Jamani tuchangie elimu, afya tuachane na michango ya harusi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani tuchangie elimu, afya tuachane na michango ya harusi.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magezi, Dec 12, 2009.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ndugu zangu wanaJF naomba nichukue nafasi hii kuwakumbusha kwamba kwa sasa hatuna sababu ya kuchangia 50,000 tshs kwa harusi alafu tunalalamika hatuna pesa ya kulipia ada ya watoto wetu shule.

  Kama mnavyojua matokeo ya std 7 yanaonyesha watoto wengi mwaka huu wameshindwa kwa hiyo wote hao ambao wameshindwa wanahitaji kupelekwa private sec. schools hapo mwakani.

  Naomba ndugu zangu wanaJF ktk mitaa yenu muanze kuitisha vikao visivyo rasmi kutathmini ni watoto wangapi wako ktk mitaa yenu na ni jinsi gani mtawasaidia kwa kuchangisha pesa ktk serikali za mitaa na kuwa support wanafunzi watakao kosa nafasi ktk sec. za serikali (za kata) na zingine.

  Nashauri ktk kila familia itolewe tshs 20,000 na pesa hizo ktk kila mtaa na pesa hizo zihifadhiwe ktk mfuko wa maendeleo wa serikali ya mtaa ambapo account signatories wawe 3 ili kuondoa wasi wasi. Watoto watakao saidiwa hawatapewa pesa bali watalipiwa ada na kununuliwa mahitaji muhimu ya shule.

  Mimi siko TZ kwa sasa lakini nawaomba wanaJF wenzangu tufanya hima na pesa hizo zichangwe kwa kuanzia tarehe 20 desemba hadi 11 januari 2010 ili kuwawezesha watoto wawahi kujiunga shule.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Dec 12, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Nia yangu si kukupinga, lakini hilo wazo umelipataje baada ya kuondoka nchi hii tu, ilikuwaje wakati ukiwapo hapa usilianzishe?

  Na hizo time-limit ulizoziset, umeangalia sawa kwamba unaongea na audience gani?...watu wa maeneo yapi nchini?..na vipato vya kivipi?

  Husomi magazeti yanayosema.."Mama amkata mwanawe kiganja kwa kuiba shs 100/=?"
  Na huo uhamasishaji utapokelewaje ghafla hivyo ndani ya timeline uliyoiweka?..Labda ukiwa nje ya Tz unakuwa na mtazamo maridhawa zaidi anyway!

  Asante kwa wazo!
   
 3. Obhusegwe

  Obhusegwe JF-Expert Member

  #3
  Dec 12, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 232
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33

  kweli
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Dec 12, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mkuu ndo maana ya kutembea nimekuta hapa kuna huo utaratibu na wala husikii mtu analalamika kwani jamii ina mipango yake kwenye masuala ya elimu na afya na maji. Pia serikali hapa inamchango wake lakini ktk kile street wana vyama vyao kiraia kwa ajili ya maendeleo.

  Sasa nikaona niwashirikishe hii kitu na nadhani nikirudi ndo suala la kuanza nalo.
   
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  Dec 12, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kuhusu time limit hii wala siyo issue kwa sbabu nimeangalia ni lini shule zinafunguliwa. Unasema ni jamii gani ninayo iongelea.......naongelea hao hao wananchi wa kawaida kwa sbabu ndio wazazi wenyewe, sasa unafikiri ni nani atakayekuja kutusaidia kama siyo sisi wenyewe??
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  Dec 12, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  hizo pesa za harusi ni matokeo ya jasho letu, na kodi tunalipa na bado mawaziri na wadosi wachache wanaziiba pale hazina , sasa leo unadai tuchangie shule na hospitali.
  kwanza waambie HAZINA NA BOT watulindie kodi zetu pale gharani, kisha zikiwa salama sasa tutajua serikali inajiweza kwa kiasi gani na kiasi gani haijiwezi , sasa tutaambiana kuchangia deficit, otherwise post yako inakera na niunadiki labda utueleze wewe umechangia TSH ngapi katika maendeleo ya shule na hospitali.
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Dec 12, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Sijui kama umesoma mchango wangu vizuri. Mimi sisemi uchangie shule na hospitali, nachosema ni kuwa na development funds ktk mitaa yetu na jinsi pekee ya kuanzisha hizo development funds ni kuchangisha wanajamii ktk mitaa husika na hizo fedha zinaweza kuwasaidia watoto wetu ktk masuala ya elimu.
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Dec 12, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  [​IMG]
  Sawa Mkuu...tutafika tu...
  Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Africa!
   
 9. M

  Magezi JF-Expert Member

  #9
  Dec 12, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Naona kama sijaeleweka lakini jamani ktk kutembea huku ukikuta kitu kizuri siyo vibaya tukajaribu kufanya na nchini kwetu. Katika haka ka nchi nilipo nao ni masikini pia lakini baadhi ya maeneo wana development funds ktk maeneo yao na fedha wanachangia kila mwezi kwa kila familia.

  Unapofika wkakti wa kupeleka watoto shule hata kama watoto wale wamedhaminiwa na serikali lakini pesa ile iantumika kununua uniforms, viatu, vitabu, n.k. na kama kuna labda familia inachangia na haina mtoto anayesoma wanapewa pesa kwa ajili ya shida mbali mbali itakayo tokea.

  Kwa hiyo serikali inawajibu wake kwa raia wake lakini sisi kama jamii tuna wajibu pia wa kuanzisha miradi/mifuko ya maendeleo kwa ajili yetu na vizazi vijavyo.
   
 10. M

  Magezi JF-Expert Member

  #10
  Dec 12, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mkuu tutafika hii picha wala isikutishe kuna nchi hata huo udongo na miti ya kujenga hivyo hakuna wanajengea magunia/maboksi na familia inaishi mfano ni ktk jiji la NewDelhi India.
   
 11. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #11
  Dec 12, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  kwanza vikao visivyo rasmi huwa haviitishwi na serikali za mitaa, huku nyumbani TZ serikali za mitaa ni serikali kamili, vikao vyote ni rasmi labda ulitaka kumaanisha vikao vya dharula.
  Pili kuhusisha hawa watu waserikali za mitaa kututunzia vijisenti vyetu nakwambia hawawezi, kama serikali kuu yenye wasomi wakila aina wameruhusu mianya ambayo imefyonza pesa za kodi pale HAZINA na BOT NI KUDANGANYANA KWAMBA HAWA WAZEE /wengi wao wataweza kulinda pesa hizo.
  Madiwani kwa kushirikiana na watendaji kata na vijiji kila kukicha wanauza ardhi na kila kinachoonekana , sembuse wakutnzie pesa.
  mimi naamini wazo lako halitafanikiwa .
  KAMA serikali hii ya ccm ingeweza kudhibiti corruption na uchafu mwingine wote hakika elimu ya Msingi hadi sekondari ingetolewa bure kabisa.....ila fedha yote wamekomba kina Manji,RA,jeetu, NA MADUDU YAO YA KINA EPA,richmond,IPTL,dowans na Sasa Shirika la reli.
   
 12. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #12
  Dec 12, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180

  Haya bana...tuombe Mungu!
   
 13. M

  Magezi JF-Expert Member

  #13
  Dec 12, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nakushangaa sana unaposema "huku nyumbani vikao vyote ni rasmi na serikali za mitaa ni serkali kamili......". Hivi unafikiri ni lini nimeondoka hapo DAR? mbona juzi tu na utumbo wote wa serikali za mitaa naujua?? hizo serikali kamili za mitaa ni zipi?? mbona mwenyekiti wa seriali ya mtaa wangu pale ubungo msewe aliitisha kikao ambacho siyo rasmi na tulihudhuria??

  Kama huna hoja za maana kuhusu hii mada bora ukae kimya, sina hata miezi mitatu nimeondoka bongo leo unani chukulia kama vile siijui bongo??

  Hayo matatizo ya serikali ya CCM kila mtu anayajua tatizo ni wapiga kura kutokuwa na elimu ambayo mimi najaribu kuona ni jinsi gani we can solve this kwa kuhakikisha watoto wetu wengi wanakuwa na elimu.

  Kuhusu utunzaji wa pesa mimi nafikiri kawaida mnachagua watu wa kutunza siyo lazima viongozi hao. mbona saccos zianaanzishwa na viongozi wa serikali ya mtaa pengine hawahusiki?? kwa nii utaratibu huo usitumike??

  It seems you are resisting to understand my idea.
   
 14. M

  Magezi JF-Expert Member

  #14
  Dec 12, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Firstlady1 uko wapi hii mada inahitaji mchango wako
   
 15. S

  Shamu JF-Expert Member

  #15
  Dec 12, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unazungumzia distribution of wealth. Hatuishi kwenye Ujamaa no more. Kama unataka kutoa hiyo michango, toa tu bila ya kuwachangisha watu wengine.

  Hayo maneno unabidi uwaambie Wabunge wa CCM, Mawaziri wake, na Rais waache kutumia hela za Wananchi vibaya, na waanze kujenga shule, hospitali, na barabara.
   
 16. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #16
  Dec 12, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  thanks Mkurugenzi, hii picha umenikumbusha mbali kweli....
   
 17. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #17
  Dec 12, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hili ni wazo zuri sana japo nadhani inahitaji muda kwa jamii kulielewa kulikubali na kulifanyia utekelezaji,

  kwa miaka karibu 50 sasa tumeona jinsi kutegemea serikali kulivotuacha taabani, mi napendekeza kabla ya kulliweka kwenye serikali za mitaa wazo hili lingeanzia kwenye zile zile jumuia zinazochangia harusi yaani badala ya kukaa vikao vya kuchangia harusi, ndugu jamaa na marafiki wasio na uwezo wenye watoto waliokosa nafasi waitishe vikao vya kuchangia elimu, kadi zitolewe michango ikusanywe watoto wapelekwe shule

  hizo milioni 2,3,4,5 nk tunazokusanya kwa hizi harusi zisizoisha zinaweza kulipia ada ya watoto wangapi kwa mwaka?

  tulipokuwa tunatafuta leseni ya makazi serikali ya mtaa ilitutoza 5000 kuchangia elimu kwenye kata japo kodi tunalipa kama kawaida, na mpaka sasa hivi hitima ya hizo pesa haijulikani..
   
 18. m

  masssaiboi JF-Expert Member

  #18
  Dec 13, 2009
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 637
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 33
  Jamaa anataka kuanzisha deci yake nini????
   
Loading...