Nyie waganga njaa hamkosi cha kusema; kwani tatizo lilikuwa wapi? Serikali yote ilikuwepo Arusha na wote walitekeleza majukumu yao chini ya maelekezo ya Raisi mlitaka ajigeuze upepo?
Chama
Gongo la. Mboto DSM
Ndg wanajamvi,
Kama ulivyo usemi wa wahenga wetu kuwa "mnyonge mnyongeni lakini haki take mpeni" Nijuzi baada ya mlipuko wa bomu kanisani huko Arusha, Rais Kikwete alikuwa ziarani nje ya nchi kama kawaida yake ya kutotulia nchini kwake lakini baada ya kutaarifiwa janga hilo la bomu, aliamua kukatisha ziara yake na kuacha malengo yake yote ya ziara hiyo na kurudi nyumbani kushirikiana na wananchi wake katika mkasa huo.
Kweli huo ni uzalendo na ninashauri vyombo vya habari viliweke wazi jambo hilo kwa watanzania kama vilivyokuwa vinaweka wazi pale marais waliomtangulia JK walipokuwa wanaendelea na mambo yao nje ya nchi wakati watanzania wanumia bila msaada. Mfano wakati wa mgomo wa madaktari muhimbili na wakati huo Raisi yuko majuu miaka ileeeeee!!!!
Unajua kuna watu kazi yao kukosoa tu,rais ana majuku mazito ya kuliongoza taifa hili,ndio maana kuna amani,hivi mtanapotoa lawama rais kafanya hiki mara kile mnapata nini,unajua mtu yeyote asiye nashukrani ukifuatilia utaona ana matatizo lukuki,nakushukuru uliyeleta hii thread hapa javini,na kumpongeza raisi wetu.
Wewe unayeona rais hafai ondoka nenda kaishi nchi nyingine utakapo mpata rais anayefaa zaidi ya huyu tuliyenaye.
Watanzania lazima tubadilike tufanye kazi tuache kutoa lama kila kukicha,hii ni dalili ya uvivu wa kufikiri.
Kikwete ni rais bora,huo ndio ukweli wa mambo.
Lokissa
Wewe ni veteran wa waganga njaaa humu JF unafahamika sana; huna jipya wala huninyimi usingizi; Kikwete mtamuota sana hamkosi la kusema hata sishangazwi sana na hilo hiyo ndiyo ajira yako; leo umevuta ngapi mpaka dk hii?
Chama
Gongo la mboto DSM
Mkuu unaendelea kujichanganya hapa tunajadili siasa; kazi unafanya mpaka ushindwe kujihusiha na siasa? Siku mapadri; mashekhe wote tunao kwenye siasa; mkuu njaa yako sema nayosina njaa ndugu wala sijawahi kuishi kwa mgongo wa mtu au chama
sina haja ya kukuwekea post nilizosifia serikali
we are not in court and Im not ablidged to so.
kazi yangu hainiruhusu kuwa mwanasiasa
lakini hainikatazi kukosoa maovu ya CCM au Chadema.
na hainizuii kutoa maoni.
kwa hili sitaweza kuwa mnafiki kumpngeza JK,ingekua ndivo kama angerudi j2 ile ile
karibu Ngaramtoni uone kilimo kwanza sio kupiga debe hapo dar ili uwahi Lumumba.
Nyie waganga njaa hamkosi cha kusema; kwani tatizo lilikuwa wapi? Serikali yote ilikuwepo Arusha na wote walitekeleza majukumu yao chini ya maelekezo ya Raisi mlitaka ajigeuze upepo?
Chama
Gongo la. Mboto DSM
Wana jamvi naomba tuwe watu wa kufikiri,
hivi ni nani kati yenu ambaye mtoto wake akiwa mla unga wa mda mrefu na baadae akaamua kucha asimpongeze?
Je mtoto akiwa mwizi na akaamua kuacha humpongezi?
Marais wa nchi hii hawakuwahi kufanya tendo alofanya JK la kurudi home kabla ya kukamilisha ratiba yake Kuwait, hata kama aliwahi lisaa limoja tu, bado ni element ya utafauti na watangulizi wake (isipokuwa Mwalimu) na kuonyesha mabadiriko kidogo.
Naomba nitambulike wazi kuwa mie sio muumini wa JK na wala hakuipata kura yangu na wala siutarajii u DC!!!
Kama aliondoka saa 12 asubuhi badala ya saa 2 usiku atakuwa amekatisha ziara kuna hafla nyingi angezifanyaSoma vizuri mawazo ya wachangiaji.kinachopingwa hapa siyo kutofika kwake haraka arusha,ila ni ile kutuhadaa eti alikatisha safari wakati siku 2 za ziara yake ziliku wa zimeisha hatudanganyiki!
Hakika huu ni mfano mfu, yaani unadhani uchungu wa JK kwa wale waliokufa kwenye mlipuko wa bomu ni sawa na angefiwa na Riz1? Angekufa Riz1 hiyo ndege ingepiga riverse angani..! Utakuwa umesahau kuwa ''Damu ni nzito kuliko Maji''Hebu fikiria wewe ni Baba wa familia, ukawa uko safarini mkoa au nje ya nchi. Ukapata taarifa kuwa nyumba yako imeungua au bahati mbaya mwanao amefariki. Kama utaachana na safari yako na kurudi nyumbani, utapongezwa kwa kuijali familia yako au utakuwa unatekeleza wajibu wako ulioahidi siku unafunga ndoa ?
Kama aliondoka saa 12 asubuhi badala ya saa 2 usiku atakuwa amekatisha ziara kuna hafla nyingi angezifanya
Chama
Gongo la mboto DSM