Jamani umeme wa Tanesco!!!!

Jamani umeme wa Tanesco!!!!

Polen na kazi,
Niende kwenye mada moja kwa moja.
Naomba kujua umeme ukishazalishwa ikitokea siku hiyo watumiaji ni wachache Mfano wakati wa usiku wa manane, Je ule umeme unaozid huenda wapi?
Je kuna sehem ya kuhifadhia ili utumike siku inayofuata? karibuni!!
Ndugu mpendwa mteja wetu umeme uliozalishwa tayari kwa matumizi hauwexi kihifadhiwa. Na hata hivyo kwa Nchi yetu tunajitosheleza kwa kiasi tunachozalisha na ziada kubaki
 
Ndugu mpendwa mteja wetu umeme uliozalishwa tayari kwa matumizi hauwexi kihifadhiwa. Na hata hivyo kwa Nchi yetu tunajitosheleza kwa kiasi tunachozalisha na ziada kubaki
Yani wewe umejibu kisiasa kweli sasa nani kasema umeme unatosha au hautoshi....
 
Matumizi yanapokua makubwa vifua umeme vingi zaidi huruhusiwa kuzalisha na kusambaza umeme...

Matumizi yanapopungua vifua umeme vichache huruhusiwa kulingana na demand...


Cc: mahondaw
 
Kwakweli umeme wao ni shida😊😊 kuja kukuekea mtu anahitaji umuabudu! Ukisha ingia mara uwe mwingi uunguze vitu!! ukihitaji kuondoa service charge hapo usiseme utazungushwa na mwishowe hawaiondoi!! Inakeraaaaa🙂🙂 Tanescooo toeni ajira kwa watu wenye weredi, uzarendo na utu!! Tanesco kama kampuni sio mbaya ila asilimia kubwa wafanyakazi wao wanaitendea vibaya! Wananikera km Nini? Rushwa imejaa kule taabu tupu yaani natamani kama kungelikuwa na kampuni nyingine ya umeme lakini pia wakafanya utafiti wa kubaini tabia zao kwa kuwawekea mitego itakayowanasa na wakishadhibitika watolewe kwenye vitengo hivyo na kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria. Lakini pia Tanesco iweke dawati huru la malalamiko ambalo litakuwa Kila eneo Tz. Na dawati huru waweza kufungua website yao au watoe email ambayo itakuwa rahisi kwa kero hiyo kufika kwa muhusika. Malalamiko yote yawe na uthibitisho km video/ audio recording, au nyaraka Fulani. Katika kushughulikia matatizo hayo, pawe huru na sio lazima atakayeandika aweke jina lake halisi ila eneo atokako tu. Itasaidia Tanesco kuwa yenye huduma nzuri.
Polen na kazi,
Niende kwenye mada moja kwa moja.
Naomba kujua umeme ukishazalishwa ikitokea siku hiyo watumiaji ni wachache Mfano wakati wa usiku wa manane, Je ule umeme unaozid huenda wapi?
Je kuna sehem ya kuhifadhia ili utumike siku inayofuata? karibuni!!
 
Generator za kuzalisha umeme zimefungwa vifaa vinavyoitwa Governor na AVR.
Vifaa hivi vinafanya kazi ya kucontrol uzalishaji wa umeme na pia speed(mwendo) wa generator kwa upande wa governor. AVR huangalia kiasi cha umeme kinachoitajika na kumjulisha governor aruhusu mafuta,maji,gas au steam viingie kwenye prime mover(water/steam/gas turbines, engines) ili kuzungusha alternator inayofua umeme.
Ikiwa mahitaji ya umeme ni madogo(yaani matumizi ni kidogo) basi AVR hupeleka taarifa kwa Governor kisha anaruhusu maji/gas/mafuta/steam kuingia kidogo kwenye prime mover kwa ajili ya kuzalisha umeme.
Endapo mahitaji ya umeme ni makubwa basi AVR hutuma taarifa kwa Governor kwa ajili ya kuongeza kiasi cha maji/gas/mafuta kuingia kwenye prime mover kwa ajili ya kuzalisha umeme zaidi.

