Jamani napewa masharti naomba ushauri

Jamani napewa masharti naomba ushauri

Tarime one

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2013
Posts
2,246
Reaction score
1,742
Jamani kuna mdada nina mahusiano naye ingawa si ya muda mrefu,na inshort ni kama yeye ndo alienianza nikajikuta na mie namwonyesha kuwa nayaweza,sasa tatizo linalonifanya niombe ushauri ni kwamba kanasa ujauzito wangu,na kwa vile yuko safi kiuchumi na inavyoonekana lengo lake lilikua mimba kaniambia niachie ngazi na yupo tayari kumtunza mtoto peke yake,pia hataki nimwambie mtu yeyote habari hii na ananilazimisha kuingia nae makubaliano maalumu ya kutojihusisha kwa namna yeyote na mtoto atakaezaliwa kisheria ili nisiwe na haki ya kuitwa baba WA mtoto atakaezaliwa,na yupo tayari kunilipa gharama za kuipotezea hiyo mimba,nimeshindwa kumwelewa ana Maana gani?ushauri jamani.
 
Ww sio baba wa mtt...mama ndio anajua nani baba usilazimishe mkuu
 
Kwani wewe unamtaka mtoto? Halafu huyo ni mnafiki! Kama alitaka kukupotezea kulikua kuna haja gani ya kujishaua kukueleza ana mimba yako?
Angekumwaga bila sababu ya msingi akabaki na mimba yake isiyokua na baba bila wewe kujua!
Picha hiyo!
 
Yule alie kuwa anapiga yowe na makelele wakati wa tendo akawa kero kwa majirani ikabidi uwe unaenda kutafuta guest ulishaa achana naye??????????????????
 
Unaleta utata, mwambie sawa ila pesa usipokee ulipwe kwa lipi? mtoto ukifanana naye majirani watakuja kumwambia baba yako ni fulani.
 
Hiyo mimba hujamwambukiza wewe, kuna mtu anahudumia na kutunza, wewe kazi yako ilikuwa ni kutindua tu.
 
Heheh..TII SHERIA BILA SHURUTI...
 
Unatuaibisha wanaumme mkuu utaingiaje mkataba wa kupoteza damu yako?
Haya ndiyo madhara ya kudate kichwakichwa na mijimama yenye hela ndo hivyo sasa ukubali matokeo kuwa lengo la mwenzako ilikuwa ni mtoto na hizo hela ulizokuwa ukitanua mwanaumme mwenzako alikuwa anaprovide na ndiyo huyo anaenda kubambikwa mtoto!
 
Kwani wewe unamtaka mtoto? Halafu huyo ni mnafiki! Kama alitaka kukupotezea kulikua kuna haja gani ya kujishaua kukueleza ana mimba yako?
Angekumwaga bila sababu ya msingi akabaki na mimba yake isiyokua na baba bila wewe kujua!
Picha hiyo!

Tatizo natumia Nokia torch,pokea LIKE yangu asee
 
Kwani wewe unamtaka mtoto? Halafu huyo ni mnafiki! Kama alitaka kukupotezea kulikua kuna haja gani ya kujishaua kukueleza ana mimba yako?
Angekumwaga bila sababu ya msingi akabaki na mimba yake isiyokua na baba bila wewe kujua!
Picha hiyo!

huyo dada hajielewi angepga kimya
 
huyo ilitakiwa kwanza akulazimishe ulee mimba ili uikimbie..

hapo angepata mwanya wa kukukimbia na mwanae..

hongera lakini kwa kuonesha uwezo wa kuzalisha!
 
Unatuaibisha wanaumme mkuu utaingiaje mkataba wa kupoteza damu yako?
Haya ndiyo madhara ya kudate kichwakichwa na mijimama yenye hela ndo hivyo sasa ukubali matokeo kuwa lengo la mwenzako ilikuwa ni mtoto na hizo hela ulizokuwa ukitanua mwanaumme mwenzako alikuwa anaprovide na ndiyo huyo anaenda kubambikwa mtoto!

Yawezekana, Ila naamini Ile mimba kapata kwangu,naamini damu yangu haitapotea.
 
Jichukulie zako ela,tena utaje dau kubwa hasaa,uyo mtt km ni wako Luna cku mtakutana.Milima haikutani binafamu..........
 
mtishie unaenda kwa mganga kumloga mimba ichoropoke,,
 
Back
Top Bottom