jamani msaada wenu mwili wangu siuelewi..

Coach

New Member
Sep 24, 2012
1
1
Mimi ni kijana wa umri wa miaka 24, mwili wangu sijui una nini maana nihisi kama vitu vinatembea mwilini na pia naota ndoto za ajabu sana, na kiukweli mambo yangu hayaendi vizuri kila nilipangalo haliendi sawa.

Nimeshajaribu kwenda hospitali baada ya vipimo hakuku na lolote baya ila bado mwili haupo vizuri, kwasasa nina mpango wa kwenda tena hospitali nikacheki.

Ndugu zangu naombeni ushauri na msaada wenu, yapo mambo mengi ambayo nashindwa kufanya tokana na hali hii.
 
Pole xana,Mkuu nenda kaipost jukwaa la siasa pia kule members wanatembelea zaidi ingawa mods wataimove bt msg itakuwa delivered tayar..Naamini wataalamu watajitokeza hapa kutoa michango yao vuta subira..!
 
Kwa kuanzia anza mazoezi kama hufanyi hivyo tayari.

Pili, kula mboga mboga kwa wingi na matunda

Zaidi ya yote, rudi tena hospitali
 
Hivyo vitu vinavyotembea ni mwasho juu ya ngozi au vinaonekana kutembea ndani ya ngozi? Kamani ni mwasho juu ya ngozi, then unawasha muda wote au unawasha kwa muda baada ya kufanya jambo fulani (eg. kuoga, kufanya kazi ya akili, kutoka jasho, etc.)?

Jaribu kufatilia vizuri jambo/dalili zinazochochea ili hata ukimweleza daktari aweze kujua pa kuanzia.
 
Kuota vibaya na kutembewa na vitu mwilini ni vitu 2 tafauti. Hebu badili mandhari ya chumbani kwako. Toa godoro nje uanike, nunua bedsheets mpya. Fanya usafi wa nguvu.
Wewe mwenyewe uoge kwa sabuni ya kuua wadudu na uvae nguo safi ya kulalia. Then angalia kama hujaota vizuri na kulala kwa amani. Wakati mwingine unahitaji kujipa psychological treatment tu bila kwenda hospitali.
 
Nadhani hata mimi kuna wakati niliwahi kuwa na hali kama yakwako. Kuna wakati unasikia kama mwili kuweweseka bila sababu, mara vitu kama vinatembea mwilini, usiku unastukastuka mara unaota maruweruwe mara moyo unaenda mbio.. Ila mi wala sikwenda hospitali. hiyo hali ilikujaisha tu yenyewe.
 
Unaota ndoto mbaya? How? Wakati wa usiku tu ama hata ukilala mchana?!!
Mambo yako yanashindwa kwenda, unamaanisha nn hapo? Inawezekana pia ukawa na neurological au psychiatric problmz. Consult ur doc
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom