pekee katika miaka 22 ya Vladimir Putin katika usukani wa Urusi.
Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine sio mara ya kwanza kwa Putin kutetea masilahi yake katika jamhuri za zamani za Soviet kwa kupeleka misuli ya kijeshi.
Kwanza ilikuwa Chechnya mwaka wa 1999, kisha Georgia mwaka wa 2008, na kisha Crimea mwaka wa 2014. Lakini vita hivyo viliishaje na vinafananaje na sasa?

Vita vya kikatili - Chechnya, 1999​

Je vilikuwaje?
Septemba 1999. Vladimir Putin, wakati huo akiwa na umri wa miaka 47, alikuwa ametoka tu kuteuliwa kuwa waziri mkuu na katika miezi michache alichukua urais wa nchi hiyo baada ya kujiuzulu kwa Boris Yeltsin mwishoni mwa mwaka huo.
Kupanda kwake kunalingana na kuanza kwa vita vya pili huko Chechnya, iliyokumbukwa kwa ukatili wake na ujumuishaji wa Putin kama "mtu hodari" anayeweza kudhibiti vitisho vya ndani kutoka kwa Urusi.
Chechnya, jamhuri ambayo wakati mmoja ilikuwa sehemu ya Muungano wa Jamhuri za Kisoshalisti za Sovieti, ilipata uhuru mwaka wa 1991 licha ya upinzani kutoka kwa serikali ya Urusi.
Lakini mnamo mwaka 1994 wanajeshi wa Urusi walikwenda katika eneo hilo kukandamiza harakati hizi za uhuru.
Miaka mitatu baadaye, wanakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa waasi wa Chechen, hatimaye wakaondoka.
Hata hivyo, mwaka wa 1999, mapigano mapya kati ya raia wa Chechen na askari wa Kirusi yakaanza.
Na mfululizo wa milipuko katika maeneo ya makazi huko Moscow ambayo Kremlin ililaumu waasi wa Kiislamu wa Chechen, kwamba walichochea mashambulizi ya pili ya kijeshi ya Kirusi.
Iliishaje?
Mnamo Februari 2000, Putin akiwa rais, wanajeshi wake waliteka tena na kuharibu mji mkuu wa Chechnya, Grozny, na mnamo Mei udhibiti ulitangazwa kutoka Moscow.
Chechnya ilijumuishwa katika Shirikisho la Urusi mnamo 2003 na vita viliisha mnamo 2009, ingawa mapigano ya hapa na pale kwa njia ya vita vya msituni yalitokea.
Gharama na ukatili wa vita hivyo vilivutia ulimwengu, huku makadirio mbalimbali yakiweka jumla ya waliokufa kuwa mamia ya maelfu.
Lakini ushindi huo ulimpatia Putin ongezeko kubwa la umaarufu wake wa ndani, baada ya kuimarisha usalama na udhibiti wa jamhuri hii ya kimkakati katika eneo la Caucasus ya Kaskazini.
Leo Chechnya, ambayo ina uthabiti zaidi, iko chini ya udhibiti thabiti wa kiongozi Ramzan Kadyrov, sawa na Shirikisho la Urusi, na ambaye wakosoaji wanamtuhumu kuwa dikteta.
"Katika kesi ya vita vya Chechnya, kilichotawala katika kuingilia kati kwa Urusi ni wasiwasi juu ya usalama na mgawanyiko wake miaka michache baada ya kuanguka kwa ujamaa," Profesa Domitilla Sagramso, kutoka Chuo Kikuu cha Kings College huko London, anaelezea BBC Mundo.

Vita fupi - Georgia, 2008​

Je vilikuwaje?
Georgia, ikiwa katika njia panda muhimu ambapo Ulaya na Asia hukutana, iliibuka kuwa nchi huru kufuatia kuanguka kwa USSR mnamo 1991. Lakini ushawishi uliofuata na unaokua wa kiuchumi na kisiasa wa Marekani nchini humo ulizua wasiwasi katika nchi jirani ya Urusi, vile vile. kama matarajio yake ya kujiunga na Umoja wa Ulaya na NATO.
Vladimir Putin, akiwa na takriban muongo mmoja madarakani, pia alitumia nguvu yake.
Uhusiano wa hali ya wasiwasi wa Georgia na Shirikisho la Urusi uliongezeka kwa msaada kamili wa Moscow kwa maeneo yaliyojitenga ya Abkhazia na Ossetia Kusini, na kusababisha vita vifupi lakini vya kuua mnamo Agosti 2008.
Iliishaje?
Kufuatia jaribio la Georgia kutwaa tena Ossetia Kusini kwa nguvu, ikipambana na waasi wanaoungwa mkono na Urusi, Putin alianzisha mashambulizi ambayo yaliwafukuza wanajeshi wa Georgia kutoka Ossetia Kusini na Abkhazia.
Baada ya siku tano za mapigano ambapo mamia ya watu walikufa, pande zote mbili zilitia saini makubaliano ya amani yaliyopatanishwa na Ufaransa.
Na Urusi ilitambua maeneo hayo mawili yaliyojitenga kuwa ni mataifa huru, na hivyo kuzua maandamano huko Georgia na nchi nyingine za Magharibi.
"Georgia iligawanywa katika kile ambacho ni Georgia yenyewe na mikoa ya Abkhazia na Ossetia Kusini, ambayo hadi leo inaendelea kukaliwa na Urusi na inaendelea kuongeza ushirikiano wao na Kremlin," anasema Sagramso.
Mathieu Boulegue, mtafiti katika programu ya Urusi na Eurasia katika taasisi ya Chatham House, anaamini kwamba "Georgia ilianza kuashiria mustakabali wa sera ya kigeni ya Urusi, wakati walianza kutimiza nia ambayo tunaiona leo.

Uvamizi "laini" - Crimea, 2014​

Je vilikuwaje?
Mapema mwaka wa 2014, Crimea ilikua kitovu cha mzozo mbaya zaidi kati ya Urusi na Magharibi tangu Vita Baridi, baada ya rais wa Ukraine anayeunga mkono Urusi Viktor Yanukovych kuondolewa madarakani baada ya wimbi la maandamano yanayoiunga mkono Ulaya.
Watu wa Ukraine waligawanyika kati ya wale waliotaka ushirikiano zaidi na Urusi na wale waliounga mkono muungano mkubwa na Umoja wa Ulaya (EU), na Moscow iliamua kuingilia kati.
Kwa muda mrefu wa Februari 2014, Putin alikuwa akituma kimya kimya maelfu ya askari wa ziada kwenye vituo vya Kirusi huko Crimea.
Raia wengi "Wajitolea" pia walihamia katika rasi kukamilisha mpango ambao ulifanyika kwa siri na kwa ufanisi.
Mnamo Ijumaa, Februari 28, Urusi iliweka vituo vya ukaguzi huko Armyansk na Chongar, makutano mawili ya barabara kuu kati ya Ukraine bara na rasi ya Crimea.
Viongozi wanaoiunga mkono Urusi walidai kuwa walihitaji kuwalinda wahalifu dhidi ya "watu wenye itikadi kali" ambao walichukua mamlaka huko Kiev na kutishia haki zao.
Mnamo Machi 16 walipanga kura ya maoni ambayo idadi ya watu iliulizwa ikiwa wanataka jamhuri inayojitegemea ijiunge na Urusi.
Ukraine na Magharibi ziliichukulia kura hiyo ya maoni kuwa ni kinyume cha sheria, huku Urusi ikiiunga mkono vikali.
Kulingana na maafisa wa eneo hilo, 95.5% ya wapiga kura waliunga mkono unyakuzi wa Urusi wa Crimea.
Iliishaje?
Mnamo Machi 18, siku mbili baada ya kuchapishwa kwa matokeo, Putin alifanya uvamizi rasmi kwa kutia saini mswada unaojumuisha Crimea katika Shirikisho la Urusi.
Mwandishi wa BBC John Simpson, ambaye alikuwa Crimea wakati huo, aliandika kwamba ulikuwa uvamizi "laini" zaidi katika nyakati za kisasa.
"Operesheni ilikuwa ya haraka sana ambayo ilishangaza wengi," anaelezea Sagramso.
"Kwa mara nyingine tena, umaarufu wa Putin uliongezeka sana miongoni mwa Warusi kwa sababu hakukuwa na umwagaji damu na ilionekana kama ustadi mkubwa," anaongeza mtaalamu huyo.
Wakati mgogoro wa Crimea ulitatuliwa kwa njia hii, mzozo kati ya waasi wanaounga mkono Urusi katika eneo la Donbas na Ukraine ulizidi kupamba moto, na kuweka msingi wa Putin kuhalalisha kuivamia Ukraine miaka nane baadaye.

Je, uvamizi huu unaweza kulinganishwa na kile kinachotokea Ukraine?​

Kila moja ya vita hivi imekuwa ya kipekee, lakini wataalam huchora mistari kadhaa inayolingana, ikijumuisha maono ya kibeberu ya Kremlin, mtazamo wake wa usalama na nia yake ya kubaki na ushawishi katika jamhuri za zamani za Soviet.
Hata hivyo, wanaonya kwamba motisha za uvamizi wa Ukraine ni kuwa tofauti "kabisa "na migogoro mingine na "mwisho" ni vigumu kutabiri.
Putin anasisitiza kwamba hii sio vita wala uvamizi, bali ni "operesheni maalum ya kijeshi" ya kutetea idadi ya watu wazungumzaji wa Kirusi katika mkoa wa Donbas.
Lakini leo miji kuu ya Ukraine imezingirwa na vikosi vya Urusi, pamoja na mji mkuu.
"Urusi inataka kujisalimisha bila masharti ya kisiasa na kijeshi kwa Ukraine yote. Inataka utii wake na kuondolewa kabisa kijeshi," Boulegue anachambua.
Sagramso anaongeza kuwa moja ya tofauti kuu na kesi za Chechnya na Georgia ni "ukamilifu wa kihemko wa taifa kubwa."
"Putin ametaja mara nyingi ukweli kwamba raia wa Ukraine na Warusi ni watu sawa. Kwake ni hali ya bandia ambayo haipaswi kupitisha sera ya Ulaya," anasema.
Kutafuta vidokezo kuhusu jinsi uvamizi wa Ukraine utaisha katika kile kilichotokea Chechnya na Georgia inaonekana kuwa ngumu, kati ya mambo mengine, na upinzani wa jumla wa watu wa Ukraine.
"Haionekani kama Ukraine itasalimu amri na hatujui ni nini hasa Kremlin itazingatia mafanikio, itafika wapi na mkakati gani wa kumaliza vita," Boulegue anahoji.
Kwa maana hii, anasema, jambo la kutia wasiwasi zaidi ni kwamba "hii inaonekana tu kuwa mwanzo, awamu ya kwanza ya kile ambacho kinaweza kuwa miongo ya athari kwa ulimwengu wote."
 
Shukrani nazidi kupata Shule walimu wangu
 
Hivi kwa nini Ukraine asikubali yaishe naamini Mrusi atamjenga upya endapo atanyanyua mikono juu
 
Back
Top Bottom