Mgirik
JF-Expert Member
- Apr 27, 2013
- 13,286
- 13,460
Nakumbuka nilipokuwa darasa la 4 nilitokea kumpenda dada mmoja alikuwa anaitwa Rusi.
Nilihangaika sana namna ya kumpata lakini nilikuwa naogopa kutongoza kipindi hicho.
Ikabidi nimweleze kaka mmoja ambaye ni mkubwa kwangu kumbe naye domo zege akanishauri niende kwa mganga ili anipe dawa ya mapenzi.
Kipindi hicho hata hela sina sikuwa na uwezo wa kupata ikabidi nikaenda kweli kwa mganga. Yule mganga akaniambia dawa ipo lakini nimpe shilingi elfu 2.
Nikaumiza kichwa namna ya kuipata nikaona ngoja nimdanganye baba kuwa nmepoteza kitabu cha mwalimu, nilipomweleza baba akanipa hiyo hela nikaenda kumpa yule mganga naye akanipa dawa nikarudi nyumbani.
Nikaanza kila asubuhi napaka ile dawa nikiwa naenda shule na namsubiri huyo Rusi tunaongozana huku nikisubiri yeye ndiyo aanze kuniambia ananipenda kwasababu nilijua ile dawa itamvuta na anipende.
Nikaona wiki inakatika Rusi hana mpango hata wa kunitamkia kuwa ananipenda nikazidi kujisiliba hayo mafuta ya dawa lakin kimya.
Nikaona acha nibadili dini nimfuate anakosali yeye huku nikizidi kupaka ile dawa lakini hakuna hata siku moja aliyoweza hata kunichekea.
Nikaishiwa nguvu baada ya kuona dawa inaisha bila hata kuona tabasamu la Rusi pamoja na jitihada zote.
Tangu siku hyo simwamini mganga yoyote nyamaafu