Jamani huu ualimu mbona karaha namna hii?

Jamani huu ualimu mbona karaha namna hii?

Nenda CWT hapo ulipo wape madai yako ukitoka ingia TSD wape madai yako na utapewa taratibu za kufata ila kifupi huwez hamishwa bila kulipwa! Komaa tsd mpk kieleweke wakikusumbua zaid tafuta namba ya katibu mkuu CWT taifa mpigie na mweleze! Kwakuwa wameamua kupambana na weww na we pambana nao! Tatzo walim wengi huwa hamjui sheria za kazi zinazowalinda! Nakuapia ukikomaa watatengua uhamisho wako kwani hawana pesa za kuchezea kukulipa! Ukishindwa nifate private nikusaidie! Niko Tamisemi


asante mkuu, nitakutafuta privately
 
hivi mkuu bado una imani na hawa wahuni CWT? kuna mwalimu yeyote unayemjua ambaye amesaidiwa na CWT?

Wapo wengi sana cha msingi fata protocol wasipokusaidia wilayani wapigie makao makuu watoe order
 
acha ujinga kijana unamkimbia mtu, nilidhani mshahara hautoshi, akihama je? wewe hukusoma sekondari ya kata mbona unaongea kilofalofa..sekondari zote za serikali baada ya kikwete ni za kata, we ulisoma wapi?
 
Pole sana mwalimu,walimu njooni Whatsapp hapa 0782774308 tushauriane private,,mada za hapa zinatugusa sana,chukua namba hiyo kabla Mods hawajatoa,hawapendi walimu tushauriane nje na hapa
 
Lofa wewe!unamkimbia mtu alafu iweje?achana na huyo Mkuu tafufa mikukuta yako fanya acha ujinga.Siku izi walimu wamekuwa watu kunug'unika tu,tutafute ela hiyo kazi ndo inaniweka hapa mjini.
 
Mwalimu acha majungu kazini chapa kazi ulizopangiwa. Baada ya muda wa kazi jishughulishe na uzalishaji mali.
 
Mmh hapa mkuu kama tupo kituo kimoja na mimi maana hayo yote ndiyo anayo mkuu wetu hapa....daah kumbe tupo wengi
 
Rejea standing orders, usihamishwe kama mzigo ndg wakulipe.....kuwa jasiri na wakikusumbua fungua mgogoro CMA wawajibike.
 
mm sio mwalim ila ukinifanyia hivyo nakuwa mtu wa kusaini na kwenda kumwagilia miwa yangu shambani ..hahaaaa
 
Tatizo nyie mnaoingia kwenye fani huwa hamjiandai KISAIKOLOJIA kupambana na changamoto za kikazi pindi mnapoajiriwa
 
Ualimu sio baba yako wala mama yako.

Timiza wajibu wako potea.

Kafanye mambo yako achana na huyo mkuu wa shule .

Tatizo mnakuwa serious sana na hiyo kazi kana kwamba kuna posho mnapewa nje ya mshahara njiwa
 
Ualimu sio baba yako wala mama yako.

Timiza wajibu wako potea.

Kafanye mambo yako achana na huyo mkuu wa shule .

Tatizo mnakuwa serious sana na hiyo kazi kana kwamba kuna posho mnapewa nje ya mshahara njiwa

mkuu nimekuelewa sasa tatizo huyu h/m wetu ni mtu wa aina yake, hapendi kuona umetoka shulen hata kama umemaliza vpndi vyako. anapenda kuona unapata shida umwelezee ili akukudharau na kukubeza

kifupi si mtu wa fadhira njema regardless umefanya jema au baya
 
Hizi mada za ualimu zimenigusa sana. ok mimi pia ni mwalimu katika halmashauli fulani. Mambo yanayonipata inafikia hatua natamani niachane tu na hii kazi

Ni hivi, baada ya kumaliza kujaza mikataba nilipostiwa kuanza kazi katika shule flani ya kata. Tulichokikuta huko sijawahi kukiona katika shule yoyote.

