James Mbatia na Maalim Seif ni zaidi ya JK - wana uthubutu!

Chigwiyemisi

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
531
225
Siku za hivi karibuni tumeshuhudia migogoro kadhaa ndani ya vyama vya siasa. Migogoro mikubwa ilikuwa kwenye vyama vitatu, CCM, NCCR-Mageuzi na CUF. Yaliyotokea wote tumeyaona. NCCR wamemfukuza Mbunge wao David Kafulila na CUF wamemfukuza mbunge wao Hamad Rashid. Sina uhakika kama migogoro ndani ya vyama hivyo itafikia mwisho ama laa ikizingatiwa kuwa wote waliofukuzwa wameshitaki mahakamani. Lakini kwa mtazamo wangu nimeona nia na uthubutu walionao viongozi wa vyama hivi viwili katika kushughulikia matatizo yao! Sitaki kuzungumzia kama wameonewa au hawajaonewa lakini uthubutu ni ishara ya ukomavu kiuongozi.

Kwa upande wa CCM, wadau wote wanaofuatilia siasa wanajua jinsi ambavyo chama hiki kimepata shida kutekeleza falsafa yake ya kujivua gamba. Kila kinapojaribu kung'ata kiungua moto mdomoni na kutema! Mwenyekiti wake ameshindwa kabisa kuchukua hatua dhidi ya wale wanaoitwa mafisadi kwenye chama chake! Huu ni udhaifu mkubwa sana kwa kiongozi mkubwa katika chama chochote kikubwa cha siasa. Ameruhusu watu kuwa maarufu zaidi ya chama! Failure, failure, failure!

Kwa misingi hiyo nimelazimika kuona kuwa Mbatia na Maalim Seif wana uthubutu kuliko JK!
Jadili!
 
Wanaotuhumiwa CCM ndo waliomuweka JK madarakani, atathubutu vipi kuwapiga chini? Akijaribu tu na yeye anaondoka. Atajuta kuwa rais
 
Umesaha kuwa RA alisema amechoshwa na siasa za CCM ndzo zlizo mfukuza nasema CCM wana aina yake ya kufukuza wanachama wake
 
CCM ilikufa siku nyingi kama chama cha siasa. Wamebakia na dola. Utakuwa ujinga kujivua gamba ambako mwisho wa kujivua gamba watajikuta wamepoteza na hiyo dola na kubaki historia kwamba kuliwahi kuwepo chama cha CCM.
 
Ukumbuke kuwa seif na mbatia walikuwa wanatishiwa kutapishwa vitumbua vilivyomo mdomoni mwao na ndio maana wakawawahi wale wenye nia ya kufanya hivyo (kafulila na hamad), sina shaka hata jk akitokea mtu anayetishia kumkaba koo ili atapike kile kilichopo mdomoni mwake wakati huu bila shaka atafanya kama wenzie walivyofanya hivi sasa na ndio maana ccm wanauchaguzi mwaka huu lakini sijasikia hata mmoja kati yao anayesema kwamba jk chama kimemshinda kwa hiyo mwaka huu atachuana naye kwenye uenyekiti, kwani kuna mtu asiyejua kuwa jk kasababisha chama kiwe mdebwedo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom