Kuna zaidi ya urafiki hapa. Kwa kipindi cha karibuni JK amekuwa zaidi kanda ya kaskazini. Ufunguzi wa tawi la CRDB marangu, Kituo cha polisi pale kibosho, uzinduzi wa KCB Moshi Branch na mazishi ya mke wa Mengi. Ziara zote hizi ni hii hiii kodi ya wananchi. Juzi jumamosi nilikuwa naelekea Arusha kikazi tena ukizingatia kuwa ilikuwa nusu siku hivyo nilitakiwa kuwahi, tulisubiri kwa zaidi ya saa moja kusubiri Mh JK apite ende pale machame kuzika. Magari yalopita pale ni zaidi ya kumi na tano hv. Tena ni yale MaVX meusi yale ya petrol cjui yale. Yanakimbia hayo cjawahi kuona. Kwa harakaharaka nikajiuliza hv huyu watu kama wabunge wa bunge lake wana kufa hajawahi kuhudhuria! Iweje leo tunamwona kwa mke wa rafiki! Kwa gharama za nani? Bado niko gizani