Jamani nisaidieni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani nisaidieni

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Meritta, Jun 8, 2011.

 1. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hi wana jamvi, mi mwenzenu nina tatizo kidogo naombeni mchango wenu wa mawazo.
  Ni binti, mtoto wa marehem shangazi tumeishi naye toka mdogo tulipendana sana na hatukuwai kumbagua. ivi majuzi alipata kazi mkoani dodoma uko alianza mawasiliano na mwanaume na alianza kumpenda ila hajawai kumuona sababu uyo mwanaume yupo DAR. Kwa upendo tu alituomba mimi na mdogo wangu twende tukamfahamu uyo shemeji sababu tuko naye uku uku Dar na tumueleze anaonekaneje sababu yeye hamfahamu, tulipoonana na shem kwa bahat mbaya akavutiwa na mdogo wangu na wakaanza mahusiano kwa siri. Baada ya muda kidogo mtoto wa anti kapata likizo ya kuja dar kusalimia na lengo kubwa ni kumjua zaidi uyo mpenzi aliyempata kwenye simu.WAliponana uyo mkaka akagundua kuwa mdogo wangu ni mzuri kuliko mtoto wa anti hivyo ak.amwambia kuwa wawe marafiki tu sababu amempenda zaidi mdogo wangu kuliko yeye. Hapo mtoto wa anti alipata hasira na kuichukia familia nzima na mpaka natuma posti hii ameondoka nyumbani na anatuita sisi wote ni wasaliti.hapa nina hofu mama akijua tatizo lililimfanya aondoke nyumban pia mi bado namkumbuka na kumpenda sasa sijui nimwambiaje ili aweze kurudi nyumbani. wana jamvi nisaidieni nimwambiaje
   
 2. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Dunia kigeugeu, ndugu kigeugeu, dada kigeugeu....Mapenz kigeugeu!

  Mi ctak kuckia hz story za mapenz! Mpe pole...
   
 3. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  aache hasira zake. wewe tulia.... kama jamaa yupo serious na dogo waache waendelee na yao na huyo mtoto wa anti atapata mwingine. mambo ya mapenzi hayanaga usuluhishi na wala hakuna kuyawaziawazia.... wewe tulia. muda tu ndo utasuluhisha maana naye huyo mtoto wa anti atapata mwingine na kusahau yaliyopita.
   
 4. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Sidhani kama huyo mkaka hata anajua maana ya kupenda. Ningemshauri huyo mtoto wa anti yako atulie tu maana Mungu amemuepusha na balaa kubwa sana, huyo mwanaume sio mwaminifu na sidhani hata kama na huyo mdogo wako watadumu cos wazuri wanazaliwa kila siku.
   
 5. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  yaani hata kuongea na mimi hataki
   
 6. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mdogo wangu nimemwambia hivyo kuwa hawatadumu lkn yeye anadai wanapendana. uyo mtoto wa anti hataki kunisikiliza ila mi nitajaribu
   
 7. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Asante kwa ushauri. ila hofu ipo kwa mama maana hajajua kwa nini mtoto wa anti kaondoka nyumbani
   
 8. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  hebu niambie huyo mdogo wako ana umri gani?
  na huyo jamaa ana umri gani?
  Ntarudi baada ya kunijibu!......................
   
 9. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mdogo ana miaka 19 pia uyo mkaka sijui ili kitu cha 27 kwa nilivyo muona
   
 10. Ole Tetian

  Ole Tetian Member

  #10
  Jun 8, 2011
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Ndani ya moyo wako una hatia?namaanisha unahisi umechangia kwa vyovyote vile hayo kutokea?kama moyo wako uko u msafi na unaamini hujapelekea hayo kutokea basi Mpe muda huyo mtoto wa shangazi yako ataelewa kila kitu!Wasiwasi weka kwa mdogo wako na kama unaweza mshauri awe makini na wakaangalie afya zao yeye na huyo shemeji yako!wakikataa mshauri acheze salama!
   
 11. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Asante kwa ushauri. moyoni mwangu mi sina wasiwasi
   
 12. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Jaribu kumwambia ukweli kuwa wewe na familia yako have nothing to do with that,pia mwambie suala la wale kuwa wewe hausiki na kilichotokea,kama ni ujinga ni wa mwanaume kutokuwa mwaminifu,tena ashukuru huyo jamaa amejionesha yeye ni nani mapema,ayakubali matokeo,kama hataki kukusikiliza mwache muda ukipita atajirudi mwenyewe usimlazimishe akuelewe!
   
 13. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  asante ndugu yangu
   
 14. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Your welcome!
   
 15. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Dah, inaonekana hao ndugu zako wanajua kupenda! Mtoto wa shangazi kazimika kichizi hata kabla ya kumuona jamaa, na mdogo wako pamoja na kujua hivo kaingia kichwakichwa bila kujali ndugu yake atajisikiaje! Tamaa?! Huyo ndugu yako ataponywa na mda, kadiri siku zinavyopita atazoea na atamshukuru Mungu kwa kumuepusha na mtu mwenye tamaa na asiyejali.
   
 16. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #16
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  ila amenichunia hata mimi ivyo inaniuma
   
 17. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #17
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Huyo dada yako (shangazi sijui) na yeye inabidi awe sehemu ya lawama.. kwa maoni naona alifanya kosa kwa kuagiza nyinyi kwenda kumuangali jamaa kama 'analipa' au 'mpotezeaji'?

  Hiyo ni sawa sawa na kumchagulia mtu mke au mume..maana kama mngesema kwamba jamaa si lolote si chochote bado angeweza kuwapa lawama, na nyie kwa vile mnampenda ndugu yenu msingependa kumpitishia taarifa za kumkatisha tamaa..
  Angeweza hata kuomba picha kupitia email au hata posta (au mabasi).

  Hilo ni somo, siku nyingine atajifunza kuyaendesha mapenzi..Huwezi kumpa nyama akufikishie..Yaani ilimpasa iwe siri yake mpaka pale ambapo wangeonana..Namsikitikia..Ila atapona maumivu baada ya muda
   
Loading...