Jamani tuwasaidie wanandoa hawa

Jamani tuwasaidie wanandoa hawa

twijuke

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Posts
547
Reaction score
252
Poleni na majukumu waungwana, kuna jambo linamtatiza mwenzetu nimeona ni busara nililete kwenu kwakuwa hapa ni uwanja mpana pasipo shaka atapata ufumbuzi na mwenzi wake. Hii ni familia ya wanandoa, jamaa anasema kwa mapenzi aliyonayo kwamke wake anaamini kama binadam naye anachoka kwa majukumu ya nyumbani, mwenzetu huyu anasema amejijengea utamaduni wa kufanya shuguli za ndani, ikiwemo kufua,kupika kufagia ndani na nje. Anasema anaona fahari kama mwanume kushiriki na mwenzi wake katika utekelezaji wa majukumu ya familia hususani kazi za ndani.

Anasemma babake mzazi ambaye ni marehemu sasa ndo aliye wajenga hasa kwa utekelezaji shuguli za ndani, anasema babake alikuwa hodari sana wa kupika hasa vitafunwa,na ansema katika familia yao hakukuwa na kazi maalum kwa watoto wa kike wala wa kiume. Ansema ameanza kupika na kufua nguo zake mwenyewe akiwa darasa la pili. Hivyo hata ndugu zake wanapomtembelea hawashangai wakikuta anapika, au kufanya shuguli za ndani. Anasema mfumo wa maisha anaoishi na mke wake umependwa sana na kaka wa mke wake ambaye ilifika mahali alimwambia natamani kuishi kama wewe shemeji uishivyo na dadangu.

Sasa mambo yako hivi, majuzi mke wa huyu bwana mpenda majukumu ya nadani, alifanya safari mkoani kumtembelea kakake alipohamishiwa kikazi, baada ya kurudi akasimulia jinsi kakake mambo yanavyomwendea vizuri, bwana huyu akisimulia anasema baada ya siku moja alirudi nyumbani akakuta mke wake anaongea na simu, bwana huyu anasema baada ya kubaini kilicho kuwa kikizungumzwa ilibidi atulie mahali ili kupata uhondo wa kinachozungumzwa.

Anasema simu ile mke wake alikuwa akimsimlia mamake aliyoyakuta kwa kaka yake, anasema mama mwenzagu kaka ameshikwa hajiwezi yuko mateka, anasema huwezi amini siku naingia kwa kaka chakula cha usiku kaka ndo aliandaa chakula cha usiku mimi nikiwa na wifi ukumbini, anasema nilipochoka ni pale kaka alipo fua nepi za mtoto huku anachekacheka, anasema mama fanya haraka tumwokoe kaka anaangamia, anasema kwajinsi nilivyo chukia niliondoka bila kuaga wakiwa kazini, nikamwabia kaka mimi naondoka nimepigiwa simu mtoto nyumbani anaumwa, na wifi sijamwambia chochote.

Sasa hapa huyu bwana anasema baada ya kubaini hayo amestisha utendaji wa majukumu ya ndani aliokuwa akifanya kwahiari yake, jambo ambalo limezusha mtafaruku mkubwa ndani ya nyumba kwakuwa mke wake aliisha jenga mazoea. Anasema yeye hajashikwa anafanya hayo kwa utashi na si kushikwa, lakini kama mke wake anasema kakake ameshikwa basi ameamua kusitisha kila kitu na hataki tena kusikia kitu kinaitwa shuguli za ndani, kwani mke wake amemwona kama mtu asiye na shukrani

Je ndugu mdau tunawashauri nini hawa wanandoa? Huyu mama mme wake amemfanyi akaona ni sahihi lakini kakake kumfanyia wifi yake anaona kashikwa.
 
Mm naona ni mapenzi ya mke na mume ktk ndoa.watakavyoamua kuishi wenyewe.pia 'mkuki kwa ngurue kwa binadam mchungu!huyo mwanamke kwake ni sahihi lakini kwa kaka yake kaona ameshikwa! Kama ni haki na yeye aache kumtumikisha mwenzake kwani yeye hakuzaliwa?
 
