pole sana kaka. muhimu hapo ni kuwa na subira, muachie Mwenyezi Mungu kwani yeye ndiye mtoaji wa kila kitu. Pia usiwe desperate sana katika kusaka mpenzi kwa kuwa ukifanya hivyo utaishia hukohuko kuachana huku ukibaki na mawazo....kama una imani ya Mwenyezi Mungu, basi amini kuwa LIKUEPUKALO LINA KHERI NA WEWE...so USITHUBUTU kulazimisha uhusiano au kufuata mkumbo kisa labda marafiki zako wako kwenye stable relationships, NO! Kila binadamu ana zamu yake, tupo kwenye foleni kaka, labda wao zamu yao imefika, ya kwako bado...ebu kwa sasa jaribu kutulia tu bila kuhangaika na hawa wasichana, utashangaa kuona unampata msichana mzuri wa chaguo lako ambaye utaridhia kumfanya MKE sio girlfriend tena..kila la kheri Inshaallah!!