Jamani kina mama kwanini mpo hivi?

Pia, tambua mchango wa mzazi katika malezi ya mwenza wako mtarajiwa, ni yeye mzazi alimfanya huyo mwenza afike hapo alipofika hadi wewe ukamuona kwamba anafaa kuwa mwanandoa mwenzako. Kama mzazi, amepitia mengi katika kumlea, hivyo heshimu maamuzi yake, usimbeze na wala usimdharau mkweo mtarajio.

Yani maamuzi kama hayo ya kunipangia budget ndani ya nyumba yangu na kutengeneza ukuta kati yangu na mume wangu bado tu niyaheshimu kisa eti huyo ndo mama ake na amehangaika na malezi? Hivi kwa nini mara nyingi wamama wa watoto wa kiume ndo wanapenda sana kuingilia ndoa za vijana wao? Mama zetu sisi mabinti hawana mchango kwenye malezi yetu, kwa nini wao wanaziheshimu ndoa zetu?? What's so special na wamama wa vijana compared na wamama wa mabinti?
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Back
Top Bottom