Aisee kwanza shule ilikuwa na walimu 7 tu ila maajabu mkuu wa shule ndo kila kitu, yeye ndo mtaaluma, mwl wa chakula na mengineyo mengi. Hakuna cha school balaza wala nini. Kwenye vikao yeye ndo msemaji mkuu na hakuna kupingwa.

Tumefight sana kuadjust lakini mwisho wa siku aligawa madaraka japo kwa shida sana lakini anapokupatia unakuwa huna full mandate na kitengo chako utafuatilia mpaka uone kero. Mfano mwl wa taaluma hana uwezo hata wa kwenda kuchapa mitihani yeye kazi yake ni kuandaa ratiba tu.

Mbaya zaidi amekaa muda mrefu kwa hiyo amewaaminisha wanafunzi na wazazi kuwa shule ni yake na hakuna mtu wa kumhamisha hivyo wanafunzi wanamheshimu yeye pekee, wanadharau walimu wengine utafikiri wanafunzi wenzao tu na ukiwaadhibu kama yeye hayupo basi akirudi watakusemea kwake na asivyo na busara utaitwa mbele yake kuhojiwa.

Hayo ni machache tu lakini kisa kikubwa kilicho nifanya niandike uzi huu ni hiki,,

Baada ya msuguano wa hayo yote walimu wote tulikubaliana kumwomba afisa elimu kuwa atuhamishie huyu mkuu ikiwezekana watuletee mwingine

Kwa shinikizo kubwa afisa elimu alituma "tume yake" kuja kuchunguza tulichokuwa tukipinga. Ilivyo ondoka tuliambiwa tutapewa feedback.

Cha ajabu ni kuwa siku ya kufunga mimi sikuwepo nilikuwa na matatizo hivyo nilikuwa na ruhusa. Habari waliyopewa ni kuwa mimi nimehamishwa kituo cha kazi na wengine watafuata. Na sitalipwa usumbufu wa aina yoyote ile kwa kuwa ni matatizo tumejitafutia sisi. Kwa hiyo gharama ya kusafirisha mizigo yangu itakuwa juu yangu, Mbaya zaidi aliwazuia walimu wezangu wasinipe taarifa hizi, japo kuna huyo mmoja kanipenyezia.

Yeye kama mkuu hajaniambia chochote hivyo ni kama chini ya kapeti.

Samahani kwa uzi mrefu wakuu, ila hapo nimejitahidi kufupisha na naombeni mchango wenu ,hivi ni kweli unaweza kuhamishwa kwa jeuri namna hiyo alafu ujigharamikie kwa uhamisho ambao hujauomba?? Kweli jamani??

Kama ni kweli nafikiria kuchukua maamuzi magumu...najua kitaa maisha ni magumu sana lakini.... HUU NI ZAIDI YA UONEVU

MAWAZO YENU TAFADHALI.

waambie sina hela ya uhamisho,usikubali kuhamishwa bila kulipwa unless umeomba mwenyewe
 
Tatizo mlishawaona wakuu wa shule miungu watu,piga mangumi huyo headmaster atakuheshimu,usimpigie shuleni mtegee yupo bar
 
Kuna wakuu wengine hawajitambui. Ni sawa na majipu tena yenye mabawa. Wamejimilikisha shule za umma, siku hizi maafisa elimu wapo chini ya wakuu wa shule kwa shule zenye ulaji hivyo ukiwapelekea malalamiko, unakuwa unawapelekea ulaji. Serikali iangalie utendaji wa hawa wakuu wa shule na mikataba yao. Mkuu wa shule kukaa shule moja kama mkuu wa shule kwa zaidi ya miaka kumi ni uzoroteshaji wa elimu katika shule hiyo.
 
Niliajiriwa mwaka jana, siku moja kwenye kikao cha walimu, mkuu akasema " nyie walimu wapya ni mavi tu, hamna kitu kichwani"
niliumia sana, Yule mkuu alikuwa anaweza kuropoka tusi lolote tu.
Nilifight nikapata kazi ya uT'A Udsm, sasa nafanya masters hapa G?ttingen university ( Germany). Uwa nikikumbuka ule udikteta na ushenz nnahis kutapika. Sijui kwann wanajisahau?
 
Back
Top Bottom