Katika gari tunaweza kusema AVR ni binadamu na Governor ni accelerator(sehemu inayokanyagwa kuongeza mafuta) Au mguu.Speed ya gari tunaweza kuichukulia kama umeme unaozalishwa kwenye generator.
Mfano gari ikiwa na speed 180 sio lazima ifike hio speed 180. Unaweza kuendesha speed ya 50,60,100 au 140.
Unapotaka speed 100 akili yako inakutuma uongeze mafuta kwa kukanyaga pedal zaidi. Ukitaka kwenda 140 inakulazimu uongeze kukanyaga mafuta zaidi. Endapo huitaji speed 140 unataka speed 40 inakulazimu upunguze mafuta kwa kulegeza mguu kidogo.
Nimejaribu kuandika kwa ufupi maana ni somo refu sana
Mkuu ungelikuwa ni mwalimu ama kama ni mwalimu, basi una uwezo mkubwa sana wa kufundisha na kufaulisha. Unadadavua vizuri hata mamuma 'anapata'!
 
Ndugu mpendwa mteja wetu umeme uliozalishwa tayari kwa matumizi hauwexi kihifadhiwa. Na hata hivyo kwa Nchi yetu tunajitosheleza kwa kiasi tunachozalisha na ziada kubaki
Hiyo ziada inayobaki mbona sehemu tu nyingi DSM umeme hakuna? Kwanini msisambaze kwa kupitia REA? Ukienda tu MSAKUZI,MADALE kuna sehemu hakuna umeme haujafika halfu unakuja kujisia kwamba umeme upo wa kutosha hadi unabaki.
 
Kwakweli umeme wao ni shida[emoji4][emoji4] kuja kukuekea mtu anahitaji umuabudu! Ukisha ingia mara uwe mwingi uunguze vitu!! ukihitaji kuondoa service charge hapo usiseme utazungushwa na mwishowe hawaiondoi!! Inakeraaaaa[emoji846][emoji846] Tanescooo toeni ajira kwa watu wenye weredi, uzarendo na utu!! Tanesco kama kampuni sio mbaya ila asilimia kubwa wafanyakazi wao wanaitendea vibaya! Wananikera km Nini? Rushwa imejaa kule taabu tupu yaani natamani kama kungelikuwa na kampuni nyingine ya umeme lakini pia wakafanya utafiti wa kubaini tabia zao kwa kuwawekea mitego itakayowanasa na wakishadhibitika watolewe kwenye vitengo hivyo na kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria. Lakini pia Tanesco iweke dawati huru la malalamiko ambalo litakuwa Kila eneo Tz. Na dawati huru waweza kufungua website yao au watoe email ambayo itakuwa rahisi kwa kero hiyo kufika kwa muhusika. Malalamiko yote yawe na uthibitisho km video/ audio recording, au nyaraka Fulani. Katika kushughulikia matatizo hayo, pawe huru na sio lazima atakayeandika aweke jina lake halisi ila eneo atokako tu. Itasaidia Tanesco kuwa yenye huduma nzuri.
Shirika lilishafuta service charge toka Mwaka 2014 hivyo wateja wote wa majumbani hawakato service charge
 
Si kweli, mbona bado watu tunalipia?? Au labda si kwa wote.
Hakuna service charge na hakuna anayekatwa kwa kuwa mfumo umewekwa imara.Tafadhali angalia stakabadhi unayopata makato yote yamewekwa
 
Hakuna service charge na hakuna anayekatwa kwa kuwa mfumo umewekwa imara.Tafadhali angalia stakabadhi unayopata makato yote yamewekwa
Mmmh! Naomba msaada hapa Sasa! Umeme wa 10,000 ni units ngap?
 
Back
Top Bottom