Ni vizuri kama anamsaidia mkewe majukumu ya nyumbani lakini nashauri kukiwa na ugeni kama wa watu wengine/ndugu huyo bwana apunguze kutoa misaada kwasababu kwa fikra zetu finyu za kiafrika mwanaume akisaidia kazi za ndani anakuwa bushoke au mume -----!atakuwa hamtendei haki mkewe akigoma kumsaidia hata wakiwa wao wawili tu kwani ndoa ni yao na waishi kwa sheria zao si kwa kufurahisha watu!
 
Kumsaidia mwenza si kosa,,,ni jambo jema sana,ingawa hizi kaz tumeshajengewa ni za wanawake,lakini isiwe too much,kama hivo jamaa kasitisha wife kanuna,,,kuna saa na wakat wa kumsaidia mwenza,na kuna kazi za kumsaidia ambazo kwa utamadun wetu wala hazileti saaana minong'ono,tatizo ni pale anayehudumiwa anapohisi ni haki yake ya kimsingi,,,,,,
 
Mwanaume hana kosa na yuko sahihi kabisa kwa uamuzi aliochukua,mwanamke anatakiwa kujua kwamba mume wake anafanya kwa upendo hivyohivyo na kaka yake anafanya kwa upendo,amuombe msamaha mumewe na aombe msamaha kwa wifi yake na kaka yake,kisha maisha yaendelee kama kawa.
 
Hahaaaa Nimecheka hapo aliposema 'fanya haraka tumuokoe'
 
amefanya uamuzi mzuri na ikitokea mkewe anataka kujua kwa nini hafanyi hizo kazi amweleze ukweli amuulize mkewe 'je ninaposaidia majukumu ya hapa nyumbani ninaangami yani anukuu yale maneno mkewe aliyokuwa anamweleza mama yake!
 
tena aache kabisa kufanya hivyo vishughuli coz
mke wake atakua anamtafsiri tofauti.tena wanawake wa
hivyo akiongea na shost zake utasikia nimemkamata hafurukuti
kumbe kaka wa watu amelelewa hivyo!!shame on her!!
 
tena aache kabisa kufanya hivyo vishughuli coz
mke wake atakua anamtafsiri tofauti.tena wanawake wa
hivyo akiongea na shost zake utasikia nimemkamata hafurukuti
kumbe kaka wa watu amelelewa hivyo!!shame on her!!

Itakuwa ndio zako hizo.
 
Yuko Sahihi huyu jamaa..huyu mwanamke anatakiwa ajue kuwa Raha anazozipata yeye anaposaidiwa na wenzake pia wanazihitaji....Kwa upande mwengine ni kwamba wanawake wanahitaji kusaidiwa ila lazima waache ujinga wa kufikiri ukisaidiwa tena ndo uanze mambo ya dharau....Mkileta Ujinga Tutagoma Tu!
 
Aje aolewe kwetu atafyatua hadi tofali...analeta mzaha.
 
Mbona sioni kama kuna msaada wowote unaohitajika hapo!!
 
Ukisaidia kazi isiwe regular, fanya kama una muda au pale msaada wako unapohitajika.

Kwa sababu ikizoeleka itaonekana hiyo ni kazi yako, tena usipoangalia unaweza kuja kuitwa na mama watoto huku akisema, "Baba fulani mbona hujaosha vyombo ...?"

Hapo maana yake ni kwamba huyo dada anajiona amemshika jamaa, na anamwona -----! Of course hata mimi ningemwona kama mke wake anavyomwona, hasa pale anapofanya kila siku kila mara!

Aache kabisa hizo mambo, awe mwanaume sasa.
 
Wanawake wengine huwa hawana shukrani na wengine kwa case kama hiyo ya kusaidiwa shughuli za ndani huwa wanatangaza sana kwa wenzao,ooh mi nimeshamshika ----- langu....
 
Back
Top Bottom