Jamani tutumie wataalam tukijenga nyumba!

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,886
13,184
View attachment 61370
Wakuu katika pita pita zangu mitaani nikakuta hiki kituko mitaa ya Mbezi Beach huko.
Ni dhahiri jamaa katika "kuokoa" matumizi hakutumia mtaalam kumchorea na hata kujenga, na paa likatoka ndivyo sivyo.

Nina uhakika kuwa dari hilo linavuja na itabidi jamaa alibomoe ili likae kimpangilio wa nyumba yenye hadhi.

Wakuu tusikwepe gharama za wahandisi na wabunifu tukifikiri fundi anatosha, kwa kifupi huyu jamaa pamoja na idea nzuri kala hasara.
 
Unahakika umetizama vizuri kweli????????

View attachment 61370
Wakuu katika pita pita zangu mitaani nikakuta hiki kituko mitaa ya Mbezi Beach huko.
Ni dhahiri jamaa katika "kuokoa" matumizi hakutumia mtaalam kumchorea na hata kujenga, na paa likatoka ndivyo sivyo.

Nina uhakika kuwa dari hilo linavuja na itabidi jamaa alibomoe ili likae kimpangilio wa nyumba yenye hadhi.Z

Wakuu tusikwepe gharama za wahandisi na wabunifu tukifikiri fundi anatosha, kwa kifupi huyu jamaa pamoja na idea nzuri kala hasara.
Mkuu tazama vizuri picha hii na hii picha si photoshop!
Kama unauona huo uwazi basi utelewa kuwa hapo ndio mwisho wa ufundi,hakuna njia rahisi kuziba uwazi huo.

Vile vile tazama paa upande wa kushoto,hapo usanifu umegoma, paa la kushoto ni tofauti na muundo wa paa la kulia.
Halafu hilo paa la kutoka juu kabisa mpaka chini,kulia mwa hilo paa ni lazima kutakuwa na uwazi/ufa unaovujisha maji wakati wa mvua.Natumaini unakaona kale kalasta kwenye coping ya mzunguko wa dari la juu, hapo ni lazima njia ya maji.

Ni hayo machache tu lakini kuna mengi tu.
Waweza kuona mwenye nyumba has an eye for good detail lakini hakutumia mtaalam kukamilisha ndoto hiyo.
 
Mwenyewe alikwambia imekamilika?

Hapo unaposema hapazibiki huo ni mwisho wa akili yako lkn nafikiri hapo panafaa kuweka vent ya kupumulia kupunguza joto ndani.

Kuhusu kuvuja sitakubishia, manake kamera yako yaweze kuwa na uwezo wa kubaini hilo
 
Ndugu yangu kama hiyo ni nyumba yako kubali tu upate ushauri na si kumkomaa kwa kuweka uchafu huo kwenye paa.
Hicho kipaa juu kushoto umeamu kufuga kuku darini?
Na hilo liuwazi kati ya floor ya kwanza na paa la chini itabidi umpate fundi kutoka ulaya kuliziba!
 
Mwenyewe alikwambia imekamilika?

Hapo unaposema hapazibiki huo ni mwisho wa akili yako lkn nafikiri hapo panafaa kuweka vent ya kupumulia kupunguza joto ndani.

Kuhusu kuvuja sitakubishia, manake kamera yako yaweze kuwa na uwezo wa kubaini hilo
Kosa kubwa lililofanyika hapo ni kuongeza chumba cha chini ambacho kinaelekea kimelazimishwa kuongezwa wakati wa ujenzi, plani yote kwishney!
Halafu mkuu wewe elewa tu kuwa JF kuna hadi maprofesa wa ujenzi humu, hata hivyo ushauri ni wa bure si lazima ukubaliane nao, pesa ni yako ati!
 
Ndio maana ukawa mwandishi wa habari na si mtaalamu wa ujenzi,hapo hakuna kosa lolote kama unavyolazimisha,hayo unayojaribu kuyaelezea ni mfumo wa kuingiza hewa ndani ya paa ili kupunguza joto ndani ya nyumba na kuna vifaa vitakavyopachikwa hapo wakati wa finishing.Hapa ninashuhudia uwezo mkubwa wa mchora ramani katika suala la roofing.
 
Watu waliozea mapaa ya mgongo wa punda utawajua tu..nenda tegeta masite ukaone paa za nyumba wewe,hiyo isikutishe sana
 
Aiseeeeee baba yangu ilo paa limetengenezwa kama nyumba za huku kwetu rombo kwajili ya kuweka au kuifadhi ndizi ya pombe mbege huyu hatakuwa mchaga mwenzangu wa tarakea rombo
 
ni kali kyeika maru awari,mnyengedhe
 
Mbona mi naona ipo safi tu. maji yanazuilika tu hapo. Inahitajika akili zaidi. Kama maji yatakua yanaingia tutafute wataalam tufanye mambo ila mpunga ujue utakutoka.
 
View attachment 61370
Wakuu katika pita pita zangu mitaani nikakuta hiki kituko mitaa ya Mbezi Beach huko.
Ni dhahiri jamaa katika "kuokoa" matumizi hakutumia mtaalam kumchorea na hata kujenga, na paa likatoka ndivyo sivyo.

Nina uhakika kuwa dari hilo linavuja na itabidi jamaa alibomoe ili likae kimpangilio wa nyumba yenye hadhi.

Wakuu tusikwepe gharama za wahandisi na wabunifu tukifikiri fundi anatosha, kwa kifupi huyu jamaa pamoja na idea nzuri kala hasara.

hii inaweza kuwa ni ya yule mtoto wa Kigogo anayetajwa tajwa Sana
 
ila ingefanyiwa finnishing ya ukweli ni nzuri....
Na ingewekwa ukuta unaoendana na nyumba
nadhani pesa ilikata ghafla mwenye nyumba akaona mradi iishe ahamie
 
Hakuna kuvuja wala nini hapo, hiyo nyumba haijesha, na paa limetulia tuli. Na huko juu hakuna kuvuja.

Kilichonikera mimi ni hizo pipe za drainage kuwekwa uchi. Ilikuwa zijengewe ziwe kwenye "utilities duct" kwa ndani, zikishuka zinakwenda kwenye tanki dogo la "filtration" zikitoka hapo zinakwenda kwenye tanki kubwa la kuhifadhi maji. Hapo anaweza vuna maji asiwe na kujuwana tena na mabomba ya mchina.
 
Ndio maana ukawa mwandishi wa habari na si mtaalamu wa ujenzi,hapo hakuna kosa lolote kama unavyolazimisha,hayo unayojaribu kuyaelezea ni mfumo wa kuingiza hewa ndani ya paa ili kupunguza joto ndani ya nyumba na kuna vifaa vitakavyopachikwa hapo wakati wa finishing.Hapa ninashuhudia uwezo mkubwa wa mchora ramani katika suala la roofing.
Kuna mauwazi kama manne hivi kwenye picha sasa wewe unaongelea uwazi upi wa kuingiza hewa?
Mi naona uwazi wa hapo chini wa mtu kuingia ndani kabisa na akafanya vitu vyake, na hilo ndio naona kosa lililo dhahiri.

Na juu kushoto kama ndio aina ya usanifu unaoushabikia basi na uandishi wangu naona niko mbali sana kujua vitu vizuri.
 
mkuu masopa hebu rekebisha picha siioni kwenye simu, ninataka kuchangia hoja pls.
 
Mkuu tazama vizuri picha hii na hii picha si photoshop!
Kama unauona huo uwazi basi utelewa kuwa hapo ndio mwisho wa ufundi,hakuna njia rahisi kuziba uwazi huo.

Vile vile tazama paa upande wa kushoto,hapo usanifu umegoma, paa la kushoto ni tofauti na muundo wa paa la kulia.
Halafu hilo paa la kutoka juu kabisa mpaka chini,kulia mwa hilo paa ni lazima kutakuwa na uwazi/ufa unaovujisha maji wakati wa mvua.Natumaini unakaona kale kalasta kwenye coping ya mzunguko wa dari la juu, hapo ni lazima njia ya maji.

Ni hayo machache tu lakini kuna mengi tu.
Waweza kuona mwenye nyumba has an eye for good detail lakini hakutumia mtaalam kukamilisha ndoto hiyo.

Wivu tuu...sioni fault kuubwa kihivyo..kiasi cha kuja kuianzishia thread hapa JF!
 
Ha ha ha
Wivu sina ila roho inauma!
Hata hivyo wivu si kitu kibaya kama mtu ni mpenda maendeleo na kutengeneza vitu standard.
Ustaarabu ni kusahihishana, nikiona umevaa suti imeliwa na panya ni wajibu kukutonya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom