Kama ni kuku mzima fanya hivi:
Mkate vipandepande muwekee kitunguu saumu kijiko kimoja cha supu kilichotwangwa,pilipili manga nusu kijiko cha chai,chumvi,ndimu.Muache masaa kadhaa viungo vikolee.Kisha mkaange.
Ukitaka kumroast muweke viungo hivo nilivyotaja juu pamoja na tangawizi kidogo kama kijiko cha chai kimoja.kisha mchemshe na maji kidogo kwanza ili viungo vikolee,kisha muongeze maji aive. Mahitaji ya roast
kitunguu 1
nyanya 5
carrot 2 zimenye,na uisugue kwenye chombo cha kusugulia carrot iwe hivi
Viazi vitano
pilipili hoho 1/2
kitunguu saumu kijiko kimoja cha chai
chumvi
mafuta ya kukaangia
nyanya ya kibati
Kaanga kitunguu kimoja kikubwa,kilichokatwa vipandepande kikianza kubadilika rangi weka hizo karoti,zikaange nazo mpaka zibadilike rangi
Weka viazi na nyanya,nyanya ya kibati pamoja na viungo unavyopendelea
Nyanya zikilainika weka supu ya kuku na kuku
Weka pilipili hoho ilokatwa vipande
Uache uchemke mpaka uwe mdikodiko,kisha epua kwakuliwa