Jamani tumsaidieje huyu dada?

Jamani tumsaidieje huyu dada?

OMWITUMA

Senior Member
Joined
Aug 6, 2013
Posts
119
Reaction score
29
Wana JF, kuna dada anaomba msaada ili aweze kupata haki yake anayoona inataka kudhulumiwa.
Mdada huyu alikuwa anafanya kazi katika shirika moja linaitwa SEDA tawi la Kagera ila makao makuu yake ni ARUSHA, kafanya kazi miaka miwili lakini leo kaachishwa kazi kwa kosa la KUBEBA UJAUZITO kabla hajaolewa, kwa hiyo kavunja masharti na adhabu yake ni kufukuzwa kazi, shirika lenyewe linashughulika na mambo ya mikopo midogomidogo kwa wananchi, Je, kwa sheria ya kazi hii ni sahihi? kwahiyo kama alipata ujauzito wao walitaka autoe? anadai mkataba aliojaza haukuwa na kipengele hicho. Je bado kuna mashirika yanaweza kuwa na sera au sheria za namna hii kweli au ni unyanyasaji kwa wanawake wenyewe wanafanyiwa kwani inasemekana mabosi wakuu ni wanawake na hawajaolewa, sasa wamemtumia Email ya kukabidhi kila mali ya shirika lakini hawataki kumpa barua ya kuachishwa kazi wala pesa za kusafirisha mizigo hadi kwao kama sheria ya kazi inavyosema pale mwajiri anapoamua kusitisha mkataba wa mwajiriwa wake. Tumsaidieje kiushauri wadau na pia hii inaweza kuwa somo kwa waajiri wenye sheria kandamizi zinazokiuka haki za binadamu. Ahsante naomba kuwasilisha ila msaada wa kisheria ni muhimu sana, mhanga kwao ni Shinyanga.😛arty:
 
whaaatt...!? Ngoja nikapekue makabrasha yangu ntarudi hapa
 
anahitaji msaada kwa kweli... ngojawaje wataalamu wa haya mambo...
 
Aende Commission of Mediation and Arbitration. Pia aangalia ni chama gani cha wafanyakazi kinawatetea hao waliopo SEDA, kama hayo ni kweli basi kesi hamna, dada kishashinda hata kabla haijaanza kusikilizwa.
 
Kwa maelezo yako kweli anahitaji msaada,maana kashafanya kazi miaka miwili.mimi nina ushahidi wa wadada wawili,mmoja aliajiriwa akiwa mjamzito mimba ilikuwa changa,docta akamwandikia hana,so alikaa kazini,na mwingine aliandikiwa pregnant positive so ilibidi arudi home mpaka ajifungue cs tayar walishamwajiri.wote hao wawili walikuwa na haki cs walishawaajiri otherwise wangeangalia kwenye intervw wakigundua wana mimba wasiwachague.so kwa kesi ya huyo dada,ana haki,seda imlipe,otherwise iwe kwenye sheria zao ambayo dada hakuiona ktk mkataba maana wengi huwa ofa hawasomi
 
kwa maelezo yako kweli anahitaji msaada,maana kashafanya kazi miaka miwili.mimi nina ushahidi wa wadada wawili,mmoja aliajiriwa akiwa mjamzito mimba ilikuwa changa,docta akamwandikia hana,so alikaa kazini,na mwingine aliandikiwa pregnant positive so ilibidi arudi home mpaka ajifungue cs tayar walishamwajiri.wote hao wawili walikuwa na haki cs walishawaajiri otherwise wangeangalia kwenye intervw wakigundua wana mimba wasiwachague.so kwa kesi ya huyo dada,ana haki,seda imlipe,otherwise iwe kwenye sheria zao ambayo dada hakuiona ktk mkataba maana wengi huwa ofa hawasomi

nimejaribu kumwuliza kuhusu mkataba aliojaza una kipengele cha kukataza kubeba ujauzito anadai hakuna.
 
acha wenye taaluma yao waje kuchangia,ila hawajamtendea haki,

Ila hao SEDA sheria zao zipo wazi ukipata ujauzito bila ndoa kazi huna,pia ni taasisi ya lakidini kwa hiyo wana maadili na sheria zao za kazi
 
SEDA kwa sasa inaitwa Vision Fund Tanzania, Jamani ninavyofahamu sheria za SEDA ni za Kikiristo perce, na Interview zao ni za dini na ajira zao zipo wazi kuwa ukibeba mimba nje ya ndoa, ukifanya zinaa, nk kazi huna. wako strict haswa! ila cha msingi ukifukuzwa kazi kuna taratibu na watazifuata maana nao ni wazoefu
 
Back
Top Bottom