cutelove
JF-Expert Member
- Oct 3, 2017
- 3,317
- 7,509
Wagombea wote waliochukua fomu na kuzirejesha wameunguliwa katika vijiji 60 kati ya 78
Wagombea hao ni wa vyama vya upinzani, kwa mujibu wa James Mbatia,hata yule ambaye amepewa fomu ya kumpitisha kugombea,ameanza kulazimishwa airejeshe kwa msimamizi wa uchaguzi
===
MBATIA: WAGOMBEA WA NCCR KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA JIMBO LA VUNJO WAMEENGULIWA WOTE
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia amedai Wanachama wa chama hicho waliochukua fomu kugombea uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika jimbo la Vunjo, wameenguliwa wote
Amesema “Waliamua kufanya uteuzi na kubandika fomu za majina ya Wagombea Novemba 4 badala ya Novemba 5, 2019 kama Kanuni na ratiba ya Uchaguzi inavyoelekeza.”
Ameongeza “Huwezi kuamini Wagombea wetu wote Jimbo la Vunjo wameenguliwa. Mchezo uliofanyika ni hatari kwa usalama wa nchi na tayari nimeiandikia Serikali barua ya malalamiko,"
Aidha, amesema "Katika Kijiji cha Komakundi eneo la Njiapanda ya Himo, Msimamizi Msaidizi alimpatia Mgombea wetu fomu ya kuteuliwa na hivi sasa wanashinikiza airejeshe, agizo ambalo tumeligomea."