James Mbatia: Sitoshiriki vikao vya Bunge vilivyobaki

James Mbatia: Sitoshiriki vikao vya Bunge vilivyobaki

vevenononombo

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2015
Posts
1,289
Reaction score
421
James Mbatia ametangaza kutounga mkono mwenendo wa bunge na amesema hatashiriki vikao vilivyobaki.

====================

Mbunge wa kuteuliwa na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi, James Mbatia, amesema hakuna Spika aliyewahi kuonyesha udhaifu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama alivyoonyesha Anna Makinda.

Amesema Makinda ameligawa vipande vipande Bunge la 10 na kutumiwa na mhimili wa utawala.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mbatia alisema badala ya Bunge kuisimamia serikali, lakini Makinda ameshindwa kuliongoza Bunge hilo kutokana na shinikizo la mhimili wa utawala na kulazimika kufuata matakwa ya CCM na hivyo kuliongoza kwa ubabe.

Alisema tofauti na ilivyokuwa katika kipindi cha Samuel Sitta na Pius Msekwa ambao walionyesha weledi na kuliongezea heshima Bunge, lakini Makinda ameriharibu kutokana na kuacha kusimamia Katiba ya nchi katika kuliongoza Bunge hilo.

"Siku zote mwanamke ndiye huwa ni mtu wa mwisho kuligawa Taifa, lakini limekuwa ni jambo la ajabu sana kuona mwanamke huyo ambaye angekuwa mstari wa mbele katika kuitetea nchi hii, lakini ameamua lifie mikononi mwake, hata bila kuficha ameonyesha wazi kwamba anatumika na serikali na CCM, Makinda yeye siyo kiranja wa bunge ni mratibu tu," alisema Mbatia.

Aliongeza: " Badala ya Bunge kusimamia serikali kama Mhimili unaojitegemea, limejivua kazi yake na kuwa kiungo cha serikali na inalisimamia, na ndiyo maana hata juzi mlisikia Serikali inasema imeoliongezea Bunge siku, badala ya Bunge lijiongezee lenyewe, hii ni fedheha."

Mbatia alisema suala la kupelekwa bungeni kwa hati ya dharura na kujadiliwa miswaada mitatu ya mafuta na gesi ni ajenda ya siri ya kutaka kuiweka gesi kama dhamana ya CCM ya kupata fedha ya uchaguzi na kwamba hicho ni kiashiria cha kuanza kuiuza nchi rejareja.

"Raslimali hizi badala ya kuwa neema kwa Watanzania, sasa inakuwa balaa, watu wachache wanataka kuwaibia Watanzania, hivi unawezaje kuwekaje miswaada hii muhimu kujadiliwa kwa pamoja na kuipeleka harakaharaka hivyo, sisi tumesema hatukubali kuona hujuma hizi zinafanyika dhidi ya rasilimali na Taifa," alisema Mbatia.

Mbatia alisema msimamo wa Wabunge wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) uko wazi, kwamba hawako tayari kujadiliwa miswaada hiyo kwa hati ya dharura na pia hawatashiriki wakati wa kuvunjwa bunge hilo Julai 9, mwaka huu.

Pia aliongeza kuwa hata wakiitwa katika meza ya maridhiano na Makinda hawatakuwa tayari kushiriki.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alipoulizwa juu ya taarifa hizo za kwamba chama hicho kina ajenga ya siri ya kuifanya gesi kusaidia kuwa dhamana katika uchaguzi, alijibu kwa kifupi kwamba ni uzushi.

Chanzo: Nipashe
 
Mh. James mbatia ametangaza kutounga mkono mwendendo wa bunge na amesema hata shiriki vikao vilivyobaki chanzo nikituo cha luninga cha channel ten leo habari

Ina make sense,what about his counterpart - Mbowe hasn't say anything yet?
 
huo unapaswa kuwa msimamo rasmi wa wabunge wote wa ukawa. kinachofanyika bungeni ni uvunjaji wa wazi wa katiba,sheria na kanuni za kudumu za bunge. bunge lile limepoteza hadhi yake limebaki kama muhuri tu wa serikali kupitishia mambo yake..
 
Mi nilijua wabunge wote wa upinzani walipigwa ban ile jana, kumbe kuna wengine walibakia?
 
Kwa sasa aingie wala asiingie haina impact tena kwani huo mswaada umeshapitishwa leo. Ninachotaka kujua sasa Ukawa watashiriki kikao cha kufunga bunge hiyo wiki ijayo tarehe 9 july 2015? Kwasababu naona kamati ya maadili walitoa maamuzi ya mhemuko ikiwepo na taarifa ya uwongo kuwahusu mh. J. Thelathini na yule wa Znz kwamba walijutia makosa yao. Naona leo Thelathini aliomba mwongozo na spika akaendeleza jazba mpaka Thelathini kuamua kutoka nje ya bunge.
 
Back
Top Bottom