Jambazi aliyetupwa jela anaswa katika piga nikupige

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,073
1,250
POLISI jijini Dar es Salaam inawashikilia watu watatu akiwemo mmoja ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 60 jela, wanaodhaniwa kuwa ni majambazi waliopora silaha ya askari.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema watuhumiwa hao walikamatwa juzi saa 7 usiku wakiwa na silaha mbili pamoja na risasi 45.

Kova alisema majina ya watuhumiwa hao yamehifadhiwa kwa sababu za upelelezi na kuwa watuhumiwa hao wamekuwa wakijihusisha na matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha akiwemo mfungwa mmoja.

“Ninashangazwa sana na huyo mtuhumiwa mmoja ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 60, lakini bado yupo uraiani anafanya uhalifu,” alisema Kova.

Kwa mujibu wa Kamanda Kova, mwaka 2003 mshitakiwa alihukumiwa kifungo cha miaka 60 jela katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Alisema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo pamoja na wenzake, kumefanyika ndani ya saa 29 ikiwa ni muda mfupi baada ya kuporwa kwa silaha saa 2.15 usiku wa Desemba 12, mwaka huu katika lindo la Benki ya Akiba Tawi la Mwananyamala ambapo askari namba G128
Konstebo Fikiri, aliporwa akiwa lindoni.

Alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunatokana na taarifa za kiintelijinsia, ufuatiliaji, umakini na mapambano makali kati ya polisi na watu hao waliokuwa kwenye gari namba 1200 BLV Toyota Mark II Grand.

Alisema gari hilo lilikamatwa baada ya kupinduka katika Barabara ya Mandela karibu na kiwanda cha ngano cha Azam wakati wakifukuzana na polisi huku wakirushiana risasi.

Kova alisema watuhumiwa hao walipora bunduki aina ya SMG yenye namba 00430 ikiwa na risasi 30 wakati askari huyo akiwa kazini pamoja na mlinzi kutoka katika Kampuni ya Ulinzi ya Ultimate, Job Emmanuel (28).

Aidha, alisema washitakiwa hao walikutwa na magari mawili yenye namba T200 BLV, Toyota Mark II Grand gari lenye namba T350 BHJ aina ya Toyota na simu nane za mkononi. Mali hizo zimetambuliwa na wamiliki wake.
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
56,226
2,000
Kweli magereza ya Tanzania yako wazi kwa watuhumiwa kutoka muda wowote wanaojisikia, ili mradi uwe na hela
 

Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
7,420
2,000
Kweli magereza ya Tanzania yako wazi kwa watuhumiwa kutoka muda wowote wanaojisikia, ili mradi uwe na hela

Yes, hakuna lisilowezekana Tanzania. Ikiwa Rais anaingia Ikulu ki-mushkeli mushkeli, kwa nini mfungwa jambazi asipewe off ya magereza ya masaa kadhaa kwenda ku-practice experience yake asiisahau?
 

Somi

JF-Expert Member
Feb 7, 2009
1,389
2,000
Nahodha na mkuu wa magereza wajiuzulu kwa hiari yao, wakikataa kikwete awaondoe. Hii inanikumbusha magereza ya mexico ambapo wafungwa wa kesi za madawa ya kulevia wanapowahonga wakuu wa magereza na kutoka nje kufanya uhalifu tena kwa kutumia silaha za magereza waliyofungwa. Nafikiri tanzania ni nchi pekee duniani kiongozi anafanya madudu na anaendelea kuwepo madarakani
 

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,716
2,000
risasi 30, wangekufa watanzania 30, heunda hata wakina Liyumba wapo mitaani, kwa magerza hii, sio hatari bali ni zaidi ya hatari,
 

Gsana

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
4,398
1,500
Sasa mgt software,unashauri tumshauri j.kikwete kuunda tume ili wajue kama watu tuliowatunza jela wamo? Au tuwe tunaita majina kila jioni? Au sisi wahasibu tupewe kazi ya kufanya Audit ya wafungwa kila cku? Tusije tukakuta magereza yako empty yan wote wako likizo. Sasa tumempa mbu kazi ya kutibu malaria sugu!
 

kinya

JF-Expert Member
Feb 20, 2009
495
225
Halafu utashangaa hili suala litaisha kimya kimya bila mtu kuwajibika!!!!!!

uwajibika hivi ni mpaka kwenye taaluma kwa tz?Mi sikujua nilifikiri kwenye sihasa tu kwani watoto na akina mama wanakufa kwenye ile hospital sijawahi kusikia ujibikaji pale.
 

Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,605
2,000
Halafi limeshakuwa kimyaaaaa wamelinyamazisha
Watanzania inabidi tuamke tulipolala:A S-alert1:
 

Fugwe

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
1,679
1,250
Kova amekurupuka kuhusu huyo mfungwa. Je, amewasiliana na Mkuu wa Jeshi la Magereza kujua kulikoni? Tatizo hapo ni two different systems operating on the same clients. Polisi anapokamata na kupeleka kesi mahakamani kwelie mtuhumiwa akikutwa na hatia anafungwa na hapo ndipo kazi ya polisi inapoishia. Magereza wanakazi ya kuwapokea na kuwahudumia wafungwa. Wakiwa gerezani wafungwa wanahaki ya kukata rufaa dhidi ya hukumu walizopewa na mahakama. Mfungwa anaposhinda rufaa yake, anaachiliwa mara moja. Hapa Magereza hawalazimiki kuiarifu polisi kuhusu kuachiliwa kwa mfungwa. KOVA angewasiliana kwanza na Mkuu wa Magereza ili ajue mfungwa huyo ni kwanini yupo nje ya gereza. Mimi ni hayo tu!
 

emrema

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
268
0
Nakubali uliyosema Fugwe lakini Magereza zina mushkeli hapa Arusha mwaka 2000 vijana 2 waliohukumiwa miaka 30 katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha kwa armed robbery walitolewa magereza kwa nguvu ya mfuko baada ya miezi 3 tu ninawafahamu walipewa sharti wahame mkoa, Baadae 2005 mmoja alikamatwa tena kwa makosa hayo hayo. Mwingine alihamia Tanga ila bado huwa anakuja Arusha occasionally na kufanya uhalifu. MAGEREZA ISAFISHWE.
 

Bobo Ashanti

Member
Nov 4, 2010
49
0
Kova amekurupuka kuhusu huyo mfungwa. Je, amewasiliana na Mkuu wa Jeshi la Magereza kujua kulikoni? Tatizo hapo ni two different systems operating on the same clients. Polisi anapokamata na kupeleka kesi mahakamani kwelie mtuhumiwa akikutwa na hatia anafungwa na hapo ndipo kazi ya polisi inapoishia. Magereza wanakazi ya kuwapokea na kuwahudumia wafungwa. Wakiwa gerezani wafungwa wanahaki ya kukata rufaa dhidi ya hukumu walizopewa na mahakama. Mfungwa anaposhinda rufaa yake, anaachiliwa mara moja. Hapa Magereza hawalazimiki kuiarifu polisi kuhusu kuachiliwa kwa mfungwa. KOVA angewasiliana kwanza na Mkuu wa Magereza ili ajue mfungwa huyo ni kwanini yupo nje ya gereza. Mimi ni hayo tu!
pamoja na maelezo ya busara uliyotoa ndugu fugwe,kaa ukijua kwamba ni ukweli usipingika kwamba kuna mchezo ambao umekuwepo ktk magereza yetu kwa miaka mingi ambapo wafungwa waliohukumiwa hawatumikii vifungo hivyo ndani ya magereza bali kwa kutoa pesa huwa wanaachiwa.mchezo huo hufanywa na maafisa wasio waaminifu kutoka idara za magereza,mahakama, polisi na hata hospitali.kinachofanyika ni kutengeneza mazingira kuonyesha mfungwa husika aidha anaumwa na kalazwa hospitali ama mfungwa huyo amefariki wakati sio hivyo bali yupo nje na mzima.wakati mwingine mfungwa wa aina hiyo huhama mji ili wanaofahamu kufungwa kwake wasishangae na kuhoji kulikoni mtu yule kuwa nje.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom