Jambo limezua jambo, kumbe siri ndio hii!!!!!!

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,891
155,895
Kila mtu amepewa fursa ya kupata nguvu kubwa zaidi katika asili, nguvu iliyomuumba na inayomtawala! Hakuna haja ya kuamini katika uwepo wa nguvu hii kubwa, kwani inaweza kuchunguzwa na kujulikana kupitia ukweli. Kwa njia hii, mwanadamu anapata maana ya maisha na uzima na milele.

Kitu kinachoitwa Muumba ni nguvu kubwa mno na nguvu hiyo huitwa nia au dhamira ya kutoa ("will to bestow") au nguvu ya upendo. Ili kutimiza asili yake, Muumba alihitaji kitu ambacho kwacho angeweza kutoa sehemu ya upendo wake. Hivyo aliumba "chombo" kinachoitwa nia au dhamira ya kupokea ("will to receive") au nguvu ya chuki. Huu ndiyo ulikuwa uumbaji wa Mungu wa pekee wa mwanzo. Yaani, Mungu aliumba nguvu mbili tu mwanzoni: Upendo na Chuki. Nguvu nyingine zote zilitokana na nguvu hizo mbili! Aliumba kitu kutoka katika kitu kisichokuwepo. Yaani, aliumba kuwepo kutokana na kutokuwepo.

Kwa hiyo, kulianzishwa nguvu mbili tu hapa ulimwenguni – Kutoa na Kupokea – ambazo ni nguvu mbili zinazopingana. Kanuni hii, kwamba hakuna chochote kinachoweza kujulikana bila kujua pia kinyume chake, inarujidia wakati wote katika asili yetu. Kadiri nguvu hizi zinavyoingiliana, kwa kupitia madaraja manne ya asili, roho ya umma (roho ya Adamu) ilisambaratika kutokana na dhambi ya Adamu. Tukio hili, kusambaratika kwa roho ya Adamu, ndilo kisayansi linaloitwa "Big Bang".

Katika kipindi cha mabilioni ya miaka tangu "Bing Bang" itokee, roho ya umma iliposambaratika, kutokana na dhambi ya Adamu, maisha yamekuwepo hapa duniani kupitia madaraja manne ya uwepo. Madaraja hayo ni: "Still" (daraja la vitu visivyokuwa na uhai: dhamira ya kutimiza mahitaji ya msingi), "Vegetative" (daraja la mimea: tamaa ya utajiri), "Animate" (daraja la wanyama: tamaa ya madaraka) na "Speaking" au "Human" (daraja la wanadamu: tamaa ya maarifa).

Kwa maneno mengine, maisha yamegawanyika katika madaraja manne ya asili: daraja la vitu visivyokuwa na uhai, daraja la mimea, daraja la wanyama, na daraja la wanadamu. Kila daraja lina mfumo wake wa maisha, uliotokana na dhamira ya kupokea na kutoa kutoka kwa Mungu.

Daraja la vitu visivyokuwa na uhai ni daraja la vitu mfu kama vile miamba, sayari, na kadhalika. Daraja hili lina kiwango kidogo sana cha dhamira ya kupokea ("will to receive") kutoka kwa Muumba, kwa lengo tu la kudumisha umbo au sura za vitu hivyo. Yaani, daraja hili lina kiwango kidogo sana cha maisha.

Katika daraja hili hakuna kipimo chochote cha ufahamu wa kiroho, wala hakuna udhibiti juu ya tamaa ya kibinafsi, isipokuwa utumwa kamili dhidi ya mazingira yake.

Katika daraja la mimea kuna mfumo wa ukuaji. Kwa sababu kuna dhamira kubwa zaidi ya kupokea kuliko ile ya daraja la vitu visivyokuwa na uhai. Kuna uelewa wa mambo ya nje ya mazingira yake, na kuna uwezo wa kupokea kile kinachofaa na kutoa kile kisichofaa.

Kwa upande wa tabia za wanadamu, sifa za daraja hili la mimea zinadhihirishwa na watu pale watu wanapokuwa na tamaa ya kujikusanyia pesa na mali kama nyongeza ya kuishi vizuri zaidi kuliko wengine. Ukiwa na tabia ya namna hiyo, hiyo asili umeiiba kutoka kwenye asili ya mimea.

Hata hivyo, dhamira ya kupokea ya daraja la mimea bado ni dhaifu lakini lina uwezo wa kuzuia tamaa yake na lina uwezo mdogo wa dhamira ya kutoa. Yaani, mimea haina uwezo wa kusaidiana. Ndiyo maana ya dhamira ya kutoa.

Mimea hupokea kile kinachofaa na hutoa kile kisichofaa. Kwa mfano, mmea hupokea kabonidioksidi kutoka kwa wanadamu na kuibadilisha kuwa oksijeni ambayo hupokelewa tena na wanadamu. Wanadamu hupumua kabonidioksidi kusheheneza mimea, na mimea hupumua oksijeni kusheheneza wanadamu. Yaani, kila mmoja hupata faida katika mzunguko huu usioisha wa kutoa na kupokea. Hayo ndiyo maisha katika ubora wake.

Tofauti na daraja la kwanza, la vitu visivyokuwa na uhai ambapo tumeona kiwango kidogo sana cha maisha, katika daraja hili la mimea tumeona angalau kiwango kikubwa kidogo cha maisha; ingawa si kikubwa kama kiwango cha maisha cha daraja linalofuata.

Katika daraja la wanyama (pamoja na viumbe wengine wote hai isipokuwa wanadamu) wanyama wana uwezo mkubwa wa kutembea. Aidha, wana tamaa kubwa inayozidi tamaa ya madaraja mawili niliyoyaelezea hivi punde; yaani, mimea na vitu visivyokuwa na uhai. Hali hii hulifanya daraja hili liwe na udhibiti mkubwa zaidi juu ya mimea na vitu visivyokuwa na uhai.

Kila mnyama hupendelea nafsi yake mwenyewe kwa namna ambayo itamfaidisha yeye, katika kuchagua kati ya mema na mabaya kwa ustawi wake mwenyewe. Kwa maneno mengine, kila mnyama ana asili ya ubinafsi uliokithiri.

Wanyama huzaa na uhitaji wenzi kuweza kufanya hivyo. Kitendo hiki kinamwakilisha Muumba; kwa kuwa kiumbe mpya anazaliwa, na maisha yanaonekana bayana.

Kwa wanadamu daraja hili (au asili hii) hudhihirishwa duniani kama nguvu ya kisiasa, mamlaka, au udhibiti katika mambo madogo kama vile masuala ya nyumbani au kazini. Kwa maneno mengine, uchu wa madaraka, utajiri, na kadhalika, ni asili ya wanadamu kutoka katika asili ya wanyama; kwani asili ya wanyama imejaa ubinafsi, na ubinafsi wa wanadamu tumeutoa katika asili ya wanyama.

Lakini katika daraja la wanadamu, wanadamu walitokea duniani baada ya kila kitu kutayarishwa katika asili kwa ajili yetu. Yaani, tulitokea baada ya msingi wa maisha kuwepo katika asili yetu.

Muundo wa asili nzima, kama ilivyoelezwa hapo awali, ni mfumo uliochangamana sana unaoweza kufananishwa na mfumo mzuri wa matairi ya meno – yaliyolainishwa kwa oili safi – kwa pamoja yakiendesha na kudumisha mazingira mazuri ulimwenguni, ambayo hutoa kila kitu tunachokihitaji ili tuishi.

Sasa; baada ya kuzielezea asili zote nne zilizoko ndani ya maisha ya vitu visivyokuwa na uhai, mimea, wanyama na wanadamu, maisha ni nini?

Maisha ni dhamira ya kupokea upendo kutoka kwa Mungu na dhamira ya kutoa upendo kurudi kwa Mungu. Maisha ni upendo; upendo wa Mungu kwa viumbe wake, na kinyume chake. Hata kama humpendi Mungu yeye anajua unampenda, kwa sababu upendo wake hauna mipaka.

Kila kinachotokea hapa ulimwenguni ni tafsiri ya dhamira ya kupokea ("will to receive") pamoja na dhamira ya kutoa ("will to bestow") kwa sababu dhamira ya kupokea na dhamira ya kutoa ndizo zilizounda asili yetu. Nguvu hizi: Kupokea na Kutoa, zijulikanazo pia kama nguvu ya chuki na nguvu ya upendo kwa mfuatano huo, ndiyo asili na maana ya maisha.

Bila asili kuumbwa maisha yasingekuwepo. Labda yangekuwepo kwa mapenzi ya Mungu mwenyewe! Lakini hata Mungu mwenyewe alitumia asili kumuumba binadamu wa kwanza.

Kwa hiyo, kila kitu ni udhihirisho wa dhamira ya kupokea na kutoa; kwa sababu ndiyo msingi wa asili yetu. Dhamira hizi, au nia hizi, ndicho kiini cha chimbuko la maisha ulimwenguni.

Madaraja manne ya asili huunda kigezo kinachorudufiwa katika kila daraja la uwepo, katika historia ya mwanadamu na katika moyo wa mwanadamu. Yanadhihirisha ufundi mkubwa na bora zaidi wa Muumba, muundo kamilifu na jumuishi ambamo viumbe wote tunaishi.

Maisha ni Dunia. Dunia ni Basi. Sisi ni wasafiri. Anayekufa amefika mwisho wa safari yake. Safiri salama.

-Enock Maregesi, mwandishi wa Kolonia Santita
 
Unacopy ma vitu huko bila reference yoyote unatuletea hapa. una assume nini sijui
 
Kila mtu ana assumptions zake kuhusu Dunia na umauti lakini all in all itabakia kua theories tu bila exact proof na hakuna ushahidi unaweza kuja kupatikana kuhusu theory hii so kilichopo ni kumtumainia muumba/ maanani baaasi hayo mengine yasiyoweza pata uthibitisho wa moja kwa moja tuachane nayo
 
Usiwe dodoki, uwe unatafakari kuliko kukubali hadi ujinga. Amini Mungu yupo uende umkose kuliko kuamini hayupo halafu ukienda umkute, itakuwa ni kilio na kusaga meno.
 
Maisha ni Dunia. Dunia ni Basi. Sisi ni wasafiri. Anayekufa amefika mwisho wa safari yake. Safiri salama.

kwa kauli yako hii unatuaminisha kuwa wale wanatuhubiria kuwa kuna maisha baada ya kifo ni warongo?
 
Back
Top Bottom