Jamani kina mama kwanini mpo hivi?

Usikute huyo Mama wa huyo kijana alimuahidi shoga yake kuwa mwanaye atakujaoa mtoto wake, ndiyo maana Mamaa anachemka kwa kupiga mkwara.
 
Kwa nini ulazimishe kuishi na mtu ambaye mzazi wake hakutaki? Kwani ndio imefika mwisho wa dunia kwamba usipokuwa na huyo basi na maisha nayo yanasimama?

Kubali matokeo usilazimishe kuwa mahali ambao hukubaliwi. Kila kitu hupangwa kwa baraka za Mungu, hata kupata baraka za wazazi wa mwenza wako nalo ni suala la baraka za Mungu. Kama Mungu yuko upande wako, basi kila kitu kitaenda sawa. Lakini usithubutu kulazimisha ndoa au uhusiano ambao huna baraka za wakwe zako, eti kisa mwenza anakupenda! Kwa mila na desturi za Ki - Tanzania, ndoa ni zaidi ya mke na mume, inahusisha wakwe, mawifi, mashemeji na koo zote mbili za Bwana na Bibi Harusi, hivyo suala la kupata baraka za mkwe halina mjadala, lazima upate baraka zao. Usilazimishe, mambo mazuri hayataki nguvu wala kulazimisha, ukiona hukubaliwi mahali basi kubali matokeo kwamba Mungu kwa hili hakuwa upande wako, songa mbele yawezekana Mungu amekuandalia mwenzako mwingine siku za usoni, na sio huyu au labda wakati wake bado haujafika.

Pia, tambua mchango wa mzazi katika malezi ya mwenza wako mtarajiwa, ni yeye mzazi alimfanya huyo mwenza afike hapo alipofika hadi wewe ukamuona kwamba anafaa kuwa mwanandoa mwenzako. Kama mzazi, amepitia mengi katika kumlea, hivyo heshimu maamuzi yake, usimbeze na wala usimdharau mkweo mtarajio.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
wakati mwingine mama yangu akisema huyu mke hafai huwa namsikiliza.... nina imani mama hawezi kunipoteza ameona mbali..!
 
yani mimi mwenzenu ndo mana kujulikana upande wa mwanaume wakati tuna date nilikuwa sitaki hata kusikia, siku ya kwanza kabisa kuonwa na ndugu wa mwanaume alienioa ni siku wamekuja kuleta mahari napo waliniona kwasababu ilikuwa pia ndo siku ya sherehe ya engagement, lakini isingekuwa ile engagement party wangenionea ukumbini, na kwa kuwa kwa mila zao wazazi wa mwanaume hawatakiwi kuja siku ya mahari basi wakwe zangu waliniona kwa mara ya kwanza ukumbini siku ya sendoff na mimi ndo mara kwanza kuwaona, lakini hao mawifi na mashemeji mara kwanza tunaoana ni kwenye mahari basiiii mara pili kuonana nao ikawa kwenye sendoff na harusi baaasi.
hufai unaficha makucha..!
 
Salama jamani kama uzi unavyojieleza hapo kuna rafiki yangu wa kike kapata mchumba na wanamtoto mmoja hadi saivi mipango ya ndoa wanayotoka siku nyingi Ila tatzo ni mama wa mchumba wake(mama mkwe) hamtaki na hanasababu ya msingi zaidi ya hamuendani,binti mbaya,mara anatabia mbaya na zingine tu za ajabu ajabu na wameshindwa kufanya mipgango ya ndoa coz itakuwa ndoa ya ajabu mama mzazi anasema hata kwa mtutu hawatapata baraka zake labda wafunge akishatoka dunian ila kwa upande wa wazazi wa binti walikuwa tayari kwa ndo ila sasa nao hawataki wanasema hawataki binti yao hakateseke bure ila binti na jamaa wanapendana sanaa tu Naomba kuwauliza wazazi hasa kina mama ni wakwe wa aina gani mnawataka Maoni na ushauri unaruhusiwa kwa ajili ya huyu rafiki yangu kipenzi

Wao wanahitaji baraka ya mama au baraka za Mungu?

Lakini inategemea sana ni SABABU ZIPI zinazomfanya huyo mama amkatae binti.

Mara nyingine wazazi wanakuwa na sababu za msingi sana ila viburi vyetu na kujifanya tunajua zaidi vinaweza kutuponza.

Lakini kwasababu tu ya "eti ana sura mbaya" huyo jamaa asimwache huyo binti.

Kama wote ni Wakristo wamwombe Mungu awatetee watafika tu.
 
Back
Top Bottom