Jamani nimeibiwa simu yangu Iringa nilikua nikitokea mbeya sasa leo imeniletea picha kwenye email yangu ya gmail kwamba kuna picha imepigwa na picha ya huyo mwizi ni hii apo je nifanyaje kumpata? kwani nilishuka tuu pale maeneo ya ipogolo kuunganisha gali ya dar kwani nilikua nawai Dar kwenye mazishi ya baba yangu mzazi sasa nimejikuta nimepoteza cm na baba mzazi pia
naomba msaada wenu jamani
picha inaweza kuwa imekua sycn kwenye account ya mwenye simu alafu ika upload kwenye dropbox..
mwenye simu akipata simu nyingine ana register same account naku retrieve data zooote
..sasa hapo kibaka atakua hajalog out chochote zaidi yakuchange chip
Umefanya uzembe sasa, maana yake hata lock screen password haujaweka!
Fanya fasta kubadili password za service zote unazotumia kwenye hiyo simu Email, FB, WhatsApp sijui unaifunga vipi account yake! Pia jaribu kwenda https://www.google.com/android/devicemanager kama ilikuwa set fresh unaweza kuiona location ya simu yako na kuifuta data zote.