Jamani Wachagga mbona mnatutesa hivi hapa Ubungo Terminal?

Kwenda moshi ni lazima mkuu kuwa na subira kidogo,ila abiria watapungua kwani ATCL,dast jet zitawapunguzia abiria na magari binafsi nayo yameibgezeka sana mkuu.Aidha muda wa kwenda moshi ni kuanzia tarehe 15 hivi so kuwa mpole.
Kuna mtu kasema tumeokoka na hatunywi tena mbege na kisusio duuuuu hata iwe vipi asili ni asili tuu hahahaaaaa
 
Wachaga kwenda Kilimanjaro kuko pale pale iwe mvua inanyesha au liwe jua linawaka.

Kama pesa sema wewe ndiyo mifuko iko na shida wachaga pesa sio shida kwako.

Tarehe 15 Dec na kuendelea tiketi zitakuwa za shida Ubungo.
 
naona mtoa mada anajitahidi kweli kweli kuchochea na kueneza chuki zake kwa wachaga,gentmacy nataka nikuambie tu swala la wachaga kwenda makwao ni la kiroho na huwezi kulipinga, na hicho unachodhamiria ww na chama chako hakitakua,...wachaga watabaki kua mstari wa mbele tu katika taifa hili,...subiri tarehe 18-24 uone ubungo itakavyojaa
 
Kwani kuna Watu hapa ' duniani ' na pengine hata ' mbinguni ' wanaowazidi ' Wachagga ' kwa kupenda kusafiri kurudi kwao ' kuhesabiwa ' na kupeleka taarifa ya ' faida ' au ' hasara ' kwa kukaa kwao mwaka mzima humu mijini?
Wapo waChina.

'... world’s largest human migration, “Chunyun”, is happening in China.'
 
Kwa masikitiko makubwa sana sisi Wasafirishaji wa hapa Ubungo Terminal tunapenda kutoa ' lawama ' zetu kubwa na za dhati kabisa kwa hawa Wachagga hasa kwa kitendo chao cha ' Kikatili ' kabisa cha kuamua rasmi kuwa msimu huu wa Siku Kuu za mwisho wa mwaka hawatosafiri tena kama kawaida yao kwenda Kwao Mkoani Kilimanjaro ( Moshi ) kuhesabiwa kama ilivyozoeleka kwa miaka takribani 50 iliyopita.

Wengine tulishachukua hadi ' mikopo ' na kununua ' Mabasi ' ili tuwasafirisheni kwani tunajua kuwa mwezi huu huwa hambaki Dar na nyote hurudi kwenu Hedaru, Same, Sanya Juu, Kiboroloni, Siha, Hai, Rombo, Marangu, Mweka, Mwanga, Usangi na kote kote huku wengine ' tulijiongeza ' na hadi kununua ' Bajaji ' na ' Pikipiki ' ili tuweze pia kuwasafirisheni wale ambao mtakuwa mmechelewa kwenda ' kuhesabiwa ' lakini hali sasa imebadilika na inaonekana ' tutaumbuka ' sana na kuingia ' hasara ' kubwa.

Kwa niaba ya Wafanyabiashara ya ' usafirishaji ' tuliopo sasa hivi hapa Ubungo Terminal naomba kuwaulizeni ' Wachagga ' wote popote pale mlipo kuanzia humu humu JF Je ni kitu gani ' kimewakumba ' hadi sasa mnaonekana mmekuwa ' wagumu ' kusafiri kwenda kwenu Mkoani Kilimanjaro ( Moshi ) kama ilivyozoeleka na ilivyo kawaida yenu? Tatizo ni nini?

Tafadhalini Wachagga naomba mnijibu haraka na sasa hivi ili nami niweze kuwajibu ' Wasafirishaji ' wenzangu sasa hivi hapa Ubungo Terminal kwani kuna wengine sasa hivi wameenda hadi kuwekeza kutaka kununua yale ' matoroli ' aina ya ' Maguta ' ili tu na wao waje kuwasafirisheni kwenda kwenu kwa kuwasukumeni kutoka Dar hadi Kilimanjaro hivyo majibu yenu yatatusaidia wengi ambao ' tulijiongeza ' katika kuwekeza katika kuwasafirisheni mwezi huu wa December.

Natanguliza ' shukurani ' zangu kwenu Wachagga wote!
Tuliza boll subiri vipomo tarehe za majeruhi ni kuanzia tarehe 18 kuendelea nakuhakikishia safari hii mpaka mwendo kasi zitapiga masafa ya rombo tarakea bishaa
 
Subiri mpaka tarehe 15 nna mpango wa kupita dar kutokea kigoma na hatimae dar to rombo useri
 
Mkuu mm Nina familia ya watu 6 na wote tutasafiri kutoka dar mpaka A town kwa ajili ya sensa
 
Tumechoka mabasi...now dayz we drive.ukirudi unabeba mikungu ya kutosha ya kiwata mixer macharare
 
Back
Top Bottom