kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
POLISI jijini Dar es Salaam inawashikilia watu watatu akiwemo mmoja ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 60 jela, wanaodhaniwa kuwa ni majambazi waliopora silaha ya askari.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema watuhumiwa hao walikamatwa juzi saa 7 usiku wakiwa na silaha mbili pamoja na risasi 45.
Kova alisema majina ya watuhumiwa hao yamehifadhiwa kwa sababu za upelelezi na kuwa watuhumiwa hao wamekuwa wakijihusisha na matukio ya unyanganyi wa kutumia silaha akiwemo mfungwa mmoja.
Ninashangazwa sana na huyo mtuhumiwa mmoja ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 60, lakini bado yupo uraiani anafanya uhalifu, alisema Kova.
Kwa mujibu wa Kamanda Kova, mwaka 2003 mshitakiwa alihukumiwa kifungo cha miaka 60 jela katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Alisema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo pamoja na wenzake, kumefanyika ndani ya saa 29 ikiwa ni muda mfupi baada ya kuporwa kwa silaha saa 2.15 usiku wa Desemba 12, mwaka huu katika lindo la Benki ya Akiba Tawi la Mwananyamala ambapo askari namba G128
Konstebo Fikiri, aliporwa akiwa lindoni.
Alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunatokana na taarifa za kiintelijinsia, ufuatiliaji, umakini na mapambano makali kati ya polisi na watu hao waliokuwa kwenye gari namba 1200 BLV Toyota Mark II Grand.
Alisema gari hilo lilikamatwa baada ya kupinduka katika Barabara ya Mandela karibu na kiwanda cha ngano cha Azam wakati wakifukuzana na polisi huku wakirushiana risasi.
Kova alisema watuhumiwa hao walipora bunduki aina ya SMG yenye namba 00430 ikiwa na risasi 30 wakati askari huyo akiwa kazini pamoja na mlinzi kutoka katika Kampuni ya Ulinzi ya Ultimate, Job Emmanuel (28).
Aidha, alisema washitakiwa hao walikutwa na magari mawili yenye namba T200 BLV, Toyota Mark II Grand gari lenye namba T350 BHJ aina ya Toyota na simu nane za mkononi. Mali hizo zimetambuliwa na wamiliki wake.