Jamani nimeyakoroga naomba ushauri

Jamani nimeyakoroga naomba ushauri

joseph2

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2015
Posts
661
Reaction score
1,370
Habari zenu wanajamii forums. Naomba ushauri kwenye hili. Nimekuwa kwenye ndowa miaka kumi na moja. Mimi nilichelewa kuowa sasa nina Miika 45 . Huyu mke wangu kusema kweli hakuwahi kunivitia kisura wala kimaumbile,. Ila kipindi naamuwa kuowa nilimuona ni mtu mpole asiye penda makuu.

Na kwavile hali yangu ya kiuchumi haikuwa nzuri sana ila nilikuwa na uwezo wa kawada wa kubadilisha mboga. Kwa hiyo kwa wakati ule nikafikiri kuwa huyu kwa vile anatoka kwenye familia ya masikini, na ni mpele basi huwenda hata maisha yakinipiga zaidi hata nisumbuwa, tutaishi katika hali yoyote.
Basi nikajiambia kuwa pamoja na kwamba hana mvuto wa sura ila tabia ya upole na ukimya vitafidia . yote.
Sasa baada ya kukaa naye kwa mda mrefu nimekuja kungunduwa vitu vilivyo nifanya ni ignore red flags na vigezo vingine navyo vilikuwa kuingiza. Mpaka leo bado anaigiza kuwa mpole. Shida ikifika wakati wa kujadili mambo serious huwa hawezi kuchagia mawazo yake anabaki tu kucheza upole na ukimya . Ila topic nyepesi kama ombea anakuwa mchagamfu sana na anachagia vizuri kabisa. Suala lingine.Intaendelea.
 
Pole sana mkuu yatakwisha..dhambi ya usalitj ni mbaya sana...Kuna mawili, umruke shemeji Yako kwamba hujamuambia hizo stories au ujishushe mtoe mkeo out, mwambie achukue anachokitaka, then nendeni hoteli nzuri sana mfurahie maisha hata siku 2 au 3 then umuahidi kwamba hiyo hali haitawahi kujirudia....
 
Tushukuru wanawake wengi kiuchumi hawapo vizuri.

Kama sheria zetu zingekuwa nzuri ulitakiwa utalakiwe, uondoke nyumbani umwachie watoto kisha unatoa matumizi kila mwezi bila kukosa.

Kama ulitaka kucheat wanawake kibao mitaani... Wanaume waliooa

FORBIDDEN ZONES
-ndugu wa mke
-rafiki wa mke
-Jirani
-beki tatu

Wanawake wanaongea saana.
 
Nimekuwa naishi na mdogo wa mke wangu. Yaani shemeji yangu amekuwa akiishi kwangu yeye na mtoto wake kwa zaidi ya miaka miwili. Huyu shemeji yangu alikuwa ameolewa ndowa ilivyo mshinda akahamia kwa dada yake yeye na mwanaye.

Sasa imefika mahali nikawa najiuliza nitaendelea kutuza familia ya mtu mwingine bila faida yoyote mpaka lini? Sasa siku moja nikajitia uchizi nikasema kwa vile nahudumia kila kitu basi angalau nimuombe huyu shemeji mapenzi ili nipoze machungu ya kulea mama na mtoto wa mtu mwigine.

Basi nilivyo tu jaribu shemeji akakasirika akaenda kumwambia dada yake . Sasa dada yake anasiku mbili ni kulia tu haongei na mimi hata kidogo . Watoto wnauliza baba umemfanya nini mama mbona analia sana, nashindwa cha kusema. Na mimi nimeamuwa nikae kimya siongei na shemeji wala mke wangu .

Naongea tu na watoto. Kila nikimwambia tuongee anakaa kimya na kuendelea kulia. Sasa ndio nimekuja kuomba ushauri kwenu. Najuwa humu kuna watu wengi huwenda kuna mtu kapitia changa mto kama yangu . Karibuni wote kwa ushauri.
Huyo ni mke wako unashindwa kumuomba msamaha mwambie ulipitiwa ni shetani tu . Ulikosea mwanzo kabisa ulipaswa kukataa ungemwambia huyo shemeji Yako muongo. Siku nyingine usirudie Tena huo ujinga
 
Mgeuzie kibao, kwamba yeye ndio alionesha dalili kukutaka kumbe lengo lake kukugombanisha na familia yako.

Pia mwambie mkeo kwamba kama walipanga pamoja ili walete migogoro katika nyumba iwe mwanzo na mwisho.

Ukimaliza hilo beat weka nauli mezani kwamba mpe mdogo wako hiyo nauli atafute pa kuvurugia ndoa za watu sio hapa
 
Usipokataa utadharaulika kuanzia ndani, jirani na hata ukoo wa kwao mwanamke.
Pia hayo machozi ya mke wako anayolia hapo ndani anapanga wapi akafanywe kulipuza kisasi na kupoza moyo. Trust me kuanzia sasa ndani ya mwaka huu na ujao utaona mabadiliko fulani. Lazima afanywe sehemu hao wapuuz maamuz yao huwa hayakwepeki.
 
Back
Top Bottom