Jamani eeh kutembelea iran ni tatizo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani eeh kutembelea iran ni tatizo?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by hashycool, Oct 16, 2010.

 1. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  Katika kipindi cha hivi karibuni nilikuwa Dubai kwa mambo kadhaa ya mabusiness, na kwa bahati mbaya kabla sija maliza kile kilichonipeleka pale muda wa visa yangu ukawa umeisha hivyo kutakiwa kutoka nje ya nchi.Kutokana na gharama kuwa kubwa za kurudi nyumbani halafu tena kurudi Dubai wataalam pale wakanishauri niende nchi ya jirani kwani visa haingechukua muda kwahiyo ingepunguza gharama,hivyo ikanibidi niende Iran ambako nilikaa kwa siku 5 kisha kurejea tena Dubai. Tatizo sasa; nilipo tua tu JK International airport watu waliojitambulisha kuwa ni usalama wa taifa wakanivuta pembeni baada ya kuangalia pass yangu na kukuta muhuri wa iran ikawa nongwa,niliwekwa chini ya ulinzi na kuanza kuhojiwa kuwa nilikwenda iran kufanya nini.. nilijitahidi kuwa elewesha kuwa nilikwenda kwa ajili ya visa change lakini hakuna aliye nielewa hivyo nikawa mtuhumiwa wa madawa ya kulevya wakisema kuwa nitakuwa nimeyabeba tumboni, walinifanya mbaya sana lakini at the end of the day hawakukuta kitu lakini badowakaendelea kunishikilia, mwishowe alikuja askari mmoja na kuiambia nieleze kama nina madawa ya kulevya ili ajue ni jinsi gani ya kunisaidia..baadae akaenda straight to the point na kuniambia kuwa niwape dola 2000 iliwaniachie. Nikaendelea namsimamo wangu ule ule kuwa mimi sio dealer na wala sijawahi hata kuyaona hayo madawa ya kulevya. Baadae walipoona sina dili ndipo wakanilazimisha niwape dola hamsini ya maji iliwaniachie kwakuwa nilikuwa nimechoka sana baada ya safari ilibidi niwape hiyo dola hamsini ili kupunguza usumbufu. Hali hiyo hiyo imeshanikumba pia katika viwanja vingine vya Nairobi na Zanzibar. Najuta kwenda Irani natamani kuchana page ya ule muhuri!
   
 2. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  pole sana mkuu ukweli ni kwamba akuna ubaya kwenda iran ila tatizo ni hiyo biashara haramu inayofanywa uko ivyo kufanya usalama wahisi umetoka kuchukua madawa ila ulitakiwa ucwape rushwa alafu hicho kitu kibaya walichokufanya hapo kwenye red ungeshea na ss tujue mkuu
   
Loading...