Jamani umeme wa Tanesco!!!!

Jamani umeme wa Tanesco!!!!

bush crazy

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
773
Reaction score
1,087
Polen na kazi,
Niende kwenye mada moja kwa moja.
Naomba kujua umeme ukishazalishwa ikitokea siku hiyo watumiaji ni wachache Mfano wakati wa usiku wa manane, Je ule umeme unaozid huenda wapi?
Je kuna sehem ya kuhifadhia ili utumike siku inayofuata? karibuni!!
 
Huwa wanapunguza load... Kuna baadhi ya generators zinapumzishwa kulingana na matumizi... Peak hours zinawashwa tena. Au kwenye hydro huwa wanapunguza load ya kuingiza kwenye grid...so wanasave pia matumizi mengi ya maji yanayokwenda kwenye turbines.
 
Generator za kuzalisha umeme zimefungwa vifaa vinavyoitwa Governor na AVR.
Vifaa hivi vinafanya kazi ya kucontrol uzalishaji wa umeme na pia speed(mwendo) wa generator kwa upande wa governor. AVR huangalia kiasi cha umeme kinachoitajika na kumjulisha governor aruhusu mafuta,maji,gas au steam viingie kwenye prime mover(water/steam/gas turbines, engines) ili kuzungusha alternator inayofua umeme.
Ikiwa mahitaji ya umeme ni madogo(yaani matumizi ni kidogo) basi AVR hupeleka taarifa kwa Governor kisha anaruhusu maji/gas/mafuta/steam kuingia kidogo kwenye prime mover kwa ajili ya kuzalisha umeme.
Endapo mahitaji ya umeme ni makubwa basi AVR hutuma taarifa kwa Governor kwa ajili ya kuongeza kiasi cha maji/gas/mafuta kuingia kwenye prime mover kwa ajili ya kuzalisha umeme zaidi.

Katika gari tunaweza kusema AVR ni binadamu na Governor ni accelerator(sehemu inayokanyagwa kuongeza mafuta) Au mguu.Speed ya gari tunaweza kuichukulia kama umeme unaozalishwa kwenye generator.
Mfano gari ikiwa na speed 180 sio lazima ifike hio speed 180. Unaweza kuendesha speed ya 50,60,100 au 140.
Unapotaka speed 100 akili yako inakutuma uongeze mafuta kwa kukanyaga pedal zaidi. Ukitaka kwenda 140 inakulazimu uongeze kukanyaga mafuta zaidi. Endapo huitaji speed 140 unataka speed 40 inakulazimu upunguze mafuta kwa kulegeza mguu kidogo.
Nimejaribu kuandika kwa ufupi maana ni somo refu sana
 
Generator za kuzalisha umeme zimefungwa vifaa vinavyoitwa Governor na AVR.
Vifaa hivi vinafanya kazi ya kucontrol uzalishaji wa umeme na pia speed(mwendo) wa generator kwa upande wa governor. AVR huangalia kiasi cha umeme kinachoitajika na kumjulisha governor aruhusu mafuta,maji,gas au steam viingie kwenye prime mover(water/steam/gas turbines, engines) ili kuzungusha alternator inayofua umeme.
Ikiwa mahitaji ya umeme ni madogo(yaani matumizi ni kidogo) basi AVR hupeleka taarifa kwa Governor kisha anaruhusu maji/gas/mafuta/steam kuingia kidogo kwenye prime mover kwa ajili ya kuzalisha umeme.
Endapo mahitaji ya umeme ni makubwa basi AVR hutuma taarifa kwa Governor kwa ajili ya kuongeza kiasi cha maji/gas/mafuta kuingia kwenye prime mover kwa ajili ya kuzalisha umeme zaidi.
Katika gari tunaweza kusema AVR ni binadamu na Governor ni accelerator(sehemu inayokanyagwa kuongeza mafuta) Au mguu.Speed ya gari tunaweza Mkuu ahsante sana!
 
Huwa wanapunguza load... Kuna baadhi ya generators zinapumzishwa kulingana na matumizi... Peak hours zinawashwa tena. Au kwenye hydro huwa wanapunguza load ya kuingiza kwenye grid...so wanasave pia matumizi mengi ya maji yanayokwenda kwenye turbines.
mkuu nashukuru kwa mchango najua weng tumejifunza!
 
Sawa Mkuu.
Kwa kifupi matumizi yanapopungua mtu unasave kile chanzo cha kuuzalisha huo umeme mfano mafuta, gas au maji.
Kama kawaida huwa unazalisha 3MW kwa kutumia lita 10,000 za mafuta na ikatokea siku hiyo mahitaji ni 2MW basi huenda ukatumia lita 7000 za mafuta. So hizo lita 3000 unasave kwa matumizi ya kuzalisha umeme kesho yake.
 
We mkuu nimekukubali kwa maelezo mazur hata mtuawe kilaza kama mimi lazma aelewe! kunywa soda moja bure!
 
Kifupi ni kuwa kwenye vituo vya kuzalisha umeme kwa maji huwa zina jicontrol kwa AVR. Lakini vituo vya gas na steam ni kupunguza idadi ya mashine ili kuwa na frequency ya 50hz.
 
AVR ni nini? hivi hizi cables zao zinafanya tx&rx data?
 
Back
Top Bottom