Jamani: They have pushed Health Workers too far: | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani: They have pushed Health Workers too far:

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by babykailama, Jun 27, 2012.

 1. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Jamani: They have pushed Health Workers too far: :embarassed2::embarassed2:


  Nilipoona Watumishi mbalimbali wa afya Muhimbili (sasa si Madaktari tu) wanasukuma ile Ambulance inayoweza kuwaka na kuendeshwa huku wakiimba kwa sauti za juu bila choir master wimbo ‘solidarity forever' na ndani yake yumo Kiongozi wa Chama cha Madaktari amelala hoi kwa kupigwa na watu wabaya sana katika nchi yetu iliyo huru na yenye utawala wa sheria, nimejikuta napangusa chozi la huruma na uchungu sana kama lile lililomdondoka Mwl. Nyerere alipokuwa akishuhudia mwili wa Waziri Mkuu Sokoine!

  Naahidi kuwa, chozi langu litaendelea kufuta utando na uchafu wowote ulio mbele ya macho yangu, hadi wabaya hao watakapowekwa katika mikono ya haki.


  Tena, niliposhuhudia kisago kikitembea kwa yule waliyemhisi kuwa Afisa wa Usalama, nikarejea taswira ya sinena inayovuta hisia wakati wote ya Sarafina wakati vijana wa ukombozi walipomchomoa yule Mwafrika mwenzao ‘Sabela', Agent wa Makaburu na wakammwagia mafuta kumchoma moto! Tafadhali sana chukua muda wako kuangalia tena kipande hiki cha Sarafina SARAFINA 1992 - YouTube na uweke msisitizo kuanzia katika dakika ya 0: 52:11 na pia 0:58:41 .

  Wakati yule wakala anateketea kwa moto, Sarafina alijisemea, "they have pushed us too far!!"  <span style="mso-ansi-language:EN-US" lang="EN-US">
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...