Jamani shemeji yangu huyu..... hadi jumapili tarehe 22/01/2017

General Galadudu

JF-Expert Member
Nov 7, 2015
1,868
2,200
Habarini za wakati kama huu wadau wenzangu wa uwanja Wetu huu pendwa, naomba niseme wazi kwamba uzi huu cjauweka hapa ili kukashifu imani ya mtu yeyote, kwa hiyo kwa atakaekwazika anisamehe tu maana hakuna namna.

Naomba ushauri juu ya huyu mke wa mdogo wangu, kipindi cha nyuma (akiwa tyr ni mke wa mdogo wangu) niliwahi kugundua tangu anatongozwa na hatimae kuopolewa na li njemba moja hivi ambalo sina uhakika sana na utimamu wa akili zake,niliiona mipango yote hadi siku ya kwenda kugegedana nilishuhudia...... lakini bahati mbaya kwa bibie ni kwamba wakati wanatoka akaniona na mi nikamuona tukawa tumeonana akastuka kiaina, wakageukiana kunong'onezana jambo nadhani alikuwa anamuonesha mimi ili kumtahadharisha, nilipoligundua hilo nikateleza pale nikahamia sehemu nyingine ambayo ilifanya niendelee kuwaona, walipogeuka hawakuniona wakachanganyikiwa zaidi....... nikaona wanaondoka harakaharaka.

Nililitafuta lile jamaa nikaunda nalo urafiki wa uongo na kweli hatimae likaingia mtegoni na bila ya kujua kuwa mwanamke liliyekuwa nae ni mke wa mtu lilijikuta linatapika mambo yoooote waliyofanya siku hiyo tena kwa kujigamba likawa linasema kwamba eti lilimgegeda PAPUCHI likapiga na 0713...... ndo maana nikasema sina imani na utimamu wa akili zake........ Hilo jambo niliumia nalo sana moyoni lakini nikaamua hilo niachane nalo, na kweli nikafanya ivo

Jumapili ya juzi tarehe 22/01/2017 jioni ilinikuta kwny hotel flani nachangamsha ubongo kdg, sasa kutokana na harakati zangu za KIJASUSI nikiwa sehemu kama hizo huwa napenda kukaa sehemu ya kujificha lakini huku nikihakikisha naangalia geti kuu ili nione wanaoingia na kutoka, macho yangu ya kipelelezi yakavutika zaidi nilipoona wanaingia mwanamke na mwanaume, na kilichonivutia sana ni kwa yule mwanaume jinsi alivokuwa amevaa, alijilazimisha kuvaa kama vijana wa kisasa lakini umbo la mwili wake halikukubaliana na mtindo wa mavazi alioutaka yeye..... nikajikuta navutika niendelee kuwafuatilia kwa macho hadi walipokwenda kukaa.

Staili waliyokaa ikanifanya niwaone wote kwa pamoja, kwa kweli hadi moyo wangu ukastuka paah..... alikuwa ni yule yule shemeji yangu mke wa mdogo wangu lakini safari hii alikuwa na mchungaji mmoja wa haya makanisa wanayoyaita ya kiroho......nilibaki nimeganda nawaangalia bila kujua la kufanya, nikajikuta naufanyia utalii kwa macho mwili wa yule mchungaji hatimae macho yakanasa kwny kidole chake.... ana pete ya ndoa imetulia pale, kumbe ana mke!!..... nikawa nawasikitikia waumini wake, mke wake na watoto wake pia, bia na nyama choma ziliteketea sana pale...... kumbe na mchungaji anapiga maji vzr tu.

Kutokana na pilika zangu..... kwa kawaida nikiwa maeneo kama hayo huwa napenda kufanya malipo ya hapo hapo kwa kila huduma ninayopatiwa, hiyo ni kutokana kwamba wakati mwingine huwa nalazimika kuondoka ghafla tena kwa uficho wa hali ya juu sana, na hata cku hiyo ilikuwa ni ivo ivo tu, nikamuona shemeji yangu anainuka kuelekea ndani eneo la mapokezi..... na mi nikainuka kwa usiri mkubwa nikaelekea huko huko lengo langu anione na kweli ikawa ivo, nilimkuta anaandikisha chumba...... aliponiona akastuka na mi nikatoa simu kujifanya naongea halafu nikampita pale pale nikatokea mlango wa nyuma nikaondoka zangu nikapotelea mtaani.

Sasa jamani ushauri wenu tu nauhitaji juu ya hili, maana najickia huruma sana juu ya mdogo wangu lakini pia nina hasira sana kwa shemeji yangu..... NIFANYEJE????
 
Huyo ni Mke wa mdogo wako au rafiki yako?
Maana angekuwa mdogo wako toka ni toke hata huku hili jambo lisingefika ungekuwa umesha mwambia utumbo wa mkewe ila kama unasubilia ushauri ya jf Ndy ufanye maamuzi subili mdogo wako akipata maradhi ndy utajua unochofanya ni utoto
 
Back
Top Bottom