Jamani tuache huu upotoshaji

Jamani tuache huu upotoshaji

albuluushiy

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2013
Posts
1,404
Reaction score
687
Haya ni maneno ambayo watu wa mrengo fulani wanatumiana;

"Bwana Yesu asifiwe, Mtumishi wa bwana Yesu kumekucha wana wa Mungu. Mswada wa kutambuliwa kwa Mahakama ya Kadhi kisheria utapelekwa bungeni 1.4.2015 kama Mwanasheria mkuu wa Serikali, George Masaju alivyoahidi na kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria na Utawala wakikubaliana tumeumia.

Mateso kwa Wakristo yataanza kama wa Nigeria, Boko Haramu, Al-Shabab Somalia, n.k. Mwombe Mungu sana ashughulikie hiyo kamati ili wasikubaliane wapinge suala hilo.pia tumuombee ulinzi Mch Chr. Mtikila amefungua kesi kupinga Mahakama ya Kadhi Kanisa lishinde kesi hiyo iliyofunguliwa, Mahakama Kuu itaanza kusikilizwa tarehe 30/03/2015 tuombe Yesu awe ndie Hakimu wa jambo hili kila ifikapo saa 6 kamili usiku tuombe kwa pamoja sauti iwe moja kwa Mungu wetu funga lango hili la kuzimu lipo wazi Joka hili Mahakama ya Kadhi linajianda kuingia kupitia lango la Katiba Pendekezi. Tuma kwa Wakristo 15 ev Elias wa Biblia ni jibu Tz"


Sasa jamani haya mambo sio uchochezi? Natarajia majibu mazuri kutoka kwenu, sio hamaki!
 
Kama Kweli TCRA sio wadini kamateni hawa wachochezi upesi kabla hili taifa halijaangamia. Kuacha upuuzi kama huu kuendelea kusambaa ni kuhatarisha amani na usalama wa taifa. Hebu TCRA wachunguze kinachoendelea kwenye mitandao hasa kipindi hiki hadi uchaguzi Mkuu. Kama tcra watakuwa serious basi wachochezi wengi watatiwa hatiani.
 
huu ni upotoshaji wa hali ya juu na huko watsap na kwenye groups watu watumiana tu
 
Kama Kweli TCRA sio wadini kamateni hawa wachochezi upesi kabla hili taifa halijaangamia. Kuacha upuuzi kama huu kuendelea kusambaa ni kuhatarisha amani na usalama wa taifa. Hebu TCRA wachunguze kinachoendelea kwenye mitandao hasa kipindi hiki hadi uchaguzi Mkuu. Kama tcra watakuwa serious basi wachochezi wengi watatiwa hatiani.

hao watu hawawezi kuguswa aisee
 
Mimi na dini yangu tu.. mengine hayanihusu
 
Siasa zozote zisizo zingatia mipaka huwa ni upumbavu, hivyo basi hatuna budi kuwapotezea hao wasiofikir juu ya kile wanachokifanya
 
Ni kweli mkuu,uzi wako na maneno yako yote ni ya kichochezi...nakusihi acha uchochezi
 
Lazima iwepo 7bb mambo yetu sisi hayatengenezwi na binaadamu yapo tayari na yametulia na katu hatuwezi kukufateni nyinyi mnoamua sheria za Muumba kuzibadili na kuziweka za kwenu ambazo mlozitunga kwa maslahi yenu ya kidunia!
 
Kwanini lakini mnang'ang'ania iwepo kwenye sheria za nchi?Nyerere a likuwa na hekima sana akijua akili za watu ukiruhusu Mbona ile furaha tunayo enjoy sasa tutaanza kuitafutia UN.
Hapa hamna uchochezi ila mwenye macho haambiwi Tazama hata siku moja.Tunayonyaona kwa wenzetu tunapata experience ila tunajua sasa meli inataka kuendeshwa na mgiriki......
 
Waache watiane upumbavu watakavotiana lakini mahakama itaanzishwa tu, atakaeleta ujinga "atapigwa tu"
 
Watu hawana kazi wanatunga uongo daily....hivi aliyezima taa humu ndani nani
 
Back
Top Bottom