PRPP synthetase
Senior Member
- Mar 16, 2017
- 193
- 80
Mimi ni kijana wa miaka 28 mkazi wa Singida japo kwa sasa nipo Iringa.
Mwaka 2018 nilikuwa Mbeya kimasomo ni mwanafunzi wa mambo ya afya katika kada ya afya. Tatizo linalonisumbua ni kuwa mwili huwa unapata msisimko kama aleji, allergy pindi nikipata joto au msisimko wa uoga.
Hali hii ilianza mwaka 2018 nikiwa Mbeya. Nilikuwa siwezi kutoka juani wala kula chakula cha moto kwa sababu ilikuwa inaniletea reaction ambayo naweza kusema ni kama aleji.
Hali hii hutoweka pindi nikikaa kivulini au kujippoza kwa maji. Hii reaction huleta vipele vidogo ambavyo huwa vinasambaa mwili mzima ila vikubwa kama upele hubakia kwenye mikono na tumboni na mgongoni huwa vipele vidogo mithili ya vipele vya msisimko wakati wa baridi.
Vipele huwa vinaota na kuwasha sana na tiba pekee inakuwa ni mimi kukaa kivulini au kujimwagia maji ya baridi ili mwili upoe na baada ya hapo hii hali inaisha hadi nirudi tena kwenye jua au nipate joto kwa kunywa chai ya moto.
Niliwahi kwenda hospitali na kupatiwa hydrocortisone cream kupaka lakini haikufua dafu na hali hiyo iliendelea hadi nilipotoka huo mkoa wa mbeya na kurudi dodoma.
Mwaka huu pia kwenye kipindi cha likizo ya corona nilikuja iringa cha kushangaza hali hii imeendelea kunisumbua na nimekosa matibabu yake.
Ombi langu kwa wataalamu specialist wa ngozi kama wapo huku naomba anayeweza kunisaidia tatizo hili kwani linaninyima raha ya maisha na siwezi kufanya kazi za mikono kwani zikileta joto tu huwa inakuwa shida.
Hali hii nimeipata baada ya kukaa mbeya na iringa.
Haijawahi kunipata katika mikoa mingine ambayo nimewahi kuishi kama Dar, morogoro, singida, pwani na dodoma.
Naomba yeyote anayeweza kunisaidia kupata msaada, iwe hapa au hata pm.
Wasalaamu!