jamani msaidieni happy | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

jamani msaidieni happy

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mujumba, May 9, 2012.

 1. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Rafiki yangu amenitumia ujumbe huu akiomba msaada, pse naomba mumsaidie, ujumbe wenyewe unasema" NAITWA happy nipo ktk wakati mgumu sana.yote niliyoyafanya leo najutia.wakati nipo secondari.nilikuwa ktk mahusiano na mkaka mmoja kwa jina Alex,kiukweli tulipenda sana ila Alex alikuwa for5 mm for6,kpnd chote icho Alex alikuwa msaada mkubwa kwangu kipesa,kimasomo,hata maradhi,ila mimi baada ya kumaliza for6 majibu yalitoka vizuri baada ya hap...o nikaingia chuo MLIMANI.Nilisoma kwa juhudi zote ila baada ya mwaka mmoja pale chuo nilitokea kumpenda kaka mmoja kwa jina Victa.na mpaka muda huu nipo ktk mahusiano nae.

  wiki iliyopita nimeenda kwakina Alex nimemwambia mm na yeye basi Alex amelia sana,ila leo hasubui kanitumia msg.kaniambia sawa happy nimekuelewa kila la kheri.nikamjibu sawa nawe pia.kwa kweli mapenz ya victa yalikuwa matamu sana Juz nilienda mlimani city na victa ila gafla nikakutana na Alex,wala sikuogopa nikamsalimia Alex mambo?then nikamtambulisha kwa victa,alex huyu mpenz wangu anaitwa Victa.alex akanijibu ok poa.baada ya hapo tukaondoka ila kwa sasa kuna tatizo kati yangu na Victa.Victa anapenda sex ya bila kutumia condom,nimemshauri tukapime kwanza jana tumeenda kupima.ila majibu sio mazuri kwan Victa ni mwathirika wa ukimwi.ila mimi niko safi.JAMAN Nataka kurud kwa Alex kwan siwez kuishi na Victa.JE UNADHAN ALEX atakubali kuwa na mimi tena????
  " mwisho wa kunukuu
   
 2. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,966
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  maskini wee Happy!!!!!!!!!!!!!!!
  "ulikimbilia kushoto ukakuta kulia kumesha bomoka".............lol
  "ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno'............
  wadosi wana sema
  "a rolling stone gathers no moss".......................
  nikuongezee na hizi
  " usiache mbachao kwa msala upitao'
  mwisho kabisa
  "baniani mbaya kiatu chake dawa"
   
 3. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  yesu wangu na maria.....
  wewe mtoto wewe .... iyo ni alert tu mungu amekupa kwamba hayo mapenzi uliyoyaparamia kwa pupa ipo siku yatakutokea puani .... tena inabidi ukapime tena maana si ulishangonoka na alex bila condomu?
  mimi nakushauri umrudie mungu .....
  achana na zinaa na tamaa za dunia hii....
  tulia kama mimi ...
  soma kwa sasa ,mapenzi yapo nenda taratibu dunia hii....
   
 4. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,674
  Trophy Points: 280
  Duh!Hongera kwa uzima wa afya,jikague ujue ni kitu gani kilikufanya uachane na na mpenzi wa kwanza!Usiniambie ni upendo!
   
 5. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  unavuna ulichopanda.... acha kuumiza hisia za watu na ujifunze kupendeka unapopendwa... otherwise, ushaharibu so chapa lapa taking into account kwamba ukimwi upo na unaua...
   
 6. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  kwakweli anahitaji ushauri nasaha
   
 7. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,966
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  well said Smile. sina cha kuongeza hapo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. promiseme

  promiseme JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2012
  Joined: Mar 15, 2010
  Messages: 2,715
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 135
  Mtumeeeeeeee! yani umeshapona hapo bado hata kukaukamshukuru mungu kakuvua hayo ndio kwanza unataka ushauri wakurejeana na awali? ebu tuliza kwanza ufikiri japo kidogo....
   
 9. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  umeona kitu hicho dada ... Dunia hii? ...loh
   
 10. mkonowapaka

  mkonowapaka JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 1,483
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  zamani nilizoea kuona Ukimwi wanapata watu wazimaa na familia zao..lets say miaka 50 na kuendelea.siku izi mambo yamekua tofaut kabisa maskini...kijana kam ahuyo hata bado hajagraduate ameathirika......what a loss to this poor nation and his family!!...am crying ooh Lord!

  kwa upande mwingine usimuache gafla ataezakufa....nenda nae tu taratibu maadam alipenda kujua afya yake kupitia wewe..usimuhukumu...ungeweza kuwa umeupata pia..kuwa mtu wake wa karibu maadam ushaiju ahali yake ni rahisi kujicontrol.
   
 11. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ushauri mzuri sana
   
 12. stephot

  stephot JF-Expert Member

  #12
  May 9, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 5,024
  Likes Received: 2,645
  Trophy Points: 280
  Pole sana,hilo ni somo kwa watu wenye papara na kukosa msimamo kwenye uchaguzi wa wapenzi and not only mapenzi hata kwenye maisha ya kawaida unatakiwa uamini kile roho yako inapenda ndicho sahihi na kama hutaweza ku-control huo mwenendo wako someday it's going to cost you.
   
 13. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #13
  May 9, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Bora uachane na mapenzi kwa muda! You don't deserve Alex's love for sure! Ulimuumiza sana bila hatia sasa yamekushinda unataka kurudi kwake?no thank you!
   
 14. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,335
  Likes Received: 2,659
  Trophy Points: 280
  Wasichana wengi wanapovuka tabaka moja kwenda jingine mara nyingi hudharau wale waliowaacha nyuma au chini. Mathalani, akipata kazi na mpenzi wake akawa bado ni mtu wa mtaani, ni rahisi huyo wa mtaani kutoswa.
  Hapa tumeona mfano hai wa Happy kumwacha Alex vile tu kafanikiwa kufika chuo kikuu na huko kakutana na Victor,so far kijana ambaye kielimu kamzidi Alex.
  Dada Happy, inampasa asubiri baada ya muda fulani upite halafu apime tena mara mbili au zaidi ili kwa uhakika kabisa athibitishe kuwa yu mzima.
  Pili, kwa heshima ya wanaume wote tafadhali Happy muache Alex aendelee na maisha yake maana awali si kwamba ulitupa tu jongoo, bali ulitupa pia na mti wake.
  Mwenyewe kwa matamshi yako hapo juu umekiri kuwa "mwaka mmoja uliopita ulipofika chuoni ulitokea kumpenda kijana mmoja kwa jina Victor"...hivyo sidhani kama kweli Alex ni aina ya mwanume ambaye kwako unaona ndiye akufahaye pamoja na mambo yote mlofanya mkiwa A-Level.

  "Majuto ni mjukuu"
   
 15. J

  JOJEETA Senior Member

  #15
  May 9, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  after ol those u hv done 2 alex i wonder hw wil u manage 2 say samahan?iz Alex a fool?sidhani kama Alex wil come back 2u again.ushaur umeshashauriwa hapo juu,katubu, mshukuru Mungu kama alivyosema smile ni bora ukawa single kwanza hata miaka mi2 hivi then utakapopata mwenzi ni vema mkapima afya zenu kwanza kabla ya kuparamiana.pole
   
 16. Shagiguku

  Shagiguku JF-Expert Member

  #16
  May 9, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 400
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45

  weeeee happy wewe, koma tena ukome kabisaaaaa utsithubutu kurudi kwa alex. maana hata hayo majibu unayodai uko sawa hayatoshi maana unatakiwa kurudi tena kupima baada ya miezi mitatu. usithubutu kurudi kumharibu alex muache aendelee na maisha yake kwa usalama wake kama kweli bado unampenda na kumthamini.
   
 17. B'REAL

  B'REAL JF-Expert Member

  #17
  May 9, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 3,107
  Likes Received: 173
  Trophy Points: 160
  dah!well said mzee...i hate people who play with other peoples feeling,inaumizaa sana na alex ni gentlemen alikubali matokeo na wewe hukusita kumtambulisha kwa victa,asee inauma sanaaa
   
 18. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #18
  May 9, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Subiri kwanza ukapime tena baada ya miezi mitatu. Upo uwezekano mkubwa kuwa nawe ni muathirika, ila titre haijafika ya kusomeka...
   
 19. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #19
  May 9, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hivi kuna wapenzi hapa duniani ambao wanatumia condom...kila siku nasikia watu wanapigana kavu kavu dah!! tutakufa wengi aisee...
   
 20. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #20
  May 9, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  yaani mawazo yangu yalikuwa kama yako, yaani mimi kwanza kwa shock niliyo nayo, IT KUD HAVE TAKEN ME EVEN A YEAR! UWIIIIIIIIIIIIIIIIIII ile kitu inatisha, sikia hivyohivyo kwa mwenzio! we happy hebu tulia kwanza, mpe nafasi huyo alex, na vikta naye usimtose ghafla, ofkoz kuwa naye karibu kumpa moyo na matumaini, na kwamba u will always b there for him, no matter what, but sio kw amapenzi tena! kuhusu alex mpotezee kwanza, muache apate muda wa kufanya maamuzi na wewe uamue yako! then afta one month am sugsesting u go again for a checkup to b sure! pole mwaya. lolest! mi ndio maana naogopa sana kucheza kibaba na kimama!
   
Loading...