jamani kuishi na watu kweli kazi

Latifaa

JF-Expert Member
Jan 18, 2012
501
257
Watu wazima wenzangu watanielewa ukubwa jalala ukubwa shimo la choo, kuishi na bidamu kazi jamani nimechoooka!
 
Pole mrembo. Kuna kanga mnazovaa zinaandikwa " mama nipe radhi kuishi na watu kazi" .


Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
 
Mbona wengine hatujakuelewa, umechoka kuishi na watu kwa maana hiyo unataka kujiua ili usiishi nao au unamaanisha nini? Ila pole eeeh!!!
 
Ndio kusema ulikua unaishi zenji?. Pole, ni upepo tu huo, utapita.
 
Watu wazima wenzangu watanielewa ukubwa jalala ukubwa shimo la choo, kuishi na bidamu kazi jamani nimechoooka!

Kazi ni msingi wa maendeleo hivyo kuishi na watu ni maendeleo. Mbona kuwa wengi wanatafuta kuishi na watu?
 
pole mwaya! vinachoshaje sasa?? kuna saa unatamani kuishi na mnyama ujue moja! lolest.
 
Ni kazi kama ukitaka umfurahishe kila mtu,HUWEZI KAMWE!
 
sheria ya kuish na mtu yyte iko hivi
1) muheshimu hata kama ni mdogo kwa nafasi yake
2) usimbague wala kunyanyasa, wala kumdharau yyte yule
3) tenda wema mara nyingi kuliko utendewavyo wewe.
4) usisubiri shukurani kwa wema wako wala usingojee hisani kwa jema lolote
5) fanya kila jambo kwa mtu pasi unafiki wowote ule kama hutaki sema sitak na kama ndiyo sema ndiyo
6)usiwe mwepesi wa kusema wala kulalamika, bali mwepesi wa kusikiliza.
7) siyo kila unachoisikiliza kiusemeshe moyo, hapa utakufa kwa presha na sukari
8)usitake mtu akujue ulivyo asijue undani wako yaani uwe msiri na mambo yako.
9) tambua kuwa siyo wote wanaokupenda, so usilaumu unapoonyeshwa kutokukubalika kwenye nafsi za watu wengine.
10) kamwe usikatishwe tamaa na matendo, maneno ama mitazamo ya watu.
11) fanya mara nyingi uwezavyo kile moyo wako upendacho usiulazimishe moyo.
12)shirikiana na wenzio katika mambo yote ya kaijamii.
13) kamwe usitie fitina kwa jambo la heri au la shari

Kubwa kuliko yote sali sana ili uongezewe hekima ya kuisha na watu na pia upendo kwako uwe ni silaha yako.
 
Back
Top Bottom