ladyfurahia
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 14,758
- 9,589
Hay! waungwana marafiki zangu Namshukuru Mungu kuniweka hata siku hii ya leo niko mzima buheri wa afya njema, wengine hatunao leo hii kwanini mm ni nani mpaka nikawepo, jamani? hiviyo sina budi kumshukuru Mungu hata wewe rafiki yangu mpenzi wangu huna budi kumshukuru Mungu kila uionapo leo.
Wapendwa wangu wa moyoni leo tena nimekuja na jambo hili ambalo nimeonelea niliseme hapa kwenu ili tujadili na kupata ufumbuzi wa kina. labda nianze kwa kuuliza swali hili hapa: samahani kama mtaboreka wanaume wa humu mjengoni? ni hivi: hivi ni kwanini ninyi wanaume mnakuwa vicheche na mnakuwa watu wa ajabu sana kuwatenda wake zenu?
Hamuoni kuwa mnasambaratisha ndoa zenu na kuleta mitafaruku ndani ya ndoa na mgawanyikano kati ya kizazi na kizazi? Mkipenda kujibu haya kazi kwenu. Jambo ambalo nimeona niliseme ni hili kwa upande wa wanaume ambao wamekuwa vicheche hata kwangu imenitokea kwani nimejaziwa wanawake lukuki hata wengine sijui majina hao hasa nimebaki naumia ndani kwa ndani nimemuomba kaka Erickb52 asaidie jahazi hili linaingia majini kajitahidi kaka wa watu kunisaidia laikini wapi? nimeona sasa ninyi marafiki zangu mnisaidie kwa huyu mtu kwani bado nampenda na sitaki kumuacha kwani tuliahidiana mbele ya mashahidi kuwa sisi tu mwili mmoja na Alichokiunganisha Mungu mwanadamu hawezi kukitenganisha, hivyo naendelea kuvumilia tu japokuwa ni karaha na mateso ndani ya ndoa lakini bado naendelea kuwepo tu msije sema kuwa mm ni king'ang'anizi lahasha wala ni ndoa lazima niijenge japokuwa inayumba sana sasa, ugomvi, manyanyaso yamekuwa mengi, ingawaje ananipenda naye hawezi nitamkia chochote kuhusu kutalikiana kwani bado ananipenda japokuwa ananiletea wanawake humu home.
Juzi kati kwenye majira ya jioni tumekaa tunasubiri msosi akaniangalia na kunikodolea macho kisha akasema mwenyewe kupitia kinywa chake "My love barafu wa moyo wangu unataka nikufanyie nini ili uone nakupenda japokuwa nimekuwa mtu nisiyemwaminifu? maneno haya aliyatamka yeye mwenyewe kwani aliona anavyonifanyia na kunipa stress kila wakati ingawaje nilishamwambia kuhusu tabia yake ya kicheche na kutamanni wanawake wa nje. Nikamwangalia kwa macho maangavu na yenye mvuto wa mapenzi kisha nikamwambia niletee au nipe chochote upendacho, mume wangu laaziz wangu Mentor wa maisha.
Akaniangalia na kusema kuwa nitakununulia gari aina ya VITZ (sijui kama nimedanganywa hapa) ila moyoni nilijawa na furaha na nilifurahia nikamrukia na kumpa kiss la agape, kwa furaha niliyonayo japokuwa bado ANANIPENDA jamani mpaka nikasahau machungu, manyanyaso yote hapa nilipo nasubiri huo muujiza utendeke nipate kufurahi na kuwa mwenye kicheko ndani ya ndoa yangu waungwana je mmelionaje hili?
Nawatakia siku njema na kazi njema