Jamani mimi sijielewi!!

Jamani mimi sijielewi!!

M.E.M.A

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2013
Posts
1,373
Reaction score
472
Habarini wana MMU.

Katika kujitafiti nimegundua nina tatizo ambalo silielewi. Tatizo lenyewe ni hili:
Kila mwanamke ninayemtongoza simpati anaishia kunitolea nje. Na kama tulikua na urafiki wa kawaida na wenyewe unakufa. Hata hivyo mwisho wa siku bila kuelewa imekuaje kuaje najikuta nina mpenzi ambaye sijamtongoza.
Katika hao ambao nawapata bila kuwatongoza wengi wao ni marafiki wa wale watongozwa. Yaani shabaha inamkosa mhusika na asiyehusika najikuta tu nipo naye.
Wakati nafikiria labda ni hisia zangu tu kwamba ninayemtaka simpati, mwaka jana nilikutana na dada mmoja skype na sijui ilikuwaje kuwaje hadi akawepo kwenye list ya friends wangu. Tulikuwa tukichat sana hadi akiniaga nasikitika. Baadae tulikuja kukutana Millenium Tower. Tukaongea sana na kucheka cheka kama machizi. Mwisho wa siku nikaingizia mada ya uhusiano nayo ikaua urafiki hadi leo. Kwa kweli iliniuma sana maana sio siri nilimpenda hadi basi. Mpaka leo siamini kweli kama imetokea. Japo nina mpenzi mwingine ki ukweli haipiti siku bila kumuwaza. Naangalia picha zake alizowahi kunitumia whatsap na facebook..nabaki kuumia tu moyoni.
Huyu ni habari ya siku za usoni, lakini nyuma yake kwa vipindi tofauti imekuwa ikitokea hivi hivi..ninayempenda kweli kweli simpati. Na hao wengineo imekuwa ni migogoro tuu kwa kuwa upendo ule wa dhati nakuwa sina..ila huwa najipa moyo kwamba mbele ya safari nitafall deeply kitu ambacho hakitokei.
Jamani nifanyeje? Hii ni my real personal life.
 
pole sana kaka. muhimu hapo ni kuwa na subira, muachie Mwenyezi Mungu kwani yeye ndiye mtoaji wa kila kitu. Pia usiwe desperate sana katika kusaka mpenzi kwa kuwa ukifanya hivyo utaishia hukohuko kuachana huku ukibaki na mawazo....kama una imani ya Mwenyezi Mungu, basi amini kuwa LIKUEPUKALO LINA KHERI NA WEWE...so USITHUBUTU kulazimisha uhusiano au kufuata mkumbo kisa labda marafiki zako wako kwenye stable relationships, NO! Kila binadamu ana zamu yake, tupo kwenye foleni kaka, labda wao zamu yao imefika, ya kwako bado...ebu kwa sasa jaribu kutulia tu bila kuhangaika na hawa wasichana, utashangaa kuona unampata msichana mzuri wa chaguo lako ambaye utaridhia kumfanya MKE sio girlfriend tena..kila la kheri Inshaallah!!
 
i c kaka pole sana nenda kwenye maombi kama ni mkristo i c mi namjua kuna mtu nayeye alikua hivyo hivyo yani ana roho nzuri kweli jamani lkn akikutongoza tu sijui unamuonaje hutaki hata kumsikia pole sana Mungu akusaidie umpate umpendae
 
sasa kama unaowapenda wamekataa kwani lazima kuanzisha mahusiano na hao marafiki zao. endelea subiri kakana usiingie kwenye mahusiano kama bado hujapenda, wait u wil have someday
 
this is a time to open your mind, not Legs! pole mkuu. Badilisha mfumo wa mahusiano. Hakikisha una mtongoza mtu mnaye endana, may be unatongoza watoto ama watu wenye intrest tofaut na wewe. Be strong.
 
pole inaonekana unaenda madaraja yasiyo yako matokeo yake unapata daraja lako halisi hivyo usilalamike , ridhika na hilo daraja lako
 
Tatizo lako unachagua matawi ambayo siyo yako. Wewe uwezo wako Escudo Unaenda Kuchagua Prado. Huoni kuwa unavaa viatu visivyokutosha?
 
Soma garage party ya kwamtoro kilio chako kitakwisha kabsaa!!
 
pole sana kaka. muhimu hapo ni kuwa na subira, muachie Mwenyezi Mungu kwani yeye ndiye mtoaji wa kila kitu. Pia usiwe desperate sana katika kusaka mpenzi kwa kuwa ukifanya hivyo utaishia hukohuko kuachana huku ukibaki na mawazo....kama una imani ya Mwenyezi Mungu, basi amini kuwa LIKUEPUKALO LINA KHERI NA WEWE...so USITHUBUTU kulazimisha uhusiano au kufuata mkumbo kisa labda marafiki zako wako kwenye stable relationships, NO! Kila binadamu ana zamu yake, tupo kwenye foleni kaka, labda wao zamu yao imefika, ya kwako bado...ebu kwa sasa jaribu kutulia tu bila kuhangaika na hawa wasichana, utashangaa kuona unampata msichana mzuri wa chaguo lako ambaye utaridhia kumfanya MKE sio girlfriend tena..kila la kheri Inshaallah!!

So wise yaani..asante sana
 
i c kaka pole sana nenda kwenye maombi kama ni mkristo i c mi namjua kuna mtu nayeye alikua hivyo hivyo yani ana roho nzuri kweli jamani lkn akikutongoza tu sijui unamuonaje hutaki hata kumsikia pole sana Mungu akusaidie umpate umpendae

Asante sana. Sasa inakuwaje hii au hampendi watu wa pole? Kwa kweli nimewahi kufunga na kuomba hadi nikapata hypoglycemia. Sijui kwa kweli what next.
 
sasa kama unaowapenda wamekataa kwani lazima kuanzisha mahusiano na hao marafiki zao. endelea subiri kakana usiingie kwenye mahusiano kama bado hujapenda, wait u wil have someday

Ndugu haiwi lazima..inatokea tokea tu hata sielewi yaani.
 
Kama umesha jitambua hivyo inabidi uwe makini sana.Huenda kuta hujui jinsi ya kuongea na mwanamke ili umvute vizuri awe karibu nawe na hata mwishoe mpendane yani kila mmoja ampende mwenzie.
 
this is a time to open your mind, not Legs! pole mkuu. Badilisha mfumo wa mahusiano. Hakikisha una mtongoza mtu mnaye endana, may be unatongoza watoto ama watu wenye intrest tofaut na wewe. Be strong.

Mkuu labda niwe sijakuelewa. Legs how?
 
Back
Top Bottom