Jambo tz: Mbunge simbachawene-ccm na khalifa -cuf

Nyakageni

JF-Expert Member
Feb 1, 2011
15,045
5,092
wakuu hebu tazama TBC1 hawa wabunge wanatetea mswada wa kuandaa tume ya ukusanyaji wa maoni ya kuandaa katiba
 
CUF ilishajichimbia kaburi hata MTATIRO afanyeje haiwezi kufufuka kwa ujinga wa hawa wabunge wake
 
CUF ilishajichimbia kaburi hata MTATIRO afanyeje haiwezi kufufuka kwa ujinga wa hawa wabunge wake

hili liko dhahiri mkuu! Wanaboa kweli hawa TBC1 yaani hata kuweka mbunge wa upinzani hakuna?
 
Elisha eliya haya maswali haya anayowapiga hawa jamaa namkubali yupo kwenye weledi hasa hata kama anataka upande fulani unafaike tatizo ninaloliona hapa ni absence ya lisu/kafulira/zito/mkosamali na pia yule bwana machary ambaye tangu awali jana aliomba muongozo mara tu baada ya aunt celina kumaliza , kamati ilipomaliza, lisu alipoomba bunge liondoe mswaada ila akanishangaza alibaki ukumbini wakati wenzake wa nccr waliondoka.....
 
Huyu mzee wa cuf khalifa anakubaliana na cdm juu ya kukiukwa kwa maelekezo ya awali ya spika mwenyewe juu ya umma haukufikiwa, sasa napata picha khalifa anaugua sana na kitendo cha cdm kupinga mfumo wa kubembelezana na wazanzibar ktk mambo ya kitaifa tu!!~!!
 
Angalau hii program imeenda kuwa balance kwa nguvu za hoja za presenter mwenyewe na siyo waalikwa simbachawene wala khalifa, waberoya nilisoma hoja zako za kuifunda cdm ila wengine waligundua kitu tofauti juu yako ktk dodoso ulilolijibu baada ya kudodoswa na mtoa hoja....tunakuomba sasa utupe picha ya nini outcome ya sekeseke la jana? Je cdm waige utamaduni wetu wa kuwaogopa wanzanzibar? Maana Mh. Khalifa anawasifia waTZ kwa kuwanyima nchi CDM kwani amewabainisha wazi kuwa hawa ndio maadui wa ukweli wa Muungano wa wetu? Huu ni wimbo tuliokuwa tunauimba against CUF huko nyuma lakini sasa CUF wanawaita CDM ni maadui wa umoja wetu, wadini na tunawasaidia ktk kuimba wimbo huu je maoni yako yanabaki palepale dhidi ya CDM??? Sisi tunatokaje baada ya hawa vijana CUF na CDM kuumana ? Ktk hili nitaomba uwe waziwazi kama mzee mwanakijiji/Masanilo/Invisible na kada yao humu jamvini
 
Khalifa suleiman Khalfa anasema Tundu Lissu amewatukana sana wazanzibar, sasa mimi nimeshindwa kuelewa aliwatukanaje.
 
TBC hawajawa balanced kwa nini hawaja wachukua wabunge wa CDM au NCCR wale walio toka nje ukumbi wa bunge ili kubalance story vizuri
 
Khalifa suleiman Khalfa anasema Tundu Lissu amewatukana sana wazanzibar, sasa mimi nimeshindwa kuelewa aliwatukanaje.
kweli amewatukana tena tusi baya pale LISSU alipoonesha hamna habari za kuwabembeleza wazanzibar ktk huu MUUNGANO.
Unajua wazenji wamezoea kuombwa na kuogopwa sasa LISSU hataki hii tabia iendelee
 
Usicheze na Lissu, yeye ni ukweli daima...wala hajaanza ukubwani. Si rahisi wala urojo wakamuelewa Lissu. Nashukuru Mungu jimboni kwetu tulimwelewa tukampa kazi ya kulisaidia taifa hili....go Lissu gooo.....

"Njaghamba iuhoma ilolo mnyampaa Lissu"
 
Usicheze na Lissu, yeye ni ukweli daima...wala hajaanza ukubwani. Si rahisi wala urojo wakamuelewa Lissu. Nashukuru Mungu jimboni kwetu tulimwelewa tukampa kazi ya kulisaidia taifa hili....go Lissu gooo.....

"Njaghamba iuhoma ilolo mnyampaa Lissu"

Huyu ni mtani wangu lakini ni bonge la mtu hatari sana katika nchi hii, maana pamoja na kuwa mwanasheria amekuwa akikiuka mambo mengi yanayohusu sheria, na amekuwa mnafiki sana,, anajiona huyo na anadharau sana hata kwa wabunge wenzake ,, kale ka asili ya kwao anataka kukaleta bungeni,..
 
lengo zima hapo ni kuhadaa wananchi ili waone mswaada hauna kasoro na ndio maana hawawezi kuwaita wabunge wa chadema hapo...by the way mi nafikiri mwognozo utolewe ili moja lijulikana ...tujipange sisi wananchi na tulianzishe
 
Tatizo la CUF ni kwamba haya haya anayo yalalamikia Lissu ndiyo msingi wa
malalamiko ya miaka mingi ya CUF kuhusu KERO ZA MUUNGANO. Lakini kwa
kuwa wanamuogopa bwana yao CCM pembeni, badala ya kumu-support
Lissu wanampinga, wao wanafikiri kupeleka barua UN, ndiyo litakuwa suluhisho
la Muungano wakati fursa wanayo ya kutumia BUNGE la JMT.

Hongera Lissu kwa kuuweka UKWEli dhahiri, achana na hao Karume-Kenge!
 
CUF ilishajichimbia kaburi hata MTATIRO afanyeje haiwezi kufufuka kwa ujinga wa hawa wabunge wake

Mimi nilikuwa namkubali sana Mtatito alipokuwa UDSM na alipokua waziri mkuu wa DARUSO na nilikuwa namkubali sana kwa harakati zake za kuwatetea wanafunzi wa UDSM wakati huo, ila kwa jinsi alivyoamua kujiunga na chama cha CUF amepotea na ameingia kwenye kundi lisilokuwa natija kwa wananchi, KWA USHAURI WANGU WA BURE KWAKE NAMUOMA AHAME CUF KABLA CV YAKE HAIJACHAFUKA SANA ...
 
Cuf wamenyamaziishwa sana na ndoa tete na ndiyo maana hoja ya kero za muungano si moto tena..Sasa hapa kila mmoja awe huru kabisa na hakuna taifa kuogopa..Ukweli ni huo na kama Muungano ni kufa ufe na kama ni kuboreshwa kwa ukweli na si kinafiki uwe..Peoples Power
 
Huo ni mfano mbaya sana wa wabunge.
Wanaongea kama wananchi wanaowasikiliza ni wachovu wa kufikiri kiasi hicho na kwamba hawawezi kuelewa kinachoendelea bungeni.
Mwanzo mbaya huleta mwisho mbaya. 'gabbage in, gabbage out'
Matayarisho ya mswada ni 'feki', hata katiba itakavyo undwa itakuwa 'feki' na hakutakuwa na jipya.
Hii ni danganya toto.
Bunge linatumika kama Rubber stamp ya watu hata si serikali.
 
Huyu ni mtani wangu lakini ni bonge la mtu hatari sana katika nchi hii, maana pamoja na kuwa mwanasheria amekuwa akikiuka mambo mengi yanayohusu sheria, na amekuwa mnafiki sana,, anajiona huyo na anadharau sana hata kwa wabunge wenzake ,, kale ka asili ya kwao anataka kukaleta bungeni,..

Sidhani kama uinafahmu huyu jamaa aiseee! Jamaa ni humble ile mbaya, ila ni jasiri kupindukia, haogopi mradi naona kuna haki.
 
Back
Top Bottom