Baada ya kipigo tulicho kipata mashabiki wa SPAIN, leo nimeendelea na utafiti wangu ulio anza juzi na leo asubuhi kwa uchungu nimefikia kikomo.Nilikua nafanya utafiti kujua mabinti wengi wanapenda timu ya Taifa ya nchi gani?, na kwa nini?. Utafiti wangu nimeufanya hapa UDOM na nje ya chuo (mjini).Matokeo ni kuwa mabinti walio hojiwa UDOM ni 124 na mabinti 84 wakadai wao wanaipenda Brazil,16 wao wakedai wanaipenda Egland,8 waipenda Ujeruman,6 waipenda Spain,10 wao hawajui kuhusu mpira wa miguu.Kwa wale wa nje ya chuo 78% ya mabinti walio hojiwa walionesha mapenzi kwa timu ya taifa ya BRAZIL. Kwa kweli sikupata sababu za msingi kwa nini wanaipenda BRAZIL, hebu na wewe njo na timu yako unayo ipenda na sababu za kwanini unaipenda. Hii ni kwa